26-0614 Nawe Hujui

UJUMBE: 65-0815 Nawe Hujui

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waliochaguliwa,

Kuzaliwa upya ni Kristo, ni ufunuo. Mungu amekufunulia siri hii kuu, na huko ndiko Kuzaliwa upya. Sasa utafanya nini ukileta kundi hilo lote pamoja? ambapo ufunuo unapatana kikamilifu,

Mungu analikusanya pamoja kundi Lake lote la Tai kwa upatano mkamilifu, akilifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake.

Ile njia ya Mungu ya kuwa na mfalme, kama Daudi alivyokuwa, ilikuwa sawa, nawe una nia moja iliyowekwa kule. Kama kiongozi mmoja na kundi la bata, na kadhalika, huwezi kuchukua wawili ama watatu wao. Kisha, unawatatiza wote pamoja, unatokea na wazo la namna yo yote.

Basi tunapaswa kufanya nini, Bwana?

Jambo tu likupasalo kufanya ni kuifanya Sauti Yangu ijulikane; wao wanaijua, kwa maana kondoo Wangu wanaijua Sauti Yangu.

Sauti Yako Kamilifu ni ipi kwa ajili ya siku hii, Bwana?

Kama niliwaudhi kwa kusema hivyo, nisameheni, lakini, nilihisi kwamba huenda mlichukizwa, bali, Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu.

Tunaliamini hilo kwa mioyo yetu yote. Hivi ndivyo sisi tunavyojisikia, Bwana.

Si lazima wathibitishe lo lote kisayansi, ama kumuuliza Msadukayo ye yote ama Mfarisayo, ama cho chote kile, juu ya jambo hilo. Nilisema hilo, wao waliamini, kwa maana kondoo Wangu huisikia Sauti Yangu.

Sauti iliyo kwenye kanda ni nini kwa Bibi-arusi Wako?

Hili ndiyo ile Sauti ya Mungu kwa jinsi ya herufi, kwa maana Hili ndilo ufunuo wote wa Yesu Kristo, Agano la Kale na lile Jipya yakiwekwa pamoja. Amina. Haya basi.

Je, kanda zingali bado ni muhimu leo?

Nami najua ya kwamba, baada ya kuondoka kwangu kutoka dunia hii, hizo kanda na vitabu vitaendelea kuwepo, na wengi wenu ninyi watoto wadogo mtaona, katika siku zijazo, ya kwamba jambo hili ni Kweli kabisa,…

Bwana, tunaamini kanda na vitabu ndio huduma Yako iliyo hai, iliyo mubashara ambayo umemwachia Bibi-arusi Wako.

Kwa nini hizo kanda ndio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI kwetu kuisikia?

Tuko katika wakati wa udanganyifu sana tuliopata kuishi ndani yake. “Utawapoteza walio Wateule kama yamkini,” kwa maana wana upako, wanaweza kufanya cho chote kama wengine wao.

“Ye yote atakayeongeza Neno moja kwenye Hili, ama kuondoa Neno moja kutoka Kwake.” Huna budi kuwa na mkataa mahali fulani.

Kwa hivyo, Mkataa wetu unabidi kuwa Neno la Mungu. Wewe umetufunulia kwamba Neno la Mungu na Sauti ya Mungu ni kitu kimoja. Sauti ni mawazo halisi ya Mungu yaliyonenwa, kama vile ulivyofanya kwa manabii wakati ulipoiandika Biblia; bali katika siku hii ya mwisho, Ulilihifadhi Neno Lako, Sauti Yako, kwa kuirekodi na kuiweka kwenye kanda. Kwa hivyo, Sauti Yako iliyonenwa kwenye kanda ndio mkataa wa Bibi-arusi.

Watu hawafikiri kuwa ni muhimu kuicheza Sauti kanisani mwao leo. Wao wanafundishwa makanisani mwao kwamba Ndugu Branham hakuwahi kamwe kusema wazicheze kanda kanisani, wao wanahitaji tu kuwasikia wahudumu wakihudumu na kulinukuu Neno.

Na kama kanisa ndilo neno lako la mwisho, hujali kamwe yale mtu ye yote anayosema. Hilo ndilo neno lako la mwisho. Ee Mungu, saidia jambo hili likolee ndani! Kwangu mimi, jambo lote ni makosa. Neno la Mungu ndilo mkataa. Lo lote Neno hilo lisemalo, basi hilo ni sahihi.

Yeye alikuwa akingojea wamkaribishe. Hilo ndilo analongojea usiku wa leo, wewe kumkaribisha.Basi angalia wakati hao wanafunzi walipomkaribisha katika ushirika wao mezani,

Anawezaje mtu yeyote kusema, kuhalalisha, au kutoa udhuru, anayetangaza kwamba anauamini Ujumbe huu wa wakati wa mwisho, kutokuzicheza kanda makanisani mwao wakati wanayo nafasi ya kuisikia SAUTI HALISI YA MUNGU? Ndio Maneno ambayo Mungu aliyonena kupitia midomo ya mwanadamu kupitia nabii Wake aliyetiwa mafuta. SAUTI PEKEE iliyothibitishwa na Nguzo ya Moto, iliyothibitishwa kwa kujua siri za moyo, iliyothibitishwa kwa ishara na maajabu, kwamba NDIO Sauti ya Mungu kwa kizazi hiki.

Angewezaje mtu yeyote kutoa udhuru, maelezo YOYOTE, au kutokuwa na hamu ya kuisikia Sauti ya Mungu kila wanapokusanyika?

Bwana, nijalie kamwe nisiichukulie Sauti Yako iliyo kwenye kanda kijuu juu. Nijalie daima niutangazie ulimwengu Hiyo ndiyo Sauti PEKEE wanayohitaji kuisikia. Nijalie nimtangazie Bibi-arusi Wako, SAUTI YAKO ILIYO KWENYE KANDA NDIO TU WANAYOHITAJI.

Tunapenda kufanya ushirika. Tunapenda kuzungumza kukuhusu Wewe na kulinukuu Neno Lako, lakini hakuna kitu kilicho kikuu zaidi ambacho Wewe ungeweza kufanya kwa ajili ya Bibi-arusi Wako kuliko kutupa sisi Neno Lako juu ya Neno, Ufunuo wa Sauti Yako, na kisha kutambua SISI NI NANI, BIBI-ARUSI WAKO MWAMINIFU.

Jinsi gani ningeweza kuendelea na kuendelea, nikishiriki kuhusu ufunuo mkuu ambao Mungu ametupa sisi. Hakuna mwisho; lakini jambo lililo kuu zaidi ambalo ningeweza kufanya ni kukualika uje uisikie wewe mwenyewe Sauti ya Mungu pamoja na sehemu ya Bibi-arusi Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia: 65-0815 – Nawe Hujui.

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:
Ufunuo 3:14-19
Wakolosai 1:9-20