22-0626 Yeye Aliye Ndani Yenu

UJUMBE: 63-1110E Yeye Aliye Ndani Yenu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Imani kuu sana,

Ninajua hii ni barua rahisi tu yenye sarufi isiyofaa, lakini nataka ulimwengu ujue ya kwamba tunaamini kila neno ambalo nabii wetu alisema na kulikubali kuwa ni Bwana Asema Hivi . Tunapomsikia yeye akisema jambo fulani kwenye kanda, tunaliamini, tunalikubali, na kisha tunalipokea kibinafsi kuwa ni Mungu Mwenyewe akizungumza nasi moja kwa moja.

Imehubiriwa, na kuthibitishwa kwelikweli kwa Neno la Mungu, ya kwamba isingekuwa ni mwanadamu, haina budi kuwa ni Mungu.

Tunaamini ishara zilezile za kuonekana dhahiri kimwili zimetukia duniani leo ambazo zilitukia wakati Yesu alipokuwa hapa. Nguzo ile ile ya Moto ambayo Mtakatifu Paulo aliiona ikiwa na Tabia ile ile, ikifanya jambo lile lile, imekuja katika wakati wetu. Ni Mungu anazungumza nasi moja kwa moja:

Ishara zile zile za kiroho ambazo alijitambulisha Mwenyewe kama Masihi, zimemtambulisha leo. Yeye yungali ni Masihi !

Unaweza tu kupokea baraka hizi kuu IWAPO unaamini kila Neno kwa kubonyeza Play ni Bwana Asema Hivi. Ikiwa wewe ni mtu ambaye huamini hivyo, na yakubidi uamue kiakili au kwa kupitia mtu fulani anayekuambia: “Hili ni Neno la Bwana, na hili ni Ndugu Branham tu anayezungumza,” basi hili si kwa ajili yako.

Katika wakati ule Musa alipowaongoza wana wa Israeli, alikuwepo mmoja, huyo alikuwa Musa. Wengine wao walifuata tu Ujumbe. Unaona?

Lakini leo hii, kwetu sisi TUNAOAMINI JAMBO HILO JINSI HIYO, mioyo yetu imejaa furaha na kububujika, ni vigumu sana kujizuia.

Ninajisikia kwamba Yeye ametukomboa. Ninajisikia ya kwamba majina yetu yamo kwenye Kitabu Chake. Ninaamini ya kwamba tumekombolewa kwa Damu ya Mwana-Kondoo .

Kwa sababu tunaamini kuwa Ujumbe huu ni Sauti ya Mungu inayozungumza nasi moja kwa moja, tunakubali hili kuwa ni Mungu Mwenyewe akizungumza nasi mdomo kwa sikio. HAKUNA SHAKA majina yetu yako kwenye Kitabu chake.

Naomba niliweke namna hii, huduma ya Yesu Kristo ikifanyika mwili katika Kanisa Lake katika siku hizi za mwisho. Hivyo ndivyo wengi wetu wanavyoamini. Ninaamini pamoja nanyi.

Hivyo ndivyo hasa sisi tunavyoamini jambo hilo , Yesu Kristo akifanyika mwili , akizungumza na Bibi-arusi Wake kwenye kanda.

Kila mara tunapobonyeza play imani yetu hufikia viwango vipya. Huyu sio tu mhubiri mwingine anayezungumza, huyu ni Mungu Mwenyewe anayezungumza nasi. Tunataka Neno safi peke yake 100% .

Hebu ni kuulize Jambo fulani . Je, William Marrion Branham ndiye mchungaji wako? Je, yeye ndiye Malaika-mjumbe wa saba aliyethibitishwa na Mungu? Je, unaamini alichomwomba Mungu afanye, Mungu alifanya ? Je! unaamini yeye alikuwa ni Sauti ya Mungu kwa wakati huu? Unaamini kila neno alilosema? Basi Jumapili utabarikiwa mara tena isivyoelezeka .

Hakuna njia nyingine unayoweza kupokea baraka hii isipokuwa unasikiliza kanda na kuamini kile unachosikia kuwa ni Bwana Asema Hivi. Huna budi kuamini Kile anachosema ni Mungu ananena nawe moja kwa moja.

Nami, kama mchungaji wenu, ndugu yenu, kwa imani niliyo nayo, nimemwomba Mungu aiweke hiyo juu yenu. Ninaamini kwamba nitapokea kile nilichoomba. Sasa ikiwa mtaamini pamoja nami; kwa imani ile niliyo nayo, ninawapa hiyo sasa hivi .

Kwetu sisi yeye ni mchungaji wetu. Hakuna mtu ulimwenguni aliye na Imani zaidi, au kuu kuliko MCHUNGAJI WETU, nabii wa Mungu. Sasa nabii wa Mungu amemwomba Mungu atupe IMANI YAKE KUU. IKIWA unaamini hilo kwa moyo wako wote, ni IMANI YAKO Hivi sasa….UTUKUFU, TUNAAMINI !!! Imani yetu inaweza kuwa dhaifu, lakini sivyo tena, kwa maana sasa tunayo IMANI yake.

Na sasa, katika Jina la Yesu Kristo, Mwana wa Mungu, kataeni mateso yenu, magonjwa yenu, na mseme “Huna budi kuondoka,” sababu mnayo imani yenu , na imani yangu, pamoja na nguvu za Yesu Kristo , Ambaye uwepo Wake wa kila mahali upo hapa kudhihirisha jambo hilo na kuthibitisha kwamba Yuko hapa, atawapa afya sasa.

Ninaweza kusema nini kitakachokufanya uje kuungana nasi na kupokea baraka hii kuu? Wazia jambo hilo, chochote unachohitaji, unaweza kukipata kama utakuja kusikiliza na kuliamini kwa urahisi.

Njoo usikilize pamoja na Bibi-arusi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville. ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania) Tutakusanyika na kusikiliza kutoka Mashariki, Magharibi, Kaskazini na Kusini, wote kwa wakati mmoja, wakati Bwana Asema hivi ikituzungumzia na kutuambia yote kuhusu: Yeye Aliye Ndani Yenu 63-1110E .

Ikiwa huwezi kusikiliza pamoja nasi kwa wakati mmoja Jumapili, haijalishi, bonyeza play tu wakati wowote na usikilize na uamini kile unachosikia kuwa ni Sauti ya Mungu inayozungumza nawe.

Ndugu. Joseph Branham