23-1126 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

UJUMBE: 63-0818 Wakati Wa Kuungana Na Ishara Yake

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mwili wa Mwili Wake, Neno la Neno Lake, Uhai wa Uhai Wake, Roho wa Roho Wake,

Ndugu na dada zangu wapendwa, Hebu someni kauli hiyo moja tena na tena. Someni kile Mungu Mwenyewe alichomaliza kuwaita. Hivi angewezaje mtu yeyote kuandika kwa maneno ya kibinadamu tu kuwa hayo yana maana gani kwetu. Haiwezekani kuyaeleza. Kama tungeweza kuyafahamu kikamilifu na kuyatumia, kwa mioyo yetu yote, nia na roho zetu zote, ninaamini kweli Unyakuo ungepaswa kutukia.

Kuna nini cha kuogopa? Kuna nini cha kuhofia? Shetani anatushambulia, anatutesa, anatutupia magonjwa, anashambulia akili zetu kwa kila namna ya mawazo mabaya, lakini hakuna kitu kinachoweza kutudhuru. Je, kuna jambo lolote linaloweza kumdhuru Yesu? HAPANA, basi wala hakuna kitu cha kutudhuru. Ndio kwanza Amesema: SISI NI Mwili Wake, Neno Lake, Uhai Wake, Roho Wake.

Ni furaha na uradhi uliyoje tulio nao mioyoni mwetu tunapotafakari yale ambayo Yeye amekuwa akituambia. Ufunuo ambao Mungu amekuwa akitufunulia, mzigo wa kanda, baada ya mzigo wa kanda, baada ya mzigo wa kanda. Roho Mtakatifu anabubujika ndani yetu kama Kisima kikuu kinachofoka maji.

Sisi tumechaguliwa tangu zamani Kuliona na Kulisikia. Hatuta na hatuwezi kuanguka wala kupotoshwa. Tuko njiani kukutana na Uongozi wetu, Mkombozi wetu, Mume wetu, Mfalme wetu, Bwana wetu, Mpenzi wetu, Mwokozi wetu, katika Mahali palipoandaliwa pa kukutania!

Hebu sikilizeni hili tena: Utimilifu kamili wa Uungu kwa jinsi ya mwili unakaa ndani YETU, Kanisa Lake, ule utangulizi. Yote aliyokuwa Mungu, aliyamimina ndani ya Kristo; na yote aliyokuwa Kristo, yalimiminwa ndani ya Kanisa; sisi, Bibi-arusi Wake. Sio jambo litakalotendeka siku moja, AMESEMA LINAFANYIKA NDANI YETU SASA HIVI.

Je, waweza kuwazia, tangu mwanzo kabisa wa wakati, Mungu hakuwahi kutoa siri Yake kuu ya ajabu ambayo ilikuwa niani Mwake kwa mtu yeyote, hadi leo hii. Kwa nini alifanya hivyo? Kwa sababu Yeye alikuwa anangojea kutujulisha SISI katika siku hizi za mwisho kama alivyoahidi. Alikuwa anatusubiri sisi. Alijua kuwa sisi ndio watu pekee tungaliweza, na tungeweza, KULIELEWA KIKAMILIFU….UTUKUFU!! !

Alituchagua sisi tuwe Bibi-arusi wake kwa sababu alijua kwamba hatutaanguka. Tungeshikilia Neno hilo haidhuru ulimwengu wote ungesema nini kulihusu. Tungeshikilia Neno hilo na NENO hilo PEKE YAKE! Sisi tumechaguliwa tangu zamani kusimama hapo. SISI tumefanywa wana wenye mamlaka na Yesu Kristo.

Kunayo mengi zaidi. Sikilizeni kwa makini….jichune. Kichwa (Mungu) na Mwili (Sisi) umekuwa kitu kimoja. Ni Mungu aliyedhihirishwa ndani YETU.

  • Mungu na Kanisa Lake wao ni MMOJA, “Kristo ndani YENU.”
  • Sisi NDIO Ufunuo Mkuu wa Mungu.
  • Sisi hata tunalibeba Jina Lake; Jina Lake ni Yesu, yule Mtiwa Mafuta.
  • SISI NDIO Mwili uliotiwa mafuta wa Kristo.
  • SISI TUNA mdhihirisha Mungu kama jinsi ule mwili ulivyofanya.

Sisi ndio Bibi-arusi Wake, tumetiwa mimba kwa Roho Wake. Kanisa, linalozaa watoto, lililotiwa mimba kwa Roho Wake likibeba Jina Lake; likibeba Uhai Wake. Tuna jibu la Shetani. Uongozi uko hapa. Kristo, Bwana aliyefufuka, yuko hapa katika Nguvu zile zile za kufufuka Kwake alizowahi kuwa, akijidhihirisha Mwenyewe ndani yetu, Bibi-arusi-Neno Lake Lililonenwa.

Mungu sasa anamuunganisha Bibi-arusi Wake pamoja. Anawaunganisha kutoka ulimwenguni kote kwa Neno Lake, jambo pekee litakalomleta Bibi-arusi Wake pamoja. Roho Mtakatifu anaongoza na kumkusanya Bibi-arusi Wake. Katika kila wakati, nabii alikuwa ndiye Roho Mtakatifu kwa ajili ya siku zao.

Liwazieni jambo hili. Wakati Watu wanaposema kuwa tunampa sifa nyingi mno malaika-mjumbe wa saba, kumbuka, Mungu Mwenyewe alizikabidhi SIRI ZAKE ZOTE alizokuwa nazo Niani Mwake kabla hata ulimwengu haujawepo, kwa malaika-mjumbe Wake wa saba. Mungu Mwenyewe alikuwa na imani na mtu huyu asilimia 100%, hata akauweka Mpango wake mkuu wa wakati wa mwisho mikononi mwake. Alimpa yeye…SIKILIZENI, AKAMPA YEYE Ufunuo wa siri Zake zote kwa mtu huyo. Alimpa mtu huyo Ufunuo wa mambo ambayo hata hayakuandikwa. Alisema chochote kile alichosema duniani kilikuwa ni muhimu sana, kingerudisha mwangwi mbinguni.

Hakuna tashwishi kwamba Mungu aliwatuma watu wakuu waliojazwa na Roho Mtakatifu katika ulimwengu huu. Lakini kila mmoja wa watu hawa, hata ikiwa wamejazwa na Roho Mtakatifu, wanaweza kuwa makosani. Mungu kamwe hakuthibitisha kile wanachosema kuwa Bwana Asema hivi, na kuwaambia muamini kila neno lao. Kulikuwa na mtu mmoja tu aliyekuwa na mamlaka hayo kutoka kwa Mungu, malaika-mjumbe Wake wa saba.

Unaweza, na unapaswa, kuwa na mchungaji. Lakini kama huyo mchungaji hakuambii ya kwamba SAUTI YA MUNGU iliyo kwenye kanda ndiyo SAUTI iliyo MUHIMU SANA KUSIKIA, na kuipa nafasi ya KWANZA mbele yenu kwa kusikiliza kanda pamoja nanyi, si kwamba tu yeye awaambie ati nabii anasema hivi, basi mchungaji mliye naye hafai.

Yeyote anayekuongoza, hata kama unadai kuwa ni Roho Mtakatifu, ni afadhali awe anakuunganisha na Ujumbe huu, Ile Sauti, kwani Ndiyo sauti Pekee inayoweza kusema, “MIMI NI SAUTI YA MUNGU KWENU”.

Kama umechaguliwa tangu zamani Kuliona, Utaliona. Ikiwa hujachaguliwa tangu zamani Kuliona, hutaliona kamwe; hujaandikiwa kuliona.

Tunaona mataifa yakiungana, tunaona ulimwengu ukiungana, tunaona makanisa yakiungana. Tunaona Bibi-arusi akiungana, akiungana na Neno. Kwa nini? Neno ni Mungu. Na kama Neno…Kama vile Bwana Arusi (akiwa ni Neno), na Bibi-arusi (akiwa ni msikiaji wa Neno), wanakuja pamoja katika Muungano. Wanaungana kama vile arusi. Unaona, wanajiandaa kufanya arusi, nao—nao wanakuwa mmoja. Neno linakuwa wewe, wewe unakuwa Neno. Yesu alisema, “Katika siku hiyo mtaijua. Yote aliyo Baba, ndivyo nilivyo Mimi; na yote niliyo Mimi, ndivyo mlivyo ninyi; na yote mliyo ninyi, ndivyo nilivyo Mimi. Katika siku hiyo mtajua ya kwamba Mimi niko ndani ya Baba Yangu, Baba ndani Yangu, Mimi ndani yenu, nanyi ndani Yangu.”

Ninawaalika mje kuungana nasi kuizunguka Sauti ya Mungu Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, ( ni saa2:00 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki), tunaposikia, Wakati Wa Kuungana na Ishara Yake 63-0818

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya ibada:

Zaburi 86:1-11
Mathayo 16:1-3