23-1217 Ile Ishara

UJUMBE: 63-0901M Ile Ishara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kipenzi Changu,

Moyo wangu unabubujika tu ninapowaona ninyi nyote mkikusanyika pamoja kuizunguka Sauti Yangu, mkisikia Neno Langu, ninapozungumza nanyi kupitia malaika Wangu.

Inanifurahisha sana kujua kwamba mnao Ufunuo wa ni nani niliyemchagua kuwa Sauti Yangu kwenu. Kuamini kila Neno alilonena halikuwa neno lake, bali Neno Langu kwenu.

Hiyo ilikuwa ni ya muhimu sana Kwangu, Nikaifanya irekodiwe na kuhifadhiwa kwa ajili yenu, ili mweze kuisikia tena na tena. Sikutaka kamwe msahau nilichosema kutoka moyoni Mwangu. Nilijua ya kwamba hiyo ingekuwa ndio njia pekee ningeweza kuwapa ninyi ile Imani Kamilifu mliyohitaji, ili tuweze kuwa pamoja.

Daima nimemtumia mtu mmoja kunena na kulifunua Neno Langu kwa Bibi-arusi Wangu. Jinsi ile tu nilivyofanya na Musa. Kile alichoagiza, ndicho alichopata, kwa maana alinena tu Maneno Yangu. Hata nilimwambia yeye, nitakufanya wewe mungu. Utakuwa mungu, na Haruni atakuwa nabii wako. Nitachukua sauti yako, nami nitaumba kwa kukutumia wewe. Nami nitanena, nao watu hawawezi kuikana. Lolote UTAKALOSEMA, litatendeka.

Sasa mmeipata Imani Kamilifu katika Neno Langu, si kwamba mnatambua tu ni nani Niliyewatumia kuwa Sauti Yangu, lakini sasa mnatambua kwamba Neno Langu linaishi na kukaa ndani yenu, hilo limekupa IMANI KAMILIFU.

Mnajua ninyi ni nani.
Mnakaa ndani Yangu, na Neno Langu ndani yenu. Ombeni mtakalo; nanyi mtapewa. katika Jina Langu mtatoa pepo; si, Mimi nitatoa, NINYI MTATOA. Kama NINYI mkiuambia mlima huu; si kama Mimi Nikiuambia, Kama NINYI mkiuambia mlima huu.

Adui yako hana nguvu tena juu yako. Wewe na Neno Langu ni MMOJA. Ikiwa una watoto ama wapendwa wako ambao hawako mahali wanapopaswa kuwa, wadai. Kama Ilifanya kazi kwako, basi itumie IMANI yako KAMILIFU katika NENO LANGU KAMILIFU linalokaa ndani yako, nawe waweza kupokea uombacho.

Lo, nimengoja kwa muda mrefu sana wewe kujitambua ni nani. Kukuona ukijiweka mwenyewe tayari kwa kulisikia Neno Langu. Nimefurahishwa sana hatimaye wakati huo umefika.

Hilo Neno Kamilifu nililonena na kuwahifadhia ninyi ndilo Ishara Yangu kwa kila mwamini leo. Ni Roho Mtakatifu; si damu, kemia, bali ni Roho Wangu Mtakatifu, Neno Langu, linaloishi na kukaa ndani yenu.

Saa ambayo hiyo Ishara haina budi kuonyeshwa waziwazi imewadia. Huna budi kuibeba Ishara pamoja nawe usiku na mchana; sio tu Jumapili, huna budi Kubonyeza Play wakati wote.

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni!

Nje huko kuna jumbe nyingi, lakini Sauti Yangu ndio Ujumbe wa wakati huu. Huna budi kupokea na kuamini kila Neno. Haina budi kuwekwa wakati wa jioni.

Ninyi kote ulimwenguni, mnaosikiliza kwenye kanda, ishara ya wakati huu iko hapa. Kuna Ishara ambayo haina budi kuwekwa, na haingalikuja wakati mwingine wo wote …mnalipata?

Njoo uiweke ile Ishara Yangu maishani mwako pamoja na Bibi-arusi wangu Jumapili hii saa 6:00 saa SITA MCHANA, saa za Jeffersonville (Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) tunapousikia Ujumbe Wangu kwa Bibi-arusi: ile Ishara 63-0901M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mwanzo 4:10
Kutoka sura ya 12
Yoshua sura ya 12
Matendo 16:31 / 19:1-7
Warumi 8:1
1 Wakorintho 12:13
Waefeso 2:12 / 4:30
Waebrania 6:4 / 9:11-14 / 10:26-29 / 11:37 / 12:24 / 13:8, 10-20
Yohana 14:12