22-0529 Imani Kamilifu

UJUMBE: 63-0825E Imani Kamilifu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi mwenye Imani Kamilifu,

Kwa mara nyingine tena, naona haiwezekani kuweka kwa maneno kile ambacho Ujumbe huu, barua za Upendo wa Mungu wa kibinafsi, zilizoandikwa kwa Damu Yake, zilizonenwa kwa Sauti Yake, zinamaanisha kwetu. Kila kitu kingine hakimaanishi chochote. Tunampenda kutoka ndani kabisa ya mioyo yetu na Ametupa Upendo Mkamilifu Kwa ajili yake . Hakuna kinachoweza kutuondoa kwenye Neno hilo. Hakuna uradhi mwingine katika maisha yetu zaidi ya kumsikia yeye akiwasiliana nasi kama Rafiki kwa rafiki.

Hata sio sisi, ni Yeye anayeishi ndani yetu, akijiita Mwenyewe. Ni kilindi kikiita kilindi. Furaha kamili ya Kubonyeza play na kumsikia Mungu akitumia sauti ya mwanadamu kutuambia, sisi ni wateule wake. Kutuambia alitupenda kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu; kwa maana alijua tungempenda kwa yote yaliyokuwa ndani yetu, na tungedumu kuwa waaminifu Kwake na Neno Lake.

Yote tunayohitaji, Ametupa. Hakuna kinachokosekana. Neno Lake aliliandika kwa namna ya barua na kulihifadhi kwa maelfu ya miaka ili aweze kutuambia Upendo wote uliokuwa moyoni Mwake kwa ajili yetu.

Ndipo upendo wake unakuwa mkuu zaidi kwetu alivyotuambia: “Nitakuja katika mwili mara nyingine tena na kunena nanyi mdomo kwa sikio ili kusiwe na kutokuelewa, kusiwe na Mkanganyiko , kusiwe na haja ya fasiri. Nitachukua muda Wangu na kuwaeleza Upendo Wangu kwenu , nanyi mtaweza kuusikia tena na tena na tena. Nataka mjue, Baba yu ndani Yangu, Mimi niko ndani yenu, ninyi mko ndani Yangu, sisi ni MMOJA. Mwili wenu ni Mwili wangu, mfupa wenu ni Mfupa wangu, roho yenu ni Roho yangu.

Nitawaambieni yote yaliyo ndani ya Moyo Wangu kwa undani sana. Nitaliweka wazi hivi kwamba mtajua bila shaka, Maneno niliyoandika na kunena ni kwa ajili yenu, na hayatashindwa kamwe.

Nitawapa Imani Kamilifu, na Itakuwa ni Mtawala wa kila hali. Haidhuru adui anasema nini, italitawala mkiwa na Imani Kamilifu katika kile Neno Langu linasema mlicho. Haidhuru adui anajaribu kuwaambia nini, hata Msimsikilize. Masikio yenu ni bubu kwa kitu kingine chochote isipokuwa kile ambacho Roho Wangu amekwisha waambieni. Kimetia nanga mioyoni mwenu, na hakuna kitu kitakachowafanya mtoke Kwake.”

Imani hiyo Kamilifu tuliyo nayo katika kuujua Ujumbe huu kuwa ni Bwana Asema hivi, tunaitumia IMANI hiyohiyo KAMILIFU kwa kila ahadi aliyotuambia ni yetu katika Neno Lake. Ikiwa sisi ni wagonjwa na tunahitaji uponyaji, ni wetu. Ikiwa tunahitaji chochote, tunaweza kukipata, kwa kuwa tumetiwa mafuta na Roho Wake. Sisi ni masihi Wake watiwa mafuta wa siku za mwisho, tukionyesha ufufuo wa Yesu Kristo.

Ni tendo la Mapenzi anapojimwaga Yeye mwenyewe ndani yetu. Tunakuwa mmoja Naye kwa ajili ya Karamu hiyo kuu ya Arusi. Roho wake yuko hapa pamoja nasi na ndani yetu. Tuna jambo moja tu la kufanya, nalo ni kuliamini, kulikubali.

Sisi sio Malaika-Mjumbe wa 7 wa Mungu, lakini sisi ni wana na binti zake. Mikono yetu ni Mikono yake. Tunaamini kile kinachonenwa kwenye kanda kuwa ni Bwana Asema hivi. Ni Neno lililo hai.

Nabii wake ndiye mchungaji wetu. Tunaposikiliza Neno lililorekodiwa, tunaamini ni Mungu anayezungumza nasi moja kwa moja. Tuna Imani Kamilifu tukiamini hivyo.

Tunapokusanyika pamoja ulimwenguni kote kumsikiliza Mungu akizungumza nasi kwa njia ya nabii Wake, imani yetu inainuliwa juu zaidi na zaidi Mungu anapomkusanya Bibi-arusi Wake pamoja kwenye Neno Lake lililothibitishwa.

Kesho haitakuwa kama siku nyingine. Tutachukua Imani yetu Kamilifu Aliyotupa na tutaitumia kwa chochote tunachohitaji, nasi tutakipokea wakati Nguzo ya Moto inaponena kupitia mjumbe Wake mteule na kutuambia:

Je, mumeelewa na hayo niliyowatendea? Ninyi mumeniita “mchungaji wenu”; nanyi mwanena vema, maana ndivyo nilivyo. Ikiwa mimi, niliye mchungaji wenu, nimekwisha tambulishwa na Yesu Kristo, ya kwamba mimi ninatenda kazi Yake, basi aminini Neno langu. Kwa kutenda hili tendo la imani, kwa kuweka mikono yangu juu yenu , nimekwisha kuhukumu magonjwa na mateso yanayowasumbua. Aminini hayo, ndipo mtatimiziwa haja zenu, hata ziwe ni nini, kwa maana mambo yote yanawezekana kwa hao waaminio . Na mnapoomba, aminini ya kwamba mmepokea mlichoomba . Nami naamini kabisa ya kwamba napokea, na moyoni mwangu napokea uponyaji wa kila mmoja wenu, naupokea, ya kwamba umetendeka. Naamini, naamini hayo kwa yote yaliyo ndani yangu .

Tunaamini kwa yote yaliyo ndani yetu, Ujumbe huu kuwa ni Sauti ya Mungu, iliyonenwa, iliyorekodiwa, iliyothibitishwa na kuhifadhiwa kwa ajili ya siku hii. Tunaamini lo lote tuombalo, tutapokea, kwa kuwa ni BWANA ASEMA HIVI NI LETU.

Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA , saa za Jeffersonville (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI Ya Tanzania),ili kupokea chochote unachohitaji tunapomsikiliza nabii wa Mungu akituambia jinsi ya kupokea: Imani Kamilifu 63-0825E .

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma Kabla Ya Ibada :

Marko Mtakatifu 11:22-26 / 16:15-18
Yohana Mtakatifu 14:12 / 15:7
Waebrania 11:1 / 4:14
Yakobo 5:14
1 Yohana 3:21