Ujumbe: 65-0119 Mungu Aliye Mwingi Wa Rehema
.
Wapendwa Mawazo Ya Mungu,
Ninyi ni Neno la Mungu lililodhihirishwa lile lililoahidiwa kwa ajili ya siku hii. Daima mlikuwa. Si kwamba mtakuwa, bali ninyi sasa hivi ni wana na binti za Mungu;, kwa maana Mungu, aliye mwingi wa rehema, alikuwa na wewe katika mawazo Yake hapo mwanzo kabisa.
Kabla hata Yeye hajafanyika mwili hapa duniani; kabla hapajakuweko chochote, wewe ulikuwa mojawapo ya mawazo Yake. Yeye alijua jina lako lingekuwa lipi. Yeye alijua rangi ya nywele ambazo wewe ungekuwa nazo. Alijua kila kitu kukuhusu wewe.
Kisha, ulipoisikia Sauti Yake ikimulika mbele yako, kulikuwa na kitu fulani ndani yako kilichopaza tu sauti; unajua wapi unakotoka nawe ukakijia. Ulijua hiyo ilikuwa Kweli. Ulijua hiyo ilikuwa njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya leo hii kwa sababu Mbegu hiyo daima ilikuwa ndani yako.
Yeye sasa anatubeba juu ya mbawa za tai. Neno linatuambia Yeye huwafananisha manabii Wake na tai kila wakati. William Marrion Branham ndiye mjumbe tai wa Mungu aliyethibitishwa kwa ajili ya siku hii. Hizo ndizo mbawa za tai tunazopaswa kubebwa nazo hadi kwenye Nchi ya ahadi, kwa sababu yeye,; nabii tai wa Mungu, anaubeba ujumbe wa Mungu, akiita kutoka na kulinena Neno Lake, akimkamilisha Bibi-arusi Wake.
Sisi tunamfuata Mungu tunapomfuata William Marrion Branham mwenye ujumbe Wake wa ukombozi. Na Biblia inasema kwamba, “…Yeye, hawakuangamia pamoja na wale ambao hawakuamini.” Kwa maana, Mungu alikuwa mwingi wa rehema kwao;, kwa sababu walikuwa wakifuata amri Zake.
Mungu anatutaka tufuate amri Zake, nazo amri Zake zilisema:; Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu. Semeni TU kile kilicho kwenye hizo kanda. Sauti Yangu ndio Sauti pekee inenayo Maneno ya kutokukosea. Yamenenwa kikamilifu nanyi mnayapokea kikamilifu kutoka kwenye Sauti Yangu. Kwa hivyo, ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndiyo tu mnayohitaji, kwa kuwa Mimi, Mungu niliye mwingi wa rehema Zangu, nimeiandaa hiyo kwa ajili yenu. Ndiyo Njia Yangu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.
Mungu aliye mwingi wa rehema alikuchagua wewe na kukukusudia kimbele ili uwe na Ufunuo huo ili uisikie Sauti hiyo. Mungu aliye mwingi wa rehema alijua katika wakati huu wa mwisho, Wakati kungekuwa na mitazamo mingi potofu, sauti nyingi na fasiri tofauti za Ujumbe, kiasi kwamba tulihitaji Sauti iliyo Kamilifu, na Njia Kamilifu, ambayo tungeweza kwenda kwake ili tuweze kuisikia sisi wenyewe, Neno, kwa Neno, kwa Neno, kile hasa Yeye alichotaka kumwambia Bibi-arusi Wake.
Huwezi kupokea alichosema mtu mwingine. Inakupasa kupokea aliyosema Mungu. Yeye alisema, “Na neno la kila mtu na liwe uongo, na Langu kweli.”
Kwa hivyo, Mungu, aliye mwingi wa rehema Zake, ameiandaa njia ambayo Bibi-arusi Wake angeweza Kuisikia Sauti Yake masaa 24/siku 7 za wiki, siku 365 za mwaka, kwa Kubonyeza Play, na kuhuishwa kwa kuisikia Sauti ya Mungu ikinena mdomo kwa sikio na mioyo yao.
Sisi ni Neno Lake lililofanyika mwili. Hatuna nguvu yoyote, lakini Yeye ametupa mamlaka Yake. Kila mmoja wetu anayo. Ukiyakataa, utakaa mahali ulipo. Lakini tukiyakubali, yatafanya yapitayo ufahamu, kwa sababu Mungu ni mwingi wa rehema Zake.
Na wakati mwanamume au mwanamke, si hoja uko katika hali gani, unayo mamlaka kutoka kwa Mungu, kwa ahadi, kwa sababu Yeye ni tajiri na ametuahidi kutufanyia mengi mno. “Kama ukiuambia mlima huu ‘Ng’oka’ na usione shaka moyoni mwako, bali uamini kwamba hayo usemayo yametukia, yatakuwa yako.” Huna uweza wowote, bali unayo mamlaka.
Bibi-arusi anaweza tu kukamilishwa na kuunganishwa kwa kulisikia Neno Lake kamilifu lililoandaliwa kwa ajili ya leo hii:; Sauti Yake. Ndio Sauti pekee inayoweza kumuunganisha na kumkamilisha Bibi-arusi. Ndio Sauti pekee ambayo Mungu alituambia yatupasa kuisikia na KUIFUATA. Kama Musa, Ndugu Branham alijua kwamba yeye ndiye aliyechaguliwa kutuchukua sisi watoto kutuingiza kwenye Nchi ya ahadi kwa sababu hiyo ahadi alipewa yeye. Naye yampasa atupeleke kwenye Nchi ya ahadi.
Nabii tai wetu alitufundisha kwa mifano. Agano la Kale lilikuwa kivuli cha Agano Jipya. Alituambia jinsi gani tunavyopaswa kuwa waangalifu na kipi cha kuwa nacho macho katika wakati huu wa mwisho. Yeye alituonya kuhusu roho ya Kora, na kuhusu Dathani, na kundi lao la watu wasioamini, walipojaribu kuiga. Wao walijaribu kuingiza kitu fulani katika mpango wa Mungu.
Hawakutaka mpango wa mtu mmoja. Hawakutaka hayo. Iliwapasa wapate jambo la kutenda. Kora alisema, “Mbona, kuna watu watakatifu kuliko wewe, Musa. Unajifanya kama kwamba wewe tu ndiye pwani kwenye…au ndiwe pekee kijiwe katika pwani, hasa.” Akasema, “Mimi—Mimi…haukupaswa kufanya hivyo. Na kuna watu wengine hapa.”
Ndugu na dada, Mimi sijaribu kuyatenganisha makanisa kwa kuyasema na kuyanukuu mambo haya, Roho Mtakatifu ndiye anayetenganisha. Usikilizeni Ujumbe huu tunaoenda kuusikia, Nabii ndiye anayemwonya Bibi-arusi ni kipi cha kuwa nacho macho. Yeye anatuambia kile hiyo roho ilichofanya wakati huo, na kile itakachofanya tena katika siku yetu.
Kwa kweli, sijaribu kuwakusanya watu katika huduma tano, wao hawawezi kabisa kumuunganisha Bibi-arusi. Mimi ninajaribu kuwaunganisha kwenye Neno la Mungu lililo safi, lisiloghoshiwa, Sauti pekee inayoweza kumuunganisha Bibi-arusi.
Tunasikia mambo yayo hayo leo,, ati Ndugu Branham si mtu pekee anayeweza kuuhubiri Ujumbe, tumeitwa kuuhubiri Ujumbe. Kwa kweli wameitwa, bali kisha, wanashindwa kutambua umuhimu wa kuisikia Sauti hiyo na kuamini Ni Ujumbe wa mtu mmoja, kwa kutoa visingizio VYA KUTOICHEZA Sauti ya Mungu katika makanisa yao, na kuiweka huduma yao kuwa muhimu zaidi.
Nayo Biblia ilisema, “Walikwenda njia ya Balaamu, na kuangamia katika maasi ya Kora.” Kuangamia katika maasi! Je maasi ya Kora yalikuwa nini? “Je, unadhani wewe tu ndiye mtu aliye mtakatifu peke yako? Kwa nini, wa Mungu…Sisi sote tu watakatifu. Kanisa lote ndivyo lilivyo. Kila…Sote tukusanyike, ndivyo inavyotupasa kuwa.” Hivyo ndivyo walivyoangamia, katika hilo. Na tulistahili hayo kabisa. Tulistahili hayo.
Ujumbe huu, Sauti Yake, ndio Sauti pekee inenayo waziwazi na inapokelewa wazi na Bibi-arusi. Huduma aminifu ni kuwatia moyo watu wadumu na Sauti Hiyo kwa kuuhubiri na kuunukuu Ujumbe. Lakini si tu kuuhubiri, bali LAZIMA waucheze makanisani mwao, na kuwaambia watu wao Hiyo ndio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI, ili Bibi-arusi aweze kuisikia Sauti ya Mungu, kutoka kwa Mungu Mwenyewe.
Hakuna kilicho kikubwa zaidi kuliko kuisikia Sauti ya Mungu. Hakuna upako ulio mkuu zaidi kuliko upako ulio kwenye kanda. Hakuna njia nyingine ya kumuunganisha Bibi-arusi ila kwa Sauti ya Mungu ilio kwenye kanda. Hakuna NJIA nyingine KAMILIFU isipokuwa kwa KUBONYEZA PLAY NA KUAMINI KILA NENO UNALOSIKIA. Kweli ni Mungu, Aliye mwingi wa rehema Zake kwa Bibi-arusi Wake. Ndio njia Yake KAMILIFU iliyoandaliwa ya leo hii.
Ninawaalika mje na muungane chini ya ule upako mkuu zaidi wa siku yetu Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, [ni saa 1:00 JIONI ya Afrika mashariki–Mh] tunapomsikia Mungu akinena na kuwafundisha watoto Wake Neno kamilifu kwa kuuleta Ujumbe:; Mungu Aliye Mwingi Wa Rehema 65-0119
Ndugu Joseph Branham
Maandiko ya kusoma: Waefeso 2:1-5