22-0102 Yakini

Ujume: 62-1230m Yakini

PDF

pakua

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi arusi wa Ujumbe wa Mtu Mmoja,

 Huu Umekuwa mwaka Mkuu jinsi gani kwa Bibi-arusi.  Ametuunganisha kutoka ulimwenguni kote kwa kitu pekee kinachoweza kuleta Bibi-arusi Wake pamoja, Ujumbe wa wakati huu, Sauti yenyewe ya Mungu ikimwita Bibi-arusi Wake atoke .

 Na sasa, naamini uko tayari kugonga kilele kile cha mwisho kule kuleta imani ambayo italinyakua Kanisa hata Utukufuni; na lipo katika hizo Jumbe!

 Ufunuo wa Ujumbe huu sasa umetia nanga ndani kabisa ya mioyo yetu.  Matendo yetu yanaambatana kabisa na Neno.  Tunajua fundisho letu ni kamilifu na Neno, haliongezi chochote Kwake wala kuondoa lolote Kwake.  Kwetu sisi, si kingine ila Neno kwenye kanda.

 Amekuwa akitutayarisha kwa ajili ya kilele cha mwisho kwa kutupa Imani tunayohitaji kwa ajili ya Unyakuo.  Imani hiyo, iko ndani yetu SASA.  Uhai wa Kristo umezalishwa karibu katika njia ya kufanyika mwili, kupitia sisi, kama ilivyokuwa ndani ya Kristo.

 Tunaweza kuona maisha yake.  “Kazi nizifanyazo mimi nanyi mtazifanya, yeye aaminiye.”  Si yeye ajifanyaye anaamini, si yeye ajidhaniaye kuwa anaamini, bali, “Yeye aaminiye.”  “Yeye aniaminiye Mimi, kazi nizifanyazo Mimi yeye naye atazifanya.”  Kwa nini?  Ametiwa nanga kwenye Mwamba uleule.  Mwamba ulikuwa nini?  Neno, daima.  Umetiwa nanga hapo.  Ni Nyota yako ya kaskazini unapopotea baharini .

 Tumetia nanga sana kwenye Mwamba huo.  Tuna hakika nalo.  Tumeyakinika nalo.  Hatuchukui Neno la mtu mwingine, tunadumu na Bwana Asema hivi.  Tumekuja kwenye Yakini Yetu.

 Tumeridhika kabisa na tumetosheka. Hakuna kushangaa tena kama ilivyokuwa katika siku za Waamuzi, na kwa walio wengi sana leo, ambapo kila mtu alifanya lililo sawa machoni pake mwenyewe, ambapo kila mtu alikuwa na yakini yake mwenyewe na kufanya yale tu aliyotaka kufanya.  Mungu habadilishi kanuni zake, hawezi na awe Mungu.  Ikiwa Mungu atawahi kusema lolote au kufanya jambo lolote, ni lazima afanye vivyo hivyo kila wakati.

 Mungu daima hutuma nabii kuwaongoza watu wake.  Alitutumia Nabii Wake malaika wa 7 ;  Mwana wa Adamu akijifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu, kumwita Bibi-arusi Wake atoke na kumwongoza .  Kanda ni Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake.  HIYO NDIO YAKINI YETU.

 Akapanda akaenda kule…Alijua…Nami napenda hilo, jinsi alivyokuja; alifikia kwenye yakini yake, nguzo yake ya kujishikilia.

 Mungu anamwita Bibi-arusi Wake pamoja. Yeye Hatabadilisha mpango Wake. Yeye Hatatuma kundi la watu kumkusanya Bibi-arusi Wake.  Bibi-arusi Wake ataungana tu kwenye Neno safi, hiyo ni Sauti ya Mungu kwenye hizo Kanda.  Ni huduma ya kweli ya Mungu kwa ajili  ya siku hii .

Hakuna njia bora ya kuanza Mwaka Mpya kuliko kukusanyika pamoja na kusikia nguzo yetu yakushikilia , Yakini yetu, ikizungumza nasi. Ningependa kuwaalika kila mmoja kuja kusikiliza pamoja nasi Jumapili saa 4:00 nne Asubuhi ., saa za Jeffersonville,( ni Saa kumi na mbili jioni ya Tanzania), ili kusikia Ujumbe: Yakini 62-1230M.

 Kama hamwezi kuungana nasi, ninawatia moyo kuchagua Ujumbe wa kucheza katika nyumba zenu, au mtie moyo mchungaji wenu kuchagua Ujumbe ambao ninyi pia mnaweza kuketi  pamoja, chini ya upako huu mkuu uliopo, na kusikia yakini ya Bibi-arusi iliyothibitishwa.

 Ndugu.  Joseph Branham