24-0114 Yeye Aliye Ndani Yenu

UJUMBE: 63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waamini wenye Imani Kamilifu,

Kila siku mioyo yetu inaenda mbio kwa matarajio makubwa. Tunangojea ile saa ifike ya kule Kuja Kwake hivi karibuni. Hofu zote zimetoweka. Hakuna kujiuliza-uliza tena, “Je! sisi ni Bibi-arusi Wake”? Imetiwa nanga ndani ya mioyo yetu zaidi ya hapo nyuma, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE.

Tumeshikwa katika hali ya Kimbinguni, tukisikiliza huduma ya Yesu Kristo, aliyefanyika mwili upya katika Kanisa Lake. Ujumbe huu umethibitishwa kotekote na Neno la Mungu, hivi kwamba hawezi kuwa ni mwanadamu, haina budi kuwa ni Mungu akinena mdomo kwa sikio na Bibi-arusi Wake.

Sisi tunaamini si mwanadamu anayenena nasi kwenye kanda hizi, ni Mungu.

Ninachojaribu kusema, “Usife moyo.” Usimruhusu Shetani akuambie ubaya kunihusu mimi; sababu ana mengi. Bali wewe shikilia matumaini hayo; sababu, usipoyashikilia, haitatendeka. Usiniangalie mimi, kama mwanadamu; mimi ni mwanadamu, nimejaa makosa. Bali tazama yale ambayo ninayosema kumhusu Yeye. Ni Yeye. Yeye Ndiye.

Yakubidi kuamini na kuwa na matumaini katika yale ANAYOSEMA, LA SIVYO HAITATENDEKA. Hatumwangalii nabii wa Mungu kama mwanadamu, kama wengi wanavyofikiri tunafanya hivyo. Tuko nyuma ya pazia la mwili wa mwanadamu, na yote tunayoyaona na kusikia ni Mungu akinena kupitia midomo ya mwanadamu, NA TUNAYO MATUMAINI NA KUAMINI KILA NENO.

Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo kwa ajili ya siku hii. Kuamini kuwa ni Mungu, si mwanadamu, anayenena kwenye kanda. Ukilikosa jambo hilo, rafiki, umeukosa Ujumbe wa wakati huu na huwezi kuwa Bibi-arusi.

Shetani anaweka fasiri yake kwenye jambo hilo, na asilimia 99% ya wakati ananukuu Ujumbe kama tu vile alivyomfanyia Hawa, bali Hawa aliamriwa kukaa na Neno; yale Adamu aliyomwambia ndio Mungu aliyosema, si yale ambayo mtu mwingine aliyosema ati yalimaanisha. Hawa alipaswa kukaa na Sauti ya Mungu.

Hii ndio siku iliyo kuu ambayo ulimwengu umewahi kujua. Maisha ya Yesu Kristo, yale aliyoishi na kujifunua Mwenyewe katika maisha ya nabii Wake, sasa yanaishi katika mwili ndani YETU, Bibi-arusi Wake.

Tunafanya vile hasa Yeye alivyotuamuru kufanya: kukaa na Neno kwa kukaa na Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ndio huduma ya kanda ya Mungu na mpango wa Mungu wa siku hii.

Ikiwa kweli unaamini William Marrion Branham alikuwa ndiye malaika-mjumbe wa saba aliyechaguliwa na Mungu, yule ambaye Mungu alimchagua kunena na kufunua siri zote zilizofichwa katika Neno, aliye Sauti ya Mungu kwa kizazi hiki, mtu aliyekuwa na imani kuliko mtu mwingine yeyote yule, yule ambaye malaika wa Bwana alimwambia “ikiwa utawafanya watu WAKUAMINI, hakuna kitu kitakachosimama mbele ya maombi yako”, basi Jumapili hii itakuwa siku kuu kuliko.

HAKUNA KITU ambacho kinachoweza kamwe kuuondoa Ufunuo wa Ujumbe Huu kwetu sisi, HAKUNA. Hatuwezi KAMWE kuutilia shaka. Kama Yeye aliusema, sisi tunauamini. Huenda tusiuelewe Wote, lakini tunauamini hata hivyo.

Yesu mwenyewe alituambia: “Yeye aliye ndani yenu ni mkuu kuliko yeye aliye katika ulimwengu.” hebu hilo na lizame mioyoni mwetu. Roho Wake anaishi ndani yetu. Je, twaweza kulishika hilo? Sasa hivi, unaposoma Barua hii, Roho Mtakatifu, Mungu Mwenyewe, Nguzo ya Moto, anaishi na kukaa ndani yetu? Tunajuaje kuwa hiyo ni kweli? MUNGU ALISEMA HIVYO!!

Shetani anaendelea kutuambia kwamba sisi ni watu walioshindwa. Na yuko sahihi, ndivyo tulivyo. Anatukumbusha, hatupo mahali tunapotakiwa kuwa katika Neno. Sahihi tena, hatuko. Tunafanya mambo tunayojua vyema kuliko kuyafanya. Tusamehe Bwana, yuko sahihi.

Lakini hata pamoja na makosa yetu yote, madhaifu yetu yote, kushindwa kwetu kote, haibadilishi ukweli wa mambo, SISI NI BIBI-ARUSI. TUNAAMINI KILA NENO!

Hatujitazami sisi wenyewe ama chochote tunachoweza kufanya, sisi ni mchafuko. Sisi tunajua tu kwamba Yeye alituchagua na kutupa Ufunuo wa Neno Lake na hakuna kitu kinachoweza kuuondoa Ufunuo huo kwetu. Huo umewekwa ndani ya mioyo na roho zetu.

Yeye alituambia inatupasa kuwa na IMANI KAMILIFU. Tunayo Bwana, IMANI KAMILIFU katika Neno Lako. Tuna imani katika Yale Nabii Wako aliyosema kuwa ni Bwana Asema Hivi. Si neno lake, bali Neno lako kwetu sisi.

Nabii Wako alituambia chochote tunachohitaji, kama tu tutaamini, na kuwa na imani katika Neno Lako, tunaweza kupata chochote tunachohitaji. TUNAAMINI.

Bwana, ninalo hitaji. Ninakuja mbele Zako nikiwa na imani yote niliyo nayo katika Neno Lako, kwa maana haiwezi kushindwa. Lakini leo, Bwana, siji mbele Zako nikiwa tu na imani yangu, bali na imani uliyompa malaika-mjumbe wako wa saba mwenye nguvu.

Ee Bwana Mungu, nakuomba uturehemu. Na jalia kila mwanamume na mwanamke ambaye ameketi sasa, ambaye ana namna yo yote ya maradhi au mateso; na kama vile Musa alivyojitupa mwenyewe katika pengo, kwa ajili ya watu, usiku wa leo ninaweka moyo wangu mbele Zako, Bwana. Na kwa imani yote niliyo nayo, ambayo iko ndani Yako, ambayo Wewe umenipa, ninawapa.

Nami ninasema: nilicho nacho, nawapa wasikizi hawa! Kwa Jina la Yesu Kristo wa Nazareti, kataeni magonjwa yenu, kwa sababu Yeye aliye ndani yenu ni mkuu, kuliko huyo Ibilisi anayejaribu kuyatwaa maisha yenu. Ninyi ni wana wa Mungu. Mmekombolewa.

Imekwisha. Neno Lake haliwezi kushindwa. Chochote tunachohitaji, tunaweza kukipokea.

Njooni muungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki) kupokea baraka hii kuu na upako kutoka kwa Mungu pindi sehemu ya Bibi-arusi watakapokusanyika kutoka duniani kote kusikiliza Sauti ya Mungu akiweka IMANI yake pamoja na IMANI yetu.

Ndugu. Joseph Branham

63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu