22-0515 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

UJUMBE: 63-0818 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mwili wa Mwili Wake, Neno la Neno Lake, Uhai wa Uhai Wake, Roho wa Roho Wake,

Mpendwa Bibi-arusi Mtangulizi ,

Tulipoketi pamoja katika ulimwengu wa roho kutoka duniani kote Jumapili iliyopita , tulikuwa tukisikiliza Sauti pekee ya Mungu iliyothibitishwa ikizungumza nasi. Kama kawaida, tulikuwa chini ya matarajio makubwa kusikia kile alichokuwa anaenda kutuambia. Roho Mtakatifu anaenda kutufunulia nini leo?

Huenda tumesikia maneno yake mara nyingi hapo kabla, lakini tulijua siku hiyo ingekuwa tofauti. Tungesikia jambo fulani ambalo hatukuwahi kusikia hapo kabla. Tungepokea Ufunuo zaidi hata ya tunavyoweza kufikiria. Angefungua mioyo yetu, akili zetu na nafsi zetu, na kufunua jambo ambalo lilikuwa SASA HIVI, katika Majira yake Halisi, kufunuliwa.

Kisha linatokea. Maneno makuu sana bwana arusi awezayo kusema na kufunua kwa Bibi-arusi wake, “Wewe ni utimilifu kamili wa Uungu kwa jinsi ya mwili, mtangulizi. Yote niliyokuwa, niliyamimina katika Kristo; yote Kristo aliyokuwa, niliyamimina ndani YAKO . WEWE NI Bibi-arusi-Neno wangu Mkamilifu niliyemchagua . “

Utu wetu wote uliruka kwa furaha. Baba ndo kwanza atuambie, sisi ni Bibi-arusi wake. Sisi ndio wale awapendao. Sisi tumetiwa mimba na Neno lake, na Neno lake PEKE YAKE . Tumbo letu limefungwa kwa kitu kingine chochote. Yeye amekuwa akitungojea sisi, na kutamani kutupata Sisi … SISI !!

Na wajua nini ? Yeye kamwe hakumtuma mtu mwingine kutuambia Maneno haya, Yeye amekuja na kuishi katika mwili wa kibinadamu kwa mara nyingine tena, ili apate kuzungumza moja kwa moja, mdomo kwa sikio, na KUTUAMBIA : “Nakupenda, Bibi-arusi wangu kipenzi .”

Tunapenda kuimba, tunapenda ushirika, tunapenda kukusanyika pamoja na waaminio, Lakini tunachopenda zaidi ya yote ni kusikia Sauti ya Mungu; Hivi asema Bwana, ikinena Nasi moja kwa moja . Kila ujumbe ni Kitu kikuu cha binafsi KWETU . Yeye aliweka kila neno Alilotaka kutuambia kwenye kanda ya sumaku hivi kwamba tuyasikie sisi wenyewe.

Ni kitu gani Yeye atatuambia na kutufunulia Jumapili hii tutakapokusanyika? ni majira gani?

Isaya alinena na kusema, “Bikira atachukua mimba na kuzaa mtoto”, lakini ilikuwa ni miaka 700 kabla ya majira yake ya kutimia. Mfalme Daudi alisema, “Walizua mikono yangu na miguu yangu.” Alizungumza kana kwamba ilikuwa mikono yake na miguu yake, lakini Hayakuwa majira yake yakutimia bado miaka 1,000.

Mungu alinena kupitia nabii wetu katika wakati wetu na kusema mambo mengi yasingewezekana kutimia mpaka leo hii. Tunaona mataifa na ulimwengu wakiungana zaidi ya wakati mwingine wowote. Tulidhani Ukomunisti ulikuwa kitu cha zamani na ulikuwa umesambaratishwa, lakini sasa tunaona ni hai sana na ni chombo mikononi mwa Mungu, kama vile alivyotabiri na kutuambia ulikuwa hivyo.

Ulimwengu ulidhani vita baridi vilikwisha, na hakuna tena tishio la vita ya nyuklia. Lakini leo, tishio la vita ya nyuklia limekuwa ni Halisi. Kila kitu kimewekwa mahali pake kama tu vile alivyotuambia kwamba itakuwa. Haya ndio majira yenyewe .

Jumapili Hii, Yeye kwa mara nyingine tena ATANENA NASI MOJA KWA MOJA , mdomo kwa sikio, nasi tutasikia Jambo kuu lingine ambalo lilinenwa na kuhifadhiwa kwa ajili yetu tu tusikie. Ni kitu gani yeye Atasema na kutufunulia? ni majira gani? Ni Kitu gani kinachotendeka ?

Mungu anamuunganisha Bibi-arusi Wake. Anakusanyika pamoja, kutoka Mashariki na Magharibi, na Kaskazini na Kusini. Kuna wakati wa kuungana, na huo unaendelea sasa hivi. Anaungana kwa sababu gani? Unyakuo.

Basi Ujumbe huu unatenda nini wakati tunaposikiliza Sauti ya Mungu kutoka kote ulimwenguni ? Kumuunganisha Bibi-arusi na Neno. Neno ni Mungu. Bwana arusi ni Neno. Bibi-arusi ni msikiaji wa hilo Neno, nasi Tunakuja pamoja katika muungano. Tunajiandaa kufanya arusi ambapo tunakuwa mmoja na Neno.

Yote aliyo Baba, ndivyo nilivyo Mimi; na yote niliyo Mimi, ndivyo mlivyo ninyi; na yote mliyo ninyi, ndivyo nilivyo Mimi. Katika siku hiyo mtajua ya kwamba Mimi niko ndani ya Baba Yangu, Baba ndani Yangu, Mimi ndani yenu, nanyi ndani Yangu.” Unaona? Katika “siku hiyo.” Siku gani ? Leo hii ! Tunaona zile siri kuu zilizofichwa za Mungu zikifunuliwa. Loo, jinsi ninavyopenda jambo hilo!

Huu ndio wakati wenyewe Hasa . Haya ndio majira yake hivi sasa . Bibi-arusi yuko tayari kwa ajili ya Bwana arusi. Tunasikiliza Tunaposikia kile kilio cha Usiku wa manane “Tazama, Bwana Arusi yuaja!” Tuko kabisa kwenye wakati wa mwisho.

Njoo uungane nasi Tunapoungana kwenye Neno, Jumapili Saa 6:00 SITA MCHANA ya Jeffersonville , ( Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Tanzania) Tunaposikia sauti ya Mungu ikituambia ni : Wakati Wa Kuungana na Ishara Yake 63-0818 .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla ya ibada :

Zaburi 86: 1-11

Mathayo Mtakatifu 16: 1-3