24-0107 Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

UJUMBE: 63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Watu Waliotengwa,

Mungu amekuja katika wakati wetu na kujifunua katika mwili wa mwanadamu, katika mtu aitwaye William Marrion Branham, ili aweze kulitimiza Neno Lake. Huo ndio Ufunuo wa Yesu Kristo katika wakati wetu.

Kuisikiliza Sauti hiyo na kuamini kila Neno ndiyo Njia pekee iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Alituma ulimwenguni watu wengi waliopakwa mafuta na Roho wake Mtakatifu, lakini Yeye alituma na kunena kupitia mtu mmoja tu kufunua Neno Lake na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Yeye kamwe habadilishi Mpango Wake wala Njia Yake ya kufanya mambo. Jinsi alivyolifanya mara ya kwanza, Yeye hulifanya jinsi hiyo kila wakati. Yeye huwaongoza watu Wake Mwenyewe, kwa Nguzo ya Moto.

Usisahau kamwe, WEWE NI Bibi-arusi mteule wa Mungu na hakuna kitu shetani anachoweza kufanya au kusema ambacho kinaweza kuliondoa hilo kutoka kwako, HAKUNA! Alikuchagua wewe tangu asili kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Alikujua tangu wakati huo, nawe ulikuwa pamoja Naye. Alijua jina lako. Alijua kila kitu kukuhusu. Alijua heri na shari zako. Alijua kushindwa kwako, makosa yako, na bado alikupenda na kukuchagua wewe kwa kuwa ulikuwa sehemu yake.

Nafsi yako inaweza tu kujilisha kwenye Neno Lake. Hakuna kinachoweza kukutosheleza ila Neno Lake. Unapenda kusoma Neno Lake na kumtafakari Yeye, ukiomba kutoka katika kilindi cha moyo wako. Unaposikia Sauti Yake ikizungumza nawe moja kwa moja, inakuinua hadi ng’ambo ya pazia la wakati. Kwa maana unajua umeketi naye katika ulimwengu wa roho wakati anaponena nawe mdomo kwa sikio, akifunua Neno lake, akikukumbusha, WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU.

Ibilisi aweza kukutwanga na kukutwanga. Waweza kushushwa moyo sana wakati mwingine na kuhisi wewe ni aliye shindwa kabisa; ujisikie kana kwamba umemkosa Yeye zaidi ya yeyote yule. Wewe ndiye mbaya zaidi kuliko wabaya wote, lakini mahali fulani, chini kabisa ndani ya nafsi yako, unasikia ile Sauti Ndogo Tulivu ikikuambia: “Hakuna kitu kinachoweza kukutenganisha na MIMI, WEWE NI NENO LANGU. Nililiweka jina lako kwenye Kitabu Changu Cha Uzima cha Mwana-Kondoo, Mimi Mwenyewe .”

Naweza kusema nini kuwatia moyo leo?

Kaeni tu katika Neno. BONYEZENI PLAY kila siku na mwisikie Sauti ya Mungu ikisema Bwana Asema hivi na kuwaambia; Ninawaunganisha katika Neno Langu. Mnaweza kushinda CHOCHOTE, kwa maana Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu. Nimewathibitishieni, mnayo IMANI KAMILIFU. Mmeiweka ile Ishara, nayo imewaweka katika Kudhikika. Nitasimama nyuma ya Neno Langu. Nitafanya kile nilichosema kuwa nitafanya.

Maneno Yake ni ya ajabu jinsi gani anayosema nasi kwenye Kanda. Tunajua si mtu fulani, mtu wa kimwili ambaye yuko miongoni mwetu. Ni Mungu wa Milele anayezungumza nasi, Bibi-arusi Wake.

Mnaalikwa kuungana na Bibi-arusi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapokusanyika kusikiliza ile Sauti Ndogo Tulivu:  63-1110M Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Mwanzo 15:16
Mathayo 23:27-34
Yohana 4:23-24 / 6:49 / 14:12
1 Petro 3:18-22
2 Petro 2:4-5
Yuda 1:5-6