22-0220 Muhuri Wa Nne

Ujume: 63-0321 Muhuri Wa Nne

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyechangamshwa,

Siku ya Ujumbe ilipowadia, tulikuwa sote mahali pamoja, kutoka duniani kote, kukaja ghafla toka Mbinguni uvumi kama uvumi wa upepo wa nguvu ukienda kasi. “ Habari za jioni wapendwa. Hebu na tusimame sasa kwa muda kidogo tu kwa maombi ”. Roho Mtakatifu akajaza nyumba zetu zote na makanisa tulimokuwa tumeketi, kwa uwepo wake.

Ndipo nguvu ya Ufunuo wa Neno ikaanza kutupa changamko la furaha, changamko la utoshelevu; changamko ya kwamba imethibitishwa, imehakikishwa, ya kwamba sisi ni Bibi-arusi Kipenzi na Mteule wa Yesu Kristo.

Tunazingojea kwa hamu kubwa hizo Ngurumo Saba zitoe sauti Zao kwetu, kwa maana tunajua sasa, bila kivuli cha shaka, ya kwamba sisi ndiyo kundi lile ambalo limechukua Neno la Mungu. Tutakata vipande vipande na kukata kwalo. Tunaweza kufunga mbingu, tunaweza kufunga hiki, ama kufanya vile, lo lote tunalotaka kufanya. Adui atauawa kwa Neno litokalo katika kinywa chetu, kwa maana ni kali kuliko upanga ukatao kuwili. Tunaweza hata kuagiza tani bilioni mia moja za inzi ikiwa tukizitaka. Lo lote TUTAKALOSEMA, Litatukia, kwa maana ni Neno la Mungu likitoka katika kinywa cha Mungu.

Tutakuwa na mamlaka makamilifu, juu ya dunia, kwa kuwa sisi ni mungu mdogo. Mungu ni Mungu wa ulimwengu wote, kila mahali, lakini tutakuwa na dunia chini ya udhibiti wetu wenyewe. Tunaweza kunena , tunaweza kutoa majina, tunaweza kusema, tunaweza kuzuia maumbile, tunaweza kufanya lolote tunalotaka; ni urithi wetu uliyorejeshwa.

Shetani anasema, “Lakini wana hatia!” Bali yeye Anapaza sauti na kusema, “HAWANA HATIA. Wameungama dhambi zao na kusimama mbele zangu wakiwa wamehesabiwa haki kabisa. Siwezi hata kulikumbuka tena. Wao ni mwanangu kabisa.”

Hilo si wazo letu, wala si neno letu, bali ni NENO LAKE, AHADI YAKE, kwa maana Mungu habadilishi kamwe mpango Wake au njia Yake ya kufanya mambo. Yeye daima anamtumia mwanadamu, Naye anatuambia sisi ni Bibi-arusi Wake aliyerejeshwa na kudhihirishwa kikamilifu ambaye amedumu na Neno Lake.

Hatujawa na kitu kingine ila Neno Lake la Asili. Hatujachezeana kimahaba, ama hata kutazama kitu kingine cho chote, bali tumedumu na Sauti ya Mungu, Neno lililofanyika Mwili, Nguzo ya Moto iliyothibitishwa, Mwana wa Adamu, Bwana Asema hivi. Sisi ni Bibi-arusi-Neno Bikira Wake.

Nena kuhusu changamko kwa Ufunuo. Kama vile dada yetu pale Kisimani, haikutulazimu kukaa usiku kucha wala kukaa hadi usiku uliofuata, tumeipata sasa hivi. Sisi ni uzao Wake. Nuru hiyo ilitujia na kitu fulani ndani kikabubujika kwa Maisha mapya. Sasa tuko njiani kuwaambia kila mtu, “Tumefaulu. Kushangaa kote kumekwisha, Mungu Mwenyewe anazungumza nasi kwa kila Ujumbe tunaosikia, akituambia: ‘Ninyi ndio wale nimekuwa nikiwangojea. Sasa nitawapeleka kwenye Fungate letu. Nimewaandalia Makao Mazuri Kila kitu jinsi tu mnavyopendelea . Tutaishi milele pamoja.”

Kwetu sisi, Kweli ya Neno la Mungu lililoahidiwa imethibitishwa na kufunuliwa. Yohana 14:12, Yoeli 2:28, Timotheo wa Pili 3, Malaki 4, Ufunuo 10. Sasa tumejazwa Mafuta nasi tumechangamshwa.

Je, ungependa kuwa na Changamko lili Hili? Unaweza, lakini kuna mahali pamoja tu pa kuipata. Kama vile Yesu alipokuwa kwenye arusi nao wakaishiwa na divai. Kwa kweli walikuwa wakinywa divai na ilikuwa ikiwapa changamko, lakini DIVAI BORA ilitoka kwa Yesu mwenyewe moja kwa moja.

Njoo unywe Divai Bora Zaidi na upokee Changamko kwa Ufunuo bora kabisa pamoja nasi Jumapili hii saa 6:00 Sita Mchana , saa za Jeffersonville, (Ni saa 2:00 Mbili Usiku ya Tanzania), tunaposikia: Muhuri wa Nne 63-0321 .

Uwe tayari kulewa kwa Divai ya Roho Mtakatifu.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma ili kujitayarisha kusikia mahubiri “ Muhuri wa Nne” 63-0321 .

Mathayo Mtakatifu Sura ya 4 yote

Luka Mtakatifu 24:49

Yohana Mtakatifu 6:63

Matendo 2:38

Ufunuo 2:18-23, 6:7-8, 10:1-7, 12:13, 13:1-14, 16:12-16, 19:15-17

Mwanzo 1:1

Zaburi 16:8-11

2 Samweli 6:14

Yeremia Sura ya 32 yote

Yoeli 2:28

Amosi 3:7

Malaki Sura ya 4 yote