23-1210 Imani Kamilifu

UJUMBE: 63-0825E Imani Kamilifu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Imani Kamilifu,

IMANI yetu huja kwa kusikia, kulisikia Neno. Neno humjia nabii.

Nabii ni:

Neno lililofanyika mwili! Haleluya! Neno likitenda kazi katika mwili wa mwanadamu, kwa ishara za kimwili kwa ishara za vitu, kwa ishara za Kimaandiko, kikamilifu, kuwaleteeni Imani Kamilifu kwa ajili ya Kunyakuliwa Kukamilifu.

Sisi tunafanya kile hasa Neno linasema tufanye kwa kuisikia Sauti ya Mungu pekee iliyothibitishwa ikinena na kufunua Neno Lake kupitia mwili wa mwanadamu ili kutupa Imani Kamilifu.

Inakupasa…masikio yako ni bubu kwa kinginecho chote isipokuwa neno analosema Roho. Unaona? “Kwake yeye aliye na sikio ( linalosikiza ), aone neno ambalo Roho ayaambia makanisa”; yeye aliye na mahali pa kusikizia, ambapo panapokea neno ambalo Roho ayaambia makanisa. Waona?

Sisi ndio mahali pake pa kusikizia ambapo panalipata na kuliamini kila Neno. Anapotupa amri: “Semeni tu yale yaliyo kwenye hizo kanda. MIMI NI Sauti ya Mungu kwenu. Mnaniita mimi mchungaji wenu, nanyi mwanena vema, maana ndivyo Nilivyo.” Sisi tunayatekeleza. Cho chote Asemacho, hamna tashwishi kamwe tunatembea moja kwa moja. Lolote Bwana anenalo kupitia nabii Wake, hamna mtu ulimwenguni anayeweza kutushawishi vinginevyo, tunaendelea vivyo hivyo.

Sasa unafikia Imani Kamilifu , ukamilifu mtimilifu usioweza kushindwa. Imani hiyo haishindwi.

Sasa tunayo Imani Kamilifu katika Neno Lake. Sisi hatujitazami wenyewe. Hatuogopi lolote, kama Ayubu. Hatuogopi kuyatazama mawimbi makubwa na kuzama ndani ya maji kama Petro. Siku hizo zimepita. SASA tunalitazama lile Neno Kamilifu linaloishi na kukaa ndani yetu. Tunafikia asili ya Bibi-arusi. Tunafikia katika hali ya kunyakuliwa.

Tunapoomba, tunaamini kwamba tunapokea kile tunachoomba, nasi tutakipokea; tutapewa. Wakati, mahali, hakuna kitu kitakachokibadilisha. Tunajua imetendeka. imekwisha Tayari. Tunajuaje? Kwa sababu si Neno letu, bali ni NENO LAKE, ambalo amesema na kutupa sisi. Tuna NGUVU NA IMANI KAMILIFU YA KULINENA.

Kama vile Yesu alivyofanya kwa ajili yake Mwenyewe, tunatambua mahali petu; sisi ni nani. Jambo pekee tunalopaswa kufanya basi, ni kuwa na imani na kile tulicho. Tuwe na imani katika kile NENO linasema tulicho! Ndipo Neno la Mungu linakuja ndani yetu na kujidhihirisha Lenyewe; kwa maana sisi ni waamini. Na mwamini ni “imani ya Mungu inayotenda ndani yetu.”

Na sasa, tunakuwa watiwa mafuta kwa Roho yuyo huyo, masihi watiwa mafuta, masihi wa siku za mwisho, kuangaza ufufuo wa Yesu Kristo; kuonyesha ya kwamba si mfu, bali yuko katika umbo la Roho Mtakatifu, yu ndani ya watu Wake, akitembea kati ya Bibi-arusi Wake, akimfanyia mapenzi, akijimwaga Mwenyewe Kwake. Wanakuwa mmoja kwa ajili ya Karamu ya Arusi; na ishara zile zile, zilizoahidiwa na Mungu yule yule, katika Neno lile lile zinafanya madhihirisho yale yale Yake.

Hamna kilichobaki kwetu ila kuliamini, na kwa Kuliamini ndiyo hakika ya mambo inayoumba Imani Kamilifu. Sikiliza hilo tena, KWA KULIAMINI NDIYO HAKIKA YA MAMBO INAYOUMBA IMANI KAMILIFU.

Je! kunacho kiungo katika mwili wako kinachotilia shaka hata Neno moja: HAPANA
Je! unaamini kila Neno: Ndiyo
Je! Amekupa Ufunuo wa Ujumbe huu: Ndiyo
Je! Ni Bibi-arusi peke yake ndio watakaokuwa na huo Ufunuo wa kweli: Ndiyo
Je! unajua wewe ni Bibi-arusi Wake: Ndiyo
Je! Alisema kwa kuamini kila Neno itakupa Imani Kamilifu: Ndiyo
BASI WEWE NDIYE BIBI-ARUSI-NENO MWENYE IMANI KAMILIFU!!

Ee Bwana tuandae zaidi ya wakati mwingine tunapokusanyika pamoja Jumapili hii kusikia Neno lako. Tusaidie tusijitazame wenyewe tena, bali tu kuamini Neno Lako ulilonena kwa ajili yetu. Tumeuona Mvuto wa Tatu ukitenda kazi nasi tunajua unakaa ndani yetu. Yatubidi tuwe tunalinena na kuliamini Neno Lako.

Tunajua unamjia hivi karibuni Bibi-arusi-Neno Wako mkamilifu. Lolote tunalohitaji, Baba, LOLOTE TUNALOHITAJI, tunajua tutalipokea. Kwa maana Ni Neno Lako ambalo umekwisha kulinena kwa ajili yetu. Hakuna lingine lakufanya ila KULIAMINI tu. Tunaliamini Baba, tunaliamini. Sasa hebu na tulitendee kazi NENO LAKO.

Tunakiri kushindwa kwetu, dhambi na makosa yetu yote. Tutazame kupitia Damu ya Mwanao ambapo tunahesabiwa haki kwa Neema na rehema zako. Jalia kuwe na badiliko ndani ya Bibi-arusi Wako zaidi ya hapo awali. Na Utumiminie Roho wako Mtakatifu na kutupa yote tunayohitaji.

Wagonjwa wataponywa magonjwa yote. Aliyerudi nyuma atarudi kwenye Neno. Bibi-arusi wako ulimwenguni kote wataona njia yako iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii na kuamini.

Kama huna mtu wa kukuwekea mikono…wewe jiwekee mikono yako mwenyewe…wewe ni mwaminio. Umekuwa Neno; unakuwa Neno, unapolipokea Neno.

Njoo Bwana Yesu, Bibi-arusi Wako anajiweka mwenyewe tayari kwa kukaa katika uwepo wa Neno Lako, kuivishwa. Tunataka kupambwa na kuvikwa kwa Neno lako.

Njoo ututie mafuta zaidi ya hapo kabla Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) wakati sehemu ya Bibi-arusi wako inapokusanyika kukusikiliza WEWE ukinena na kutufunulia jinsi ya kupata: Imani Kamilifu 63-0825E.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Marko 11:22-26 / 16:15-18
Yohana 14:12 / 15:7
Waebrania 11:1 / 4:14
Yakobo 5:14
1 Yohana 3:21