22-0501 Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila Ya Kumwonya Kwanza

UJUMBE: 63-0724 Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila Ya Kumwonya Kwanza

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa kamani ndogo , springi kuu, ama chochote ulicho :

Sote ni Mwili wa Kristo, katika mahali petu, katika upatano, tukijaribu kufanya kazi vizuri sana tuwezavyo kwa ajili Yake. Hakuna kitu kingine muhimu kwetu, ila Neno Lake, Ujumbe huu.

Tunapenda tu kusikia nabii wa Mungu akituambia : “Kuna jambo fulani juu yenu watu fulani. Ninyi ni watu maalum katika maisha yangu. Kuna kitu kingine ambacho napenda tu kukutana nanyi na kuzungumza tu nanyi ”.

“Naangalia huku kwenye huduma yangu ndogo nyenyekevu; Yesu Kristo yeye yule jana, leo, na hata milele, nami naona kile inachofanya; inaita na kuunganisha kundi la Bibi-arusi pamoja. Nikutoa Gurudumu kutoka kwenye gurudumu.”

Tunajua si mwanadamu, ni Neno la Mungu linalomkusanya Bibi-arusi Wake pamoja. Mambo ambayo tunaona yakitekelezwa si kitu mbali na Mungu. Hakuna tena huenda ikawa ndivyo, ingewezekana , inaonekana kana kwamba huenda ikawa, NI MUNGU!!

Tumefika mahali hapo kwamba Ndio Lulu ya thamani kubwa kwetu. Tumeachana na chochote mtu yeyote anachotuambia kinyume Chake. Hatuangalii kile mwanadamu ametimiza. Tunaangalia kile Mungu amesema na kile Yeye ameahidi angefanya katika Siku yetu, nasi tunamwona Yeye akikifanya.

Huo ndio Mkataa wetu. Kila kitu tulicho sisi, kila kitu tulichokuwa, kila kitu tunachotumaini kuwa, kimewekwa juu ya Ujumbe huu. Ni zaidi ya uhai kwetu.

Ni kama Haijawahi hapo kabla katika historia ya ulimwengu, tunamwona Mungu akitoa onyo, Jiandaeni kwa ajili ya hukumu. Bomu za atomiki ziko kwenye mabanda yake, kila kitu kiko tayari.

Wakati huu, si kwa kikundi kidogo tu cha watu, kama ilivyokuwa katika siku za Nuhu, au katika siku za Ibrahimu; ni Mungu akiwaonya watu wa ulimwengu mzima, akinena kupitia nabii Wake, hili ndilo onyo lenu la mwisho.

Yeye Anatuambia, “Kabla sijaruhusu jambo hili litukie, ninatoa wito wa mwisho, kama tu nilivyofanya Sodoma, Tokeni kwake. Iweni tayari. Jambo fulani litatukia ”.

Ulimwengu unategemea ufanisi wao mkuu wa sayansi; uzalishaji wa kisayansi umeleta mauti kwa vizazi. Walio werevu na wenye elimu wanaingia upande wa kiakili : UMOJA WA MATAIFA , NATO, Shirikisho la Mataifa. Kila siku tunaona hukumu ikikaribia zaidi na zaidi. Kile nabii alichoona tokea mbali na kutuambia kingekuja kutokea, kinatendeka: Urusi, Vita, Mafuta, Vatikani, Wayahudi, Mabomu ya Nyuklia.

Hakuna tena kujiuliza nini kitatokea. Tunaliona likitendeka kila siku, na hofu duniani ni Hakika na inazidi kuwa kubwa zaidi na zaidi kila siku.

Lakini ni kama tu alivyofanya katika siku za Hezekia, wakati Mungu aliponena kupitia nabii wake na kuwaonya watu, “ Tengenezeni Mambo , kwa kuwa hukumu iko tayari kuanguka”. Nabii wake alikuwa akiwatayarisha watu kwa ajili ya wakati ule uliokuwa unakuja.

Nuhu aliwatayarisha watu kwa wakati wake. Ulikuwa ni wito wa rehema kabla ya hukumu. Mungu alikuwa na njia iliyoandaliwa, nabii wa kuwaongoza.

Aliwatumia Neno Lake. Naye daima hulituma Neno Lake kwa nabii Wake, kama alivyofanya katika wakati wa Nuhu. Alifanya jambo lile lile katika siku za Nuhu. Katika siku za Eli-…za Musa, tunaona Yeye alifanya jambo lile lile. Aliwatumia nabii Wake, nao wakajitenga na kutokuamini. Sasa, watu wa jinsi hiyo ndio waliotoka. Hao ndio walioliamini.

Tumejitenga na kutokuamini kote. Mungu anayo njia iliyoandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake leo. Alituahidi katika Neno Lake, “Kabla ya hukumu, nitawapelekea nabii kulikusanya Kundi langu dogo nyenyekevu, nami nitawaketisha upande mmoja, nao watakuwa na amani, wakiingojea hukumu ijayo na kuiepuka. ”.

Sisi ndio kundi lile dogo. Sisi ndio wale ambao Baba anaowapenda nasi tunangojea kwa hamu kubwa Ujio wake wa hivi karibuni . Ulimwengu unaporomoka pande zote kutuzunguka, lakini sisi tuko katika pumziko na amani.

Tunajua tuko katika mapenzi yake makamilifu. Haijalishi tuko wapi ulimwenguni, Mungu ana njia iliyoandaliwa kwamba sisi sote tunaweza kuungana pamoja kwenye Neno Lake, kwenye Sauti Yake. Ni njia iliyoandaliwa na Mungu.

Naye huyu nabii akawaongoza kwenye njia iliyoandaliwa na Mungu. Sasa, hiyo ndiyo njia ya Mungu ya kufanya mambo. Unaona?

Njoo uepuke hukumu ijayo pamoja nasi na usikilize:  63-0724 Mungu Hamwiti Mtu Hukumuni Bila ya Kumwonya Kwanza , Jumapili hii saa 6:00 Sita MCHANA , saa za Jeffersonville (Ni Saa 1:00 Moja JIONI ya Tanzania). Ni Sauti ya Mungu ikinena na kutuambia: Hii ndiyo njia Yangu iliyoandaliwa kwa ajili ya Siku hii.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kwa maandalizi ya kusikiliza Ujumbe :

Isaya 38:1-5

Amosi Sura ya 1 yote.