24-0121 Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo?

UJUMBE: 63-1124M Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo?

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wapenda Kanda,

Tunaupenda Ujumbe huu kwa moyo wetu wote. Ni utamu wa miwa ya Mungu. Ni Neno la Mungu ambalo limethibitishwa kinaganaga, na kuhakikishwa, tena na tena. Ujumbe huu ni jibu la Neno la Mungu. Ni Kristo yeye yule aliyetiwa mafuta, lile Neno lililotiwa mafuta la siku yetu.

Tuna Neno la Mungu lililothibitishwa hapa, likithibitisha, kuhakikishwa na Roho, ya kwamba Yeye ametupokea na kutupa Ubatizo wa Roho Mtakatifu. Tumebatizwa katika Jina la Yesu Kristo. Injili ile ile, ishara zile zile, maajabu yale yale, huduma ile ile, hata Nguzo ya Moto ile ile ikionekana mbele zetu, ikionyesha ishara na maajabu. Hakuna udhuru, mahali po pote.

Ni wakati wa kuungana kwa Mungu na Bibi-arusi Wake. Bibi-arusi wa Kristo amekwishaitwa. Tumetiwa muhuri katika Ufalme wa Mungu. Mitambo iko hapa tunangojea tu Nguvu za Utendaji zitakazotuondoa kwenye dunia hii kuingia Utukufuni, katika Kunyakuliwa.

Hizo Nguvu za utendaji ni kujazwa tena kwa Roho Mtakatifu. Jiwe la Kufunika litashuka na kuungana na ule Mwili. Ndipo, wakati Kichwa hicho na Mwili huo vinapoungana pamoja, zile nguvu kamili za Roho Mtakatifu zitatuinua SISI juu na waliokufa katika Kristo watafufuka katika uzuri wa utakatifu Wake, na kuruka kwenda hewani.

Saa hiyo inawadia haraka sana. Wakati umefika mwisho. Maamuzi ya mwisho hayana budi kufanywa. Utafanya nini na Neno lililotiwa mafuta la siku hii? Msimamo wako ni upi juu ya Ujumbe wa saa hii?

Je, hivi utasema tu: “Ninaamini Ujumbe. Ninaamini Mungu alimtuma nabii.”

Usifikie tu umbali huu, ukasema, “Naamini Ujumbe.” Tii mjumbe.

Iwapo huna budi KUMTII mjumbe: ANGALIA, alisema tii mjumbe. Basi ni muhimu jinsi gani kuamini na kusikia kila Neno ambalo mjumbe huyo alilosema?

Unasema, “ Vema, Naamini kila neno lililosemwa, Ndugu Branham.” Hilo ni sawa, bali hiyo ni—hiyo ni uwezo tu wa kusoma.

Kwa nini watu wasiridhike na kanda? Kila mtu hawezi kuwa nabii. Kuna nabii mmoja tu, na Neno huja kwa nabii huyo.

Kanisa lilifanya vizuri mpaka walipoanza kulihoji hilo; ama walitaka sauti zingine kuwaambia, na kuwafasiria, yale ambayo nabii huyo aliyosema. Walitaka Kora na Dathani wa sasa.

Mnaona, ilianza na upotoshaji mdogo tu wa Neno, na, jambo lile lile, inaishia vile vile.

Kama ilianza hivyo, na itaishia hivyo, upotoshaji mdogo tu wa Neno, hakika mnatambua jinsi gani MNAVYOPASWA kukaa na kanda. Hakika mnaona kwa nini Mungu alihakikisha kuwa Ujumbe huu umerekodiwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya Bibi-arusi.

Sisemi mambo haya kuwashusha wachungaji wenu, au kusema msimsikilize mchungaji wenu, HAPANA, bali kuwaonyesha umuhimu wa kubonyeza play na kuusikia Ujumbe huu kwenye kanda.

Jinsi Kanisa linapaswa kuwa linahakikisha tena, na tena, na tena, na tena! Tunakungojea Kuja Kwake. Tunaamka, tunakungojea kule kuondoka. Inatubidi kulichunguza kwa Neno, si kile mtu fulani alichosema. Hakikisha unajua, wewe mwenyewe, kama tukio la kibinafsi pamoja na Kristo. Lichunguze tena, na tena, na tena.

AMESEMAJE? Inatubidi kulichunguza kwa Neno tena, na tena, na tena. Unalichunguzaje kwa Neno? Neno la siku hii ni lipi? Ni lile lile kama lilivyokuwa tangu mwanzo, Biblia.

Mungu anasema ni nani aliye mfasiri wa Neno Lake? ni Mimi? Ni Mchungaji wako? HAPANA, nabii wa Mungu aliyethibitishwa wa wakati huu ndiye mfasiri pekee wa Neno. Kwa hiyo, ni lazima ulichunguze kwa KANDA kila Neno analosema mtu yeyote tena, na tena, na tena!

Ikiwa tamshi hilo ni la kweli, na unaamini kwamba jambo lililo muhimu zaidi ambalo mtu yeyote, au mchungaji yeyote analoweza kufanya, ni KUBONYEZA PLAY, Basi kwa nini hilo ni gumu sana kwa yeyote anayedai kuamini Ujumbe kusema hivyo? Kwa sababu tu hawaliamini.

Uamuzi WAKO wa mwisho ni upi? Kwangu mimi na nyumba yangu, tutabaki na Ujumbe huu na mjumbe wa Mungu, Kanda hizi. Tunaamini hakuna kitu muhimu zaidi kuliko kusikiliza Sauti ya Mungu kwenye kanda.

  • Kuna Sauti MOJA tu ya Bwana Asema Hivi.
  • Kuna Sauti MOJA tu ambayo Nguzo ya Moto iliithibitisha.
  • Kuna malaika-mjumbe wa saba MMOJA tu.
  • Kuna Sauti MOJA tu ambayo Bibi-arusi wote wanayoweza kukubaliana kwake.
  • Kuna Sauti ya Mungu MOJA tu kwa ajili ya kizazi hiki.

Kama unao Ufunuo huo huo, njoo uungane nami na kundi dogo la waaminio ulimwenguni kote wanaoamini jinsi hiyo hiyo, Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunaposikia na kufanya uamuzi wetu wa mwisho: Nimtendeje Yesu Aitwaye Kristo? 63-1124M.

Ndugu. Joseph Branham