23-1203 Ninawezaje Kushinda?

UJUMBE: 63-0825M Ninawezaje Kushinda?

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Yungiyungi la Kidimbwini,

Jinsi gani mioyo yetu ilivyoruka kwa furaha Jumapili tulipomsikia Bwana wetu akinena na kutuambia kile kinachotendeka sasa hivi. Tunaungana na Neno na kuwa MMOJA Naye. Hivi karibuni sana tutaungana na watakatifu waliotutangulia kuwa WAMOJA nao. Kisha sisi sote pamoja tutaungana na Kristo kama MMOJA kwenye Karamu ya Arusi ya Mwana-Kondoo.

Ni furaha iliyoje iliyojaza nafsi zetu wakati Alipotuambia kuwazia kwamba katika dakika moja, katika kufumba na kufumbua jicho, ulimwengu hata hautajua kinachoendelea; lakini kwa ghafula, tutawaona mbele ya macho yetu wapendwa wetu walioondoka, nasi tutaungana nao tena.

Ni matarajio yaliyoje yanayojaza mioyo yetu kuwazia, kwa ghafula, tutawaona wamesimama mbele yetu baba zetu, mama zetu, kaka, dada, waume, wake, watoto, hata nabii wetu. TUTAWAONA, KATIKA MWILI!!

Tutajua papo hapo, hili NDILO; wakati umefika, tumefaulu, IMEKWISHA. Nena kuhusu changamko kwa Ufunuo!! Nikiliwazia na kulinena tu sasa hivi, naweza kuwasikia mkipaza sauti, UTUKUFU, HALELUYA, JINA LA BWANA LIHIMIDIWE.

Ni Wakati wa jinsi gani tunaokuwa nao, tukila barua hizi za mapenzi tulizoachiwa. Barua za mapenzi tunazoweza kuzichomoa wakati wowote tunapotaka na kuzisoma tena na tena na tena. Si hivyo tu, bali na KUBWA ZAIDI, tunaweza KUMSIKIA Bwana wetu Mwenyewe akisema kupitia midomo ya mwanadamu na kutuambia, “Nilizihifadhi barua hizi za mapenzi kwa ajili yako tu, kipenzi Changu. Nilijua wakati ungefika ambao ungehitaji kunisikia Mimi nikikuambia jinsi ninavyokupenda na kwamba wewe ni Wangu.”

“Nilitaka kukuambia kila siku adui anapokushambulia, unapopitia mitihani na majaribu yako yote, WEWE NI WANGU. Tayari nimelipa ile gharama. Tayari nimeshinda chochote kile…umenisikia kipenzi? CHOCHOTE unachokihitaji, nimekwisha kushinda kwa ajili yako, kwa sababu Nakupenda”.

“Nilikujua kabla hata ulimwengu haujawepo. Wewe ulikuwa sehemu Yangu WAKATI HUO. Hukumbuki hilo sasa, lakini Mimi ninakumbuka. Usisahau nilichokuambia, wewe ni Mwili wa Mwili Wangu, Roho wa Roho Yangu, Mfupa wa Mfupa Wangu”.

“Ule wakati umefika sasa ambao nimekuwa nikiwaambia. Hakutakuwa na huzuni tena, hakutakuwa na mitihani na majaribu tena; siku hizo zimekwisha. Sasa ni sisi sote tu pamoja Milele yote”.

“Jipe moyo. Endelea kusonga. Kule Kupambazuka kwa siku ile kumekaribia. Mvutano wote unaopitia kila siku ni wa kukuleta karibu na Mimi”.

“Wakati jambo lolote linapokujia, na unaanza kuhisi umevunjika moyo sana, umechoka na huwezi, na kuonekana kama huwezi kuendelea mbele, inakubidi usisahau kamwe, Mimi Niko hapo pamoja nawe. Neno Langu linaishi ndani yako. Wewe ni Neno Langu.”

“Niliwaambia, mnene Neno. Lo lote mtakalo, mkisali, aminini ya kwamba mtalipokea, nanyi mtalipata. Mtapewa jambo hilo. Tayari Mimi nimekwishawashindia jambo hilo”.

Maneno haya yanamaanisha nini kwetu. Yanatuhifadhi kila siku. Linaziinua Roho zetu na kutuweka katika ulimwengu wa Roho pamoja Naye. Tunamwishia tu Mungu na Neno Lake. Tuna kusudi moja, hilo ni Yesu Kristo. Nje ya Hilo, hakuna jambo lingine linalojalisha.

Tumelipata lile Ono. Pazia limevutwa nyuma nasi tunamwona Yeye, Neno Lake lililofanyika mwili, akizungumza nasi kupitia midomo ya mwanadamu. Tuna mapenzi na Neno hili, Ujumbe huu, Sauti hiyo.

Njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,( Ni saa 2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki ) upate uzoefu uliyo mkuu maishani mwako. Usikie jinsi ya kushinda kila vita ambavyo Shetani anatupa mbele yako. Ujaze moyo wako kwa furaha na shangwe kujua wewe ni Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Ndugu. Joseph Branham

63-0825M Ninawezaje Kushinda?

Maandiko ya Kusoma kabla ya ibada :

Ufunuo 3:21-22