UJUMBE: 65-0418E Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?
- 26-0412 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?
- 24-0707 Je! Mungu Habadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?
- 22-1218 Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?
Wapendwa Waliohuishwa,
Jinsi gani mioyo yetu ilivyoinuka kama Tai wikendi hii ya Pasaka. Siku baada ya siku, upako Wake ulizidi kuwa mkubwa. Ushirika, Kuzikwa, Ukamilifu, kisha kile kilele kikuu Alichotujengea: Ni Kuchomoza kwa Jua…UTUKUFU, AMEFUFUKA na Yuko hai ndani ya kila mmoja wetu. Yeye alikuwa akilifunua Neno Lake kwa kila mmoja wetu jinsi tusivyowahi kusikia hapo awali. Ule upako uliifurika mioyo yetu, uwepo Wake uliitanda hewa; ilionekana kana kwamba Unyakuo ulikuwa umekaribia.
Yeye alituambia yale yaliyotukia miaka 2000 iliyopita, na kisha yale yaliyokuwa yakitukia sasa mwaka wa 2026. Yesu alikuwa Chembe ya kwanza ya Ngano ya Mungu iliyofufuka kutoka kwa wafu. Yeye alikuwa amefufuliwa na Nguvu za Mungu za kuhuisha. Mungu alikuwa ameyahuisha maisha Yake, akamfufua kutoka kwa wafu, Naye alikuwa malimbuko ya kwanza ya wale waliolala. Yeye alikuwa wa kwanza kukomaa, Mganda wa Mungu uliotikiswa kama ukumbusho wa kutoa shukrani kwa Mungu, akiamini kwamba sisi wengine tungekuja. Ilikuwa ishara.
KISHA YEYE AKATUFUNULIA KILE KILICHOTUKIA LEO. Kama vile Yeye alivyotikiswa siku ya Pentekoste wakati sauti kutoka Mbinguni iliposikika kama upepo wa nguvu ukienda kasi ukitikiswa juu ya watu. Ulikuwa ukitikiswa tena mbele ya watu kama alivyoahidi katika Luka 17:30 na Malaki 4, wakati Mwana wa Adamu atakapofunuliwa na kutikiswa tena juu ya watu.
Sasa, Mwana wa Adamu ni Nani? “Hapo mwanzo alikuwako Neno, naye Neno alikuwa kwa Mungu, naye Neno alikuwa Mungu. Naye Neno akafanyika mwili, akakaa kwetu.” Na iwapo mafundisho yote tuliyo nayo, na thibitisho la Neno la Mungu; kwa Neno la Mungu, kwa ishara, kwa maajabu, tunaona leo, ya kwamba katika Kitabu cha—cha Luka hapa, ya kwamba kama tulivyonukuu hicho hivi punde, ama Lu—Luka mlango wa 17 na kifungu cha 30; na Malaki 4, na Maandiko mbalimbali ambayo tunayajua, ya kwamba hilo Neno tena linatikiswa juu ya watu, ya kwamba mapokeo yaliyokufa ya mwanadamu yamekufa, na Mwana wa Mungu yu hai tena na ubatizo wa Roho Mtakatifu moja kwa moja miongoni mwetu, naye anatupa Uzima.
Roho Mtakatifu aliendelea kutikisa na kutikisa juu yetu, akifunua na kufunua Neno Lake… Nguvu za utendaji, mitambo, Nguvu za kuhuisha…
Ndipo, ilipoonekana kana kwamba Haiwezi kuwa kuu zaidi, Yeye alituambia:
Naye akaniruhusu niangalie ng’ambo ya pazia, nami nikawaona ninyi nyote kule ng’ambo… Wote uliowahi kupenda, na wote waliowahi kukupenda, umepewa wewe.” Mnaona? Niliwaona hao kila mahali pale namna hiyo. Ilikuwa nini? Nguvu za kuhuisha.
YEYE ALITUONA SISI KULE!! Ng’ambo ya pazia la wakati….tulikuwa KULE pamoja naye; wapendwa wetu wote waliotutangulia…akina baba, mama, watoto. Tulikuwa kule pamoja nao na wale wote ambao hatujawahi kukutana nao: Musa, Eliya, Petro, Paulo….tulikuwa sote kule pamoja.
Kisha, kama vile Roho Mtakatifu alivyo mzuri, Yeye hakutaka kutusahau sisi tulio wagonjwa, wenye huzuni na waliopigwa, kwa hivyo Yeye alijitikisa Mwenyewe juu yetu tena ili kila mtu aponywe chochote kile tulichokuwa na haja nacho.
Watu hawa, ambao ni raia wenza wa Ufalme, mmiliki wa Nguvu za kuhuisha, lihuishe kwao, Bwana, sasa hivi. Pia naomba Roho aende kutoka tai hadi tai, kutoka kwenye Neno hadi Neno, mpaka utimilifu wa Yesu Kristo udhihirishwe katika kila mmoja wa hiyo miili, kwa ajili ya haja za kimwili, za kiroho, ama haja zozote walizo nazo, tunapowekeana mikono sisi kwa sisi. Katika Jina la Yesu Kristo.
Neno Hilo. Sauti Hiyo. KILA KITU tunachokihitaji kiko kwenye kanda, Ewe, Bibi-arusi. Mungu habadilishi nia Yake kuhusu Neno Lake. Hakuna nukta moja au yodi moja inayoweza kubadilishwa, kwa hivyo Yeye alitengeneza njia ambayo Bibi-arusi Wake angeweza kusikia kwa masikio yao wenyewe kile hasa Yeye alichotaka kuwaambia.
Mungu amenena na Bibi-arusi Wake na kufunua KILA KITU. Kimerekodiwa. Bibi-arusi lazima aje kwa Bwana Arusi; hiyo ndio Njia Yake kamilifu iliyoandaliwa ambayo imetengenezwa kwa ajili ya siku hii. Ni BWANA ASEMA HIVI.
Je! Mungu hubadilisha Nia Yake kuhusu Neno Lake? HAPANA. Yeye anayo MAPENZI MAKAMILIFU NA MAPENZI YAKURUHUSIA. Bibi-arusi yambidi awe katika MAPENZI YAKE MAKAMILIFU. Hakuna Mapenzi yaliyo makamilifu zaidi, au mahali pakamilifu, kuliko kuisikia Sauti ya Mungu moja kwa moja kutoka kwa Mungu Mwenyewe.
Mwaliko wangu kwa kila mmoja wenu ni muungane nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki), kuisikia Sauti ya Mungu ikituletea Neno Safi. Hakuna haja ya kubahatisha, wewe keti tu na useme AMINA KWA KILA NENO….hakuna mahali pengine hilo linaweza kufanywa, ila kwa KUBONYEZA PLAY.
Ndugu Joseph Branham.
Ujumbe: 65-0418E — Je! Mungu Hubadilisha Nia Yake Kuhusu Neno Lake?
Tutaanzia kwenye aya ya 61.
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:
Kutoka sura ya 19
Hesabu 22:31
Mathayo Mt. 28:19
Luka 17:30
Ufunuo sura ya 17