26-0531 Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

UJUMBE: 65-0801M Mungu Wa Wakati Huu Mwovu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kundi dogo, Bibi-arusi Neno Bikira wa Kristo:

Jinsi gani mioyo yetu ilivyofurahi tulipomsikia malaika Wake mwenye nguvu akitangaza kwamba sisi ndio Uzao wa Mungu uliochaguliwa tangu asili ambao hauwezi kutenda kitu kingine chochote ila kuifuata Sauti Yake. Ni zaidi ya maisha kwetu sisi. Unaweza kuyatwaa maisha yetu, lakini huwezi kuichukua Sauti Yake. Sisi ni Mmoja na Neno Lake. Sisi ni Mmoja na Sauti Yake. Sisi ni Mmoja na Yeye.

Inaonekana la kushangaza kwetu sisi kwamba tunaeleweka vibaya na kudhihakiwa kwa sababu tunasema tunaamini katika kuzicheza kanda; kwamba ni Sauti ya Mungu ikinena na Bibi-arusi Wake. Shetani amewafanya watu kudanganywa sana hivi kwamba wanadhani kwa sisi kutangaza kwamba sisi ni kanisa la kanda, ati ni jambo fulani lililo kinyume na Neno, jambo fulani la makosa, na ati tunapotoshwa, huku wakati wote Ndio njia kamilifu ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake.

Inawezaje kuwa njia nyingineyo? Ukilifasiri vibaya Neno moja lililonenwa, umepotea. Wao wanaweza kuwa na nia na lengo sahihi, bali wawe wamekosea. Mtu anaweza kuwa ametiwa mafuta na Roho Mtakatifu na bado awe amekosea.

Kama Mungu hangekuwa ameiandaa njia ambayo Bibi-arusi Wake wangeweza kusikia wao wenyewe kila Neno, basi kungekuwa na haja ya njia nyingine. Bali Yeye ameiandaa njia kwa kila mwanadamu duniani kupata fursa ya kulisikia Neno likizungumza nao moja kwa moja bila kuhitaji fasiri, maelezo, au ufafanuzi. Yote ni Bwana Asema Hivi…MWISHO WA MANENO!

Sote tunakubaliana kwamba ni lazima tudumu na Neno ili tuweze kuwa Bibi-arusi Wake.

Ninaamini ya kwamba kila kitu tunachohitaji kimeandikwa papa Hapa, kinahitaji tu kufasiriwa na Roho Mtakatifu. Siamini ya kwamba mtu ye yote duniani ana haki ya kuweka fasiri yake kwenye Neno. Mungu hahitaji mtu ye yote kulifasiri Neno Lake. Yeye ndiye anayejifasiria. Alisema angefanya jambo hilo, Naye hulifanya.

Waziwazi, Bwana amenena na kumfunulia Bibi-arusi Wake kwamba hakuna njia nyingine ya kuwa Bibi-arusi Wake mteule ila kudumu na Neno Lake. Mungu Mwenyewe hulifasiri Neno Lake Mwenyewe, na hakuna mtu aliye na haki ya kuongeza fasiri yake Kwake.

Neno pia linasema kwamba NABII Wake ndiye mfasiri wa Neno Lake. Yeye ni Sauti ya Mungu kwa watu. Kile yeye asemacho ndilo Neno la siku yetu.

Kwa kuisikiliza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda, sisi ni unabii unaotimizwa.

Hakuna kilicho na nguvu zaidi, kitakatifu zaidi, hakuna kinachotimiza zaidi, hakuna kilicho kikamilifu zaidi kuliko kuisikiliza Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ikizungumza nawe.

Wakati wengine wanaweza kusema jambo hilo halina lolote, tai wanakusanyika na kushangilia kwa furaha kubwa mno, wakiwa na uhakika kwamba wanalishika Neno la Mungu. Alituambia kama una kinasasauti, likusanye kundi la watu pamoja, na ukaicheze, na msikilize kwa makini. Kwa neema na rehema Zake, hicho ndicho hasa tunachofanya.

Mungu ametuita kutoka katika wakati huu mwovu kwa ajili ya Jina Lake. Tunapitia mitihani na majaribu mengi ambayo hayajawahi kutokea. Shetani yuko katika mashambulizi kwani anajua wakati wake umekwisha. Unaweza kujiuliza, nawezaje kupitia mambo haya yote, na huku mimi ni Bibi-arusi Wake?

Unadhihirishwa, unajaribiwa, na kumthibitishia Shetani, SISI NI BIBI-ARUSI WAKE YEYE. Sisi ni Neno lililo katika mwili. Tunaweza kunena Neno nalo litatimia. Ni BWANA ASEMA HIVI.

Tuna Sauti ya Mungu ikizungumza moja kwa moja na Shetani na kumwambia:

Shetani, umeshindwa. Wewe u muongo. Na, kama mtumishi wa Mungu, na kama watumishi, tunakuamuru ya kwamba katika Jina la Yesu Kristo, ya kwamba utii Neno la Mungu na utoke ndani ya watu, kwa maana imeandikwa, “Katika Jina Langu watatoa pepo.”

Lolote…LOLOTE tunalohitaji, tunahitaji tu kuomba, kuamini na kukaa papo hapo. Linaweza kudhihirika mara moja; yaweza kuwa wiki, mwezi, mwaka. Haijalishi kile tunachokiona au kuhisi, LIILITUKIA PAPO HAPO.

Kila ibada tunayokusanyika pamoja inazidi kuwa Kuu zaidi na zaidi kwa Tai wa Mungu. Tumekusanyika katika nia Moja na kwa Umoja, tukiketi pamoja katika ulimwengu wa roho, tukiisikiliza Sauti ikizungumza nasi na kutukamilisha kwa Neno Lake.

Tungependa muungane nasi Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoisikia Sauti ya Mungu ikizungumza nasi kwa mara nyingine tena na kutuletea fasiri ya Neno Lake Mwenyewe.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: Mungu Wa Wakati Huu Mwovu 65-0801M

Maandiko ya kusoma kabla ya Kuusikiliza Ujumbe:
Mathayo Mt. sura ya 24 / 27:15-23
Luka Mtakatifu 17:30
Yohana Mt. 1:1 / 14:12
Matendo 10:47-48
1 Wakorintho 4:1-5 / sura ya 14
2 Wakorintho 4:1-6
Wagalatia 1:1-4
Waefeso 2:1-2 / 4:30
2 Wathesalonike 2:2-4 / 2:11
Waebrania sura ya 7
1 Yohana sura ya 1 / 3:10 / 4:4-5
Ufunuo 3:14 / 13:4 / sura ya 6-8 na 11-12 / 18:1-5
Mithali 3:5
Isaya 14:12-14