21-1219 Ile Ishara

UJUMBE: 63-0901M Ile Ishara

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi wa Ishara,

Haijawahi kutokea wakati kama huu hapo awali katika historia ya ulimwengu. Ulimwengu wote ulilazimika kushuhudia jambo hilo, kwani sayari tano zilijipanga zenyewe pamoja. Kuna jambo lililokuwa likitukia mnamo Desemba 12, 2021 katika mbingu, huku jambo fulani likiendelea duniani. Bibi-arusi waliungana wenyewe pamoja kutoka ulimwenguni kote kama vile Mungu alivyonena kupitia kwa nabii Wake, na Bibi-arusi Wake alikuwa na Ushirika na Kutawazana Miguu kwa pamoja katika nyumba zao.

Ni hali na uwepo wa Bwana ulioje uliokuwa ndani ya nyumba zetu. Baadhi ya vijana wa kanda waliingia ndani ya nyumba zetu nasi tukaifanya nyumba yetu kuwa kanisa la Bwana. Tuliweka Ishara kwa nyumba zetu na kwa familia zetu. Roho Mtakatifu aliijaza nyumba yetu, mioyo yetu, na nafsi zetu kwa uwepo wake. Ilikuwa kana kwamba sisi ni wana wa Israeli tukijiandaa kwa safari yetu ya kutoka.

Neno lilikuwa likisema nasi kupitia malaika wake na lilitumika kwenye nyumba zetu. Mauti ilikuwa imetuzunguka, lakini tulijua tulikuwa salama na ingepita juu ya nyumba zetu. Tulikuwa tunajiandaa kuondoka kuelekea Nchi YETU ya Ahadi.

Hatujawahi kamwe kuhisi ukaribu kama tulivyohisi usiku ule. Tulijua jambo fulani Lilikuwa likitendeka. Tulijua alikuwa anatutayarisha kwa ajili ya Kuja Kwake, lakini ilibidi iwe wakati huu, siku hii, mwezi huu, mwaka huu. Kila kitu kilikuwa kikamilifu na mahali pake. Ilikuwa na maana. Ilikuwa inatokea kama ishara kwa ulimwengu.

Kila tukio la kiroho ni ishara kutoka kwa Mungu. Iweni waangalifu. Tazameni hilo, mnaona. Tazameni, kila tukio la kiroho, kila kitu kinachotendeka, ni ishara. Hatuko hapa kwa bahati. Mambo haya hayatendeki kwa bahati. Ni ishara. Ni ishara, kuingia—ingieni mahali pa salama, upesi. Nuhu alikuwa ishara kwa kizazi chake; Elija alikuwa ishara kwa chake; Yohana alikuwa ishara kwa chake. Mnaona? Kila kitu, Ujumbe wa wakati huu, ni ishara. Uchunguze, tazama unachofanya. Unaona? Ni ishara. Kila kitu kina maana yake.

Musa alipoanza huduma yake katika Israeli, kwa ishara kuu, waona, Israeli walikusanyika upesi toka kila sehemu ya Misri kuenda Gosheni, wakirudi nyumbani kwao, kwa maana walijua kitu fulani kilikuwa karibu kutukia. Lo, ni mfano jinsi gani!

Ni mfano mkamilifu jinsi gani leo hii, Bibi-arusi anapokusanyika kwenye Neno safi lisiloghoshiwa la wakati huu; kwa sababu sisi pia tunajua, kuna jambo linakaribia kutukia.

wanakuja kutoka Mashariki na Magharibi, Wanatoka nchi za mbali; Kula karamu pamoja na Mfalme, kula kama wageni Wake, kwenye Chakula Chake Kilichohifadhiwa MEZANI PAKE.

Alimtuma malaika Wake nabii akiwa na Ujumbe kumwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake kwenye Nchi ya Ahadi. Amejitambulisha Mwenyewe miongoni mwetu kwa Nguzo ya Moto. Kisha, Yeye ametuma Ishara Yake ili Bibi-arusi Wake akae chini ya hiyo, kwa maana Yeye anaitambua Ishara hiyo Pekee.

Ishara ni nini leo hii?

Yeye hutambua tu I—Ishara. Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Huo ndio Ujumbe wa siku hizi! Huo ndio Ujumbe wa wakati huu! Katika Jina la Yesu Kristo, upokeeni !

Bibi-arusi na Kristo wanakuwa Mmoja. Huduma ya Bibi-arusi, na huduma ya Kristo, ni sawa. Mungu Mwenyewe Anatambua Ujumbe wa mjumbe Wake. Amemtambua Bibi-arusi Wake. Hasi inakuwa chanya. Kila ahadi katika Neno Lake ni YETU. Ni lazima itutii.

Tunakuwa Bibi-arusi Neno mkamilifu kwa njia iliyoandaliwa na Mungu kwa siku ya leo: Sauti Yake, Neno Lake, kwenye Kanda. Mungu kamwe habadilishi mpango Wake. Daima amemtuma nabii kuwaongoza watu wake. Alikuwa na wengine walioitwa na kutiwa mafuta, bali wao wangeweza kusema TU yale nabii aliyosema, kwa maana Maneno yake yalikuwa BWANA ASEMA HIVI kwa watu.

Unawezaje kuwa na UHAKIKA asilimia 100% kwamba unalosikia ni Neno KAMILIFU la Mungu? Kuna njia moja tu kwangu mimi: Bonyeza Play.

Hakika kuna wengine ambao wameitwa kuhubiri Neno, kwa maana limo ndani ya Neno na haliwezi kupingwa, lakini wanaweza tu kuhubiri Neno ambalo wamesikia kwenye Kanda kutoka kwa mjumbe wa Mungu. Hawawezi kuhubiri, kufundisha, kufasiri, kuondoa au KUONGEZA CHOCHOTE KWAKE kwani ni NENO KAMILIFU LA MUNGU. Hivyo ndivyo Neno lisemavyo.

Si vibaya kumsikia mhudumu, kama wengine wasemavyo, wala si vibaya kwenda kanisani. Unapaswa kwenda kanisani, Lakini Bibi-arusi anataka kusikia chakula cha kondoo, na wengi wanaamini njia pekee ya kusikia Neno safi ni Kubonyeza Play.

Mungu awabariki na huduma yao Mungu aliyowaitia. Kwa maana mimi siko kinyume chao na ninawapenda nakuamini nitatumia Umilele pamoja na Bibi-arusi Wake wote aliyechaguliwa tangu awali. Mimi niko tu kwa ajili ya huduma ya kanda.

Wengi husema ni lazima uwe na mhudumu ili uwe Bibi-arusi. Ninakubali , ninaye , William Marrion Branham, kwa maana yeye ndiye mhudumu mkuu sana aliye na huduma kuu sana kuliko zote ulimwenguni. Kwa maana si neno lake, ujumbe wake, mawazo yake, wala si fasiri yake. Ndilo Neno pekee la Mungu lililothibitishwa kwa ajili ya Wakati wetu. Na ndiyo, ndio HUDUMA kuu sana HAI iliyopo .

Maswali yangu ni: Je! Unaweza tu kusikiliza Kanda na kuwa Bibi-arusi wa Kristo, au je, inanibidi kuwa na kitu zaidi ya Sauti ya Mungu kwenye kanda?

Mimi na nyumba yangu, sisi ni NYUMBA YA KANDA, na tunaamini sisi ni Bibi-arusi Wake na Kila TUNACHOHITAJI ni Sauti ya Mungu kwenye kanda.

Ikiwa ungependa kuungana nasi nyumbani kwako, kanisani, garini au popote pale ambapo Bwana yuko nawe, ili kusikia Bwana Asema hivi, uungana nasi Jumapili saa 3:00 Tatu asubuhi, saa za Jeffersonville, ( ni saa 11:00 kumi na moja jioni ya Tanzania), kusikia Neno la Mungu likimkamilisha Bibi-arusi Wake na kutuletea Ujumbe: Ile Ishara 63-0901M

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikia Ujumbe:

Mwanzo 4:10

Kutoka sura ya 12 yote

Yoshua sura ya 12 yote

Matendo 16:31 / 19:1-7

Warumi 8:1

1 Wakorintho 12:13

Waefeso 2:12 / 4:30

Waebrania 6:4 / 9:11-14 / 10:26-29 / 11:37 / 12:24 / 13:8,10-20

Yohana Mtakatifu 14:12