22-0619 Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

UJUMBE: 63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Baba Mpendwa, ninaweza kuandika nini leo ili upate kunitumia, kwa njia fulani ndogo, kumtia moyo Bibi-arusi Wako wa thamani?

Mungu amekuja katika wakati wetu na kuishi katika mwili wa mwanadamu, ndani ya mtu aitwaye William Marrion Branham, ili aweze kufunua na kutimiza Neno Lake. Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo katika wakati wetu.

Kuisikiliza Sauti hiyo na kuamini kila Neno ndiyo njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa siku ya leo. Alituma ulimwenguni watu wengi waliotiwa mafuta na Roho wake Mtakatifu, Lakini Yeye hutuma na kunena kupitia mtu mmoja tu kufunua Neno Lake na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Yeye kamwe habadilishi Mpango Wake au Njia Yake ya kufanya mambo. Jinsi alivyofanya jambo hilo mara ya kwanza, Yeye hulifanya hilo kila wakati. Yeye huwaongoza watu Wake Mwenyewe, kwa Nguzo ya Moto.

Wewe ni Bibi-arusi mteule wa Mungu na hakuna kitu shetani anachoweza kufanya au kusema ambacho kinaweza kulitoa jambo hilo kwako, HAKUNA! Alikuchagua tangu asili kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alikujua wakati huo, nawe ulikuwa pamoja Naye wakati huo. Alijua jina lako. Alijua kila kitu kukuhusu. Alijua mema na mabaya yako. Alijua kushindwa kwako, makosa yako, na bado alikupenda, kwa kuwa ulikuwa sehemu yake.

Nafsi yako inaweza tu kujilisha Neno Lake. Hakuna kinachoweza kukutosheleza ila Neno Lake. Unapenda kusoma Neno Lake na kumtafakari Yeye, kuomba kutoka ndani kabisa ya moyo wako, lakini unaposikia Sauti Yake ikizungumza nawe moja kwa moja, inakuinua juu ng’ambo ya pazia la wakati. Kwa maana unajua umeketi naye katika ulimwengu wa roho huku akinena nawe mdomo kwa sikio, akifunua Neno lake, akikukumbusha, WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU.

Shetani anaweza kukupiga tena na tena. Unaweza kushushwa moyo sana wakati mwingine na kuhisi wewe ni uliyeshindwa kabisa; Kujisikia kana kwamba umemkosea zaidi ya mtu yeyote yule. Wewe ni mbaya zaidi kuliko waovu wote , lakini mahali fulani, ndani kabisa katika nafsi yako, unasikia ile Sauti Ndogo tulivu ikikuambia: “Hakuna kitu kinachoweza kukutenganisha na Neno Langu, WEWE NI NENO LANGU. Nililiweka jina lako kwenye Kitabu changu cha Uzima cha Mwana-Kondoo, Mimi Mwenyewe.”

Niseme nini ili kukutia moyo leo hii? Bonyeza Play tu kila siku na usikie Sauti ya Mungu ikinena na kukuambia: Bwana Asema hivi.

Umealikwa kuungana na Bibi-arusi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA ., Saa za Jeffersonville,( Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania ) tunapokusanyika kusikiliza ile sauti ndogo tulivu: 63-1110m Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada :

Mwanzo 15:16
Mathayo Mtakatifu 23:27-34
Yohana Mtakatifu 4:23-24 / 6:49 / 14:12
1 Petro 3:18-22
2 Petro 2:4-5
Yuda 1:5-6