26-1101 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2

Ujumbe: 60-0518 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Mpenzi,

Je, mko tayari, enyi wana na binti za Mungu wenye mamlaka na mliodhihirishwa, kuketi pamoja katika ulimwengu wa roho, kuungana na Bibi-arusi kutoka kote ulimwenguni, kuisikia Sauti ya Mungu ikisema nanyi mdomo kwa sikio?

Ndiyo!!! Tuko tayari kuisikia Sauti ya Mungu ikituambia sisi ni nani hasa.

Nawaiteni ninyi “mpenzi” kwa kuwa ndivyo mlivyo. Ninyi—ninyi ni wapenzi wangu. Mwajua nini? Hebu… Hili hapa Andiko limekuja. Paulo alisema, “Nawaonea ninyi (Kanisa Lake) wivu, wivu wa Mungu, kwa kuwa nimewaposea.” Haya basi, huyo amelipata. Ndilo hilo. “Kwa kuwa nimewaposea, nimewaposa kwa Kristo, kama bikira safi.”

Utukufu kwa Mungu, malaika Wake ametuposa Kwake Yeye. Sisi ni mabikira safi kwa Neno Lake, Ujumbe huu, kwa Sauti Yake iliyo kwenye kanda. Sasa tumeposwa kwa Kristo.

Tutakuwa tayari na kusubiri kwa hamu kubwa Jumapili. Tutauma kidole chetu, tutafinya nafsi zetu, na kuifanya thabiti mioyo yetu. Tutapiga kelele kwa mara nyingine tena, tukimsifu Bwana, tukipaza sauti “amina, haleluya”, kama vile nyota za asubuhi zilipoimba pamoja na wana wa Mungu walipopiga kelele kwa furaha; walipouona mpango wa wokovu, Mungu alipoyaweka majina yetu kwenye Kitabu Chake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Je, hivi tunaweza kuelewa kwamba Baba Mungu ametusubiri, tangu mwanzo wa ulimwengu, hadi leo hii, SISI? Yeye aliona mahali ambapo tungedhihirishwa katika siku za mwisho, naye amekuwa akingojea na kuugua ili tuinuke kwa nguvu za Roho Mtakatifu kutufunulia mambo ya siri ambayo yamefichwa hadi leo hii.

Kote katika nyakati zote, manabii wamengojea kufikia hadi siku hizi za mwisho ili mambo haya yaonekane. Baba Mungu alisema Yeye amelingojea Kanisa Lake likue kutoka wakati wa Kilutheri, wakati wa Kibatisti, wakati wa Kimethodisti, wakati wa Kipentekoste, na sasa tuko moja kwa moja kwenye kule kuwekwa kwa lile Jiwe la Kifuniko. Ndipo Jengo limekamilika.

Zile siku zilizoahidiwa ambazo Bwana alizozinena na kuzitamani sasa zinatukia na zinatimizwa mbele yetu… NA NDANI YETU. Sasa tuko ndani ya Kristo Yesu, tukiwa tumeketi katika amani ya Kimbinguni, baraka za Kimbinguni, Roho wa Kimbinguni, ambapo kila kitu ni chetu. Tuko katika Nchi ya Ahadi nasi tunamiliki kabisa kila kitu.

Mbegu Yake ya kwanza iliyofikia kukomaa kikamilifu nayo ikatikiswa mbele ya Bibi-arusi Wake. Roho Mtakatifu alimrudishia Baba Mungu ripoti na kusema haya kumhusu malaika Wake mwenye nguvu:

Malaika Wako anakua katika neema! Yeye anabambua miti. Anawachukua hao kondoo na anaweza kuwachunga kama tu ufanyavyo Wewe. Yeye hatawapa kamwe miani. Hatawapa kamwe magugu magumu. Wanapomkaribia, wakisema, ‘Tunataka kujiunga na kanisa,’ anasema, ‘Nyamazeni, hamhitaji hilo! La, bwana. Haya ndiyo mnayohitaji, “Tubuni mkabatizwe, kila mmoja wenu, katika Jina la Yesu Kristo, mpate ondoleo la dhambi zenu. Mtapokea kipawa cha Roho Mtakatifu.”’

“Loo, yeye kweli anasema hivyo?”

“Naam, Bwana, kweli anasema Hivyo.”

“Naam, hivyo ndivyo nilivyoliandika hasa.”

“Hivyo ndivyo anavyolisema.”

“Unajua nini? Nilimwona Askofu Mkuu Fulani akimwambia kwamba ‘hangeweza kuja katika mji huu na kufanya mkutano.’ Bali, Unajua, nilimwongoza, nikasema, ‘Nenda hata hivyo.’ Walimwambia afadhali azirudishe kanda zake zote, nawe usiziache zitoke.’ Tulienda hata hivyo!”

“Huyo ni mwanangu mwenye mamlaka ambaye nimekuwa nikimsubiri. Sasa Mimi naweza kunena kupitia yeye na kuzifunua siri zangu zote zilizofichwa kwa kondoo Wangu.”

“Ajabu Baba Mungu.”

“Sasa ungependa nikupe ripoti ya watoto Wako wengine?”

“Ndiyo, wao wanaendeleaje?”

“Ee Baba…Ungewajivunia sana. Wao ni kipande kilichotolewa kwenye lile gogo la kale. Hao maaskofu wakuu wa kale bado wangali wanawaambia jambo lile lile, wasiende kwenye hayo makanisa ya kanda kuisikia Sauti Yako. Wao wanasema hizo kanda sio Sauti iliyo muhimu zaidi wanayopaswa kuisikia; ati kunazo sauti zaidi zilizo muhimu sasa hivi.”

“Hivi unajua Kondoo Wako wanawaambia nini hao wahubiri?”

“FUMBA MDOMO WAKO, SISI TUNADUMU NA KANDA, TUNADUMU NA SAUTI YA MUNGU.”

“Wao wanafanya hivyo kweli?”

“Naam, Bwana, wao ni kama tu Wewe.”

“Loo, ajabu vipi. Hilo linanifurahisha mno. Nimekuwa nikiwasubiri kwa muda mrefu sana. Sasa na wao wako tayari KUFANYWA WANA WENYE MAMLAKA!!”

“Watakuwa katika jukumu lao Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, (ni saa 2:00 Usiku ya Afrika mashariki–Mh) kuisikia Sauti Yako. Wao wataungana na kukusanyika kutoka kote ulimwenguni na kumwalika kila mtu kuungana nao.”

“Ajabu, NITAKUWA KULE PAMOJA NAO.”

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #2 60-0518

Maandiko:

Mwanzo 1:26
Waefeso Sura ya Kwanza
Warumi 8:19
Wagalatia 1:6-9
Waebrania Sura ya Sita
Yohana 1:17