UJUMBE: 60-0522M Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3
- 26-1108 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3
- 25-0518 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3
- 21-0704 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3
- 18-0701 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3 – Preliminari
- 16-0228M Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3
Wapendwa Waliofanywa Wana Wenye Mamlaka,
Serikali za dunia zinawaambia watu, “Jiandaeni, jiandaeni kwa ajili ya siku ya mwisho wa dunia. Wekeni akiba ya chakula na maji kwa ajili ya familia yenu ili muwe tayari kwa ajili ya kile kinachokuja.” Dunia iko katika hofu. Nini kitatokea? Kesho italeta nini?
Tunauona unabii ukitimia mbele ya macho yetu. Ulimwengu unaporomoka. Hofu na kutatarika vimeenea kote ulimwenguni, bila kujua kipi kinachokuja. Wakati ujao utakuwaje? Tunaweza kufanya nini? Je, huu ndio mwisho?
Wakati huo huo, Baba Mungu amekuwa akituonya na kutuandaa pia. Tayari amehifadhi chakula na maji yetu kwa ajili yetu, na tumekuwa tukila na kunywa kutoka kwenye kisima chetu cha maji. Tuko tayari, si kwa ajili ya siku ya mwisho wa dunia, bali kwa ajili ya Unyakuo!!
Bibi-arusi wa Kristo hajawahi kuwa mwenye furaha zaidi au kuridhika mno jinsi hii. Baba Mungu anamwambia Bibi-arusi wake mdogo ulimwenguni kote, “MSIOGOPE, furahini. Ninyi ndio wateule wangu. Ninawaandaa kwa ajili ya Unyakuo, Siku yenu ya Harusi. Ninawatoa katika machafuko haya. Ninyi ni Wana na Binti Zangu Wenye mamlaka. Ule utimilifu wa wakati unakuja.”
Tunayo yubile ya jinsi gani. Kila Neno tunalolisikia ni kibamba cha dhahabu kwetu sisi. Tunalipokea tu na kuendelea kuling’arisha na kuling’arisha tena na tena. Kisha tunasema:
“Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana.” “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana.” “Mtakatifu, mtakatifu, mtakatifu, kwa Bwana.”
Sisi tumeyaelekeza macho yetu Kalvari, na hakuna kitakachotuzuia! Tunatembea katika Barabara Kuu ya Mfalme, tukiwa tumepakwa na Mafuta ya thamani, tukiingia Patakatifu pa Patakatifu.
Wakati adui anapojaribu kutuambia tumepotea na sisi si Bibi-arusi Wake, sisi tunabonyeza Play tu Naye anatupazia sauti na kusema:
Sahauni kabisa kwamba mtapotea na mtafanya hivi, na mnaogopa hili.” Msiogope kitu, kwa kuwa anajaribu kuwaambieni mlipo, mu nani, jinsi mnavyosimama.
Ulimwengu uko katika HOFU, na wakati huo huo Baba Mungu anatuambia, “Msiogope CHOCHOTE, Mimi nawaambieni ninyi ni nani na wapi mnakoenda.” …UTUKUFU!!
Katika udhaifu wetu wa kibinadamu tunashindwa kila siku. Tunafanya makosa mengi sana. Tunafanya mambo mengi ambayo hatupaswi kufanya. Kisha shetani anatutwanga na kututwanga, akisema tunawezaje sisi kuwa Bibi-arusi.
Bali tumekuwa imara. Tunajua haswa kipi cha kufanya: Kubonyeza Play ili kusikia kile Baba Mungu asemacho.
Sasa, waweza ukatenda mambo makosa, na kila unapofanya mambo vibaya utayajutia. Naam, bwana, utavuna unachopanda! Bali hilo halina uhusiano wo wote na wokovu wako. Unapozaliwa na Roho wa Mungu, una Uzima wa Milele na huwezi kufa kamwe kama vile Mungu asivyoweza kufa. Wewe ni sehemu ya Mungu, wewe ni mwana wa Mungu.
Ilimpendeza Mungu kutuchagua tangu zamani. Ilimpendeza Mungu kutufanya Wana na Binti. Ilimpendeza Mungu Kutufanya kuwa Wana. Ilimpendeza Mungu kutupa sisi Ufunuo wa kweli wa Yeye ni nani na sisi ni nani. Ilimpendeza Mungu kumpeleka malaika Wake ng’ambo ya pazia la wakati na kumwonyesha yeye SISI upande wa pili ili tuweze kufurahi na tusiwe na HOFU.
Kwa bahati mbaya, kanda hizi si za kila mtu. Ni za kanisa la nabii tu…Utukufu, hao ni sisi. Kila dakika tuwezayo, na kila wakati tunapokusanyika pamoja, kile sisi tunachotaka kufanya tu ni Kubonyeza Play ili kuisikia Sauti ya Mungu.
Wengine wanalipata vizuri. Wao hawalioni tu kama sisi. Wanaliona vivyo hivyo, bali kwetu sisi… Ni vizuri sana kulitazama; kwa maana tunajua ndio njia iliyoandaliwa na Baba Mungu kwa ajili ya siku hii.
Kila siku ulimwengu na watu wake wanazidi kujawa na msongo wa mawazo. Kila kitu kinaonekana cheusi na giza zaidi. Bali kwa Bibi-arusi, kila siku inaleta changamko zaidi kwa Ufunuo. Tumepumzika, tumejazwa na Roho Wake Mtakatifu, tumeketi pamoja katika mahali pa kimbinguni.
Je, umewahi kujiuliza ilikuwaje siku ile ya Pentekoste wakati ulipokuja ule upepo wenye nguvu ukienda kasi naye Roho Mtakatifu akakijaza kile chumba, na kila mmoja mle?
Usifikiri tena. Njoo uungane nasi Jumapili saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 2:00 USIKU ya Afrika mashariki–Mh) anapowakusanya pamoja tai Wake, akikiijaza chumba chako kwa Roho Wake Mtakatifu, na kutuandaa kwa ajili ya Kuja Kwake hivi karibuni kwa kutulisha chakula Chake kilichohifadhiwa. Mtakula na kunywa kutoka kwenye ghala Lake, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #3 60-0522M
Maandiko:
Mathayo 28:19
Yohana 17:7-19
Matendo 9:1-6, Sura ya 18 na 19
Warumi 8:14-19
1 Wakorintho 12:12-13
Wagalatia 1:8-18
Waefeso Sura ya 1
Waebrania 6:4-6, 9:11-12