22-0508 Kristo Ni Siri ya Mungu iliyofunuliwa

UJUMBE: 63-0728 Kristo Ni Siri Ya Mungu Iliyofunuliwa

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Wapenzi wa Moyo Wake,

Ninayo heshima kubwa zaidi duniani. Bwana ameniruhusu nimtambulishe yeye mwenyewe kwenu, ili aweze kusema nanyi moja kwa moja kupitia chombo alichochagua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu ili kunena na kuwafunulia Neno lake lote.

Si mtu wa Mungu tu, Ni Mungu Mwenyewe, Nguzo ya Moto, Roho Mtakatifu akizungumza nawe moja kwa moja, mdomo kwa sikio, nasi tunayo heshima na majaliwa kumwita nabii Wake mteule, MCHUNGAJI WETU.

Kamwe hatujiulizi kama kile tunachosikiliza ni mwanadamu, fikira zake, wazo lake, au fasiri yake ya Neno. Ni Mungu Mwenyewe Akinena nasi BWANA ASEMA HIVI.

Ninajua watu wanakariri tu jambo hilo, lakini sisi tunakunywa ndani . Kwa maana ndicho kitu pekee ambacho hukata kiu yetu na kutosheleza nafsi zetu. Ni Maneno ya Uzima wa Milele. Kwetu sisi, Ni Sauti ya Mungu. Ni Ujumbe wa wakati huu. Kwa hiyo, ni Neno, Sauti, Kanda, SIO KINGINECHO!

Tumeungana pamoja chini ya Kiongozi mmoja kama Israeli wa kale. Mungu Mmoja, aliyethibitishwa kwa Nguzo ya Moto, na kujifunua Mwenyewe kupitia nabii Wake kuwa Neno. Mungu yeye yule, Nguzo ile ile ya Moto, vivyo hivyo leo. Mungu hawezi kamwe kubadilisha asili yake. Mpango Wake hauwezi kamwe kubadilika kutoka kwa kile Alichoanza nacho, kwa sababu Yeye hana kikomo na mpango Wake na mawazo Yake yote ni kamilifu.

Ndiyo maana tuna matazamio makubwa kusikia kile ambacho anaenda kutufunulia siku ya Jumapili. Alisema ya kwamba Yeye amepiga pande zote za ncha zake, ndani na nje yake, na hata alionyesha kwa Maandiko na mpangilio wake wa matukio, mpaka tunajua ya kwamba Ujumbe huu ni Kweli kabisa. Hakuna makosa .

Lakini Jumapili, Roho Mtakatifu ataushika Ujumbe na kuuweka mahali ulipo sasa. Yeye ataujenga tangu pale ulipoanzia, na kuujenga moja kwa moja hadi wakati huu wa sasa.
Hebu tunywe machache tu ya yale Mungu atakayotuambia na kutufunulia kupitia mchungaji wetu siku ya Jumapili:

Ninyi ni mboni ya moyo wangu, wale ambao mmezaliwa kwa Bwana kwa Roho na kwa Neno la Kweli. Ninaomba tu na kumwomba Bwana awabariki na kuwaweka nyinyi kuunganishwa pamoja kwa vifungo vya upendo wa Kristo.

Bwana aliniweka Ni hifadhi Chakula ghalani kwa ajili yenu; mboga zenye afya nzuri, hapa katika maskani hii. Na leo hii, utapokea mzigo mzima wa Kanda . Itakufunulia Yesu Kristo katika saa tunayoishi. Ujumbe huu utawahifadhi na kuwatia nguvu. Utawapa nguvu za kiroho kwa kazi iliyo mbele yenu.

Hebu niwaambieni tena ninajua mnapenda kulisikia jambo hili: Ninyi ndiyo nambari iliyoteuliwa na iliyochaguliwa tangu zamani, ndio watu pekee watakaolisikiliza. Ninyi ndiye Bibi-arusi mteule ambaye hataanguka bali atashikilia Neno hilo bila kujali wengine wote ulimwenguni kote wanasema nini kuhusu hilo. Wewe ni Bibi-arusi Neno!

Mungu amekufunulia siri hii kuu, na huko ndiko Kuzaliwa upya. Sasa anakuleta pamoja ambapo ufunuo ulipo katika upatano mkamilifu. Mungu akilidhihirisha kupitia Neno Lake kwa matendo yale yale, mambo yale yale aliyofanya, akilidhihirisha Neno ndani yako.

Usisahau kamwe, Roho Mtakatifu, peke yake, ndiye Mfunuzi wa ufunuo wa Kiungu wa Kristo, na amekuwako katika nyakati zote. Kumbuka, Nyakati zote ! Neno la Bwana lilikuja kwa nani? Nabii, peke yake.

Ninatambua kuwa ninazungumza na maelfu kwenye kanda, tuna huduma ya kanda kote ulimwenguni. Na inaonekana kuwa tunaweza kutengeneza kanda kutoka hapa ambayo ni bora mara kumi kuliko mahali popote pengine . Ninatumai tu kila mwanamume anayesikia kanda hii, na kila mwanamke, ataelewa.

Sasa ni juu yao ikiwa wanataka kusikiliza kanda yoyote , lakini sitaki mlikose hili. Enyi watu wa kanda; huko msituni na popote mnapoisikia, sasa sikilizeni.

Tunazo kanda  kuhusu kile tunachoamini. Tunazo kanda zinazohusu nidhamu kanisani, jinsi tunavyoenenda sisi wenyewe katika kanisa la Mungu, jinsi tunavyopaswa kuja hapa pamoja na kuketi pamoja katika ulimwengu wa roho.

Natumai kila mtu kwenye kanda analipata jambo hilo. Ukishindwa, rudi kwenye kanda  hii tena . Sijui nitakuwa nanyi kwa muda gani zaidi. Kumbukeni, Hii ​​ndiyo Kweli, ya BWANA ASEMA HIVI. Ni kweli. Ni Maandiko .

Uongozi na Mwili umekuwa kitu kimoja. Ni Mungu akidhihirishwa ndani yenu , watu Wake. Hiyo ndiyo sababu mume na mke si wawili tena; wao ni mmoja. Mungu na Kanisa Lake ni mmoja, “Kristo ndani yenu,” ufunuo mkuu wa Mungu.

Sio wazo langu; ni Nguvu Zake, ni Neno Lake. Aliliahidi ; ndilo hili hapa. Alisema lingekuwa hapa, ndilo hili hapa. Ninyi ni wana wa Mungu. Si kwamba mtakuwa ; MKO SASA HIVI!

Jaza kikombe chetu Bwana, tunakiinua juu, Bwana, njoo ukate kiu ya roho zetu. Mkate wa Mbinguni, utulishe, hadi tusihitaji zaidi. Jaza kikombe chetu, kijaze mpaka pomoni na utufanye tuwe wazima.

Ni wakati wa jinsi gani wa uamsho tutakaokuwa nao ulimwenguni kote tutakapokusanyika Jumapili ili kusikia: Kristo Ni Siri ya Mungu iliyofunuliwa 63-0728 saa 06:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville.( ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania ).

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya Kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe :

Mathayo Mtakatifu 16:15-17

Luka Mtakatifu Sura ya 24 yote

Yohana Mtakatifu 5:24 / 14:12

1 Wakorintho Sura ya 2 yote

Waefeso Sura ya 1 yote

Wakolosai Sura ya 1 yote

Ufunuo 7:9-10