UJUMBE: 65-0220 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia
- 26-0315 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia
- 24-0616 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia
- 22-1120 Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia
Mpendwa Bi. Yesu Kristo,
Hii ndiyo siku yenyewe. Huu ndio wakati wenyewe. Mungu alimtuma tai Wake mwenye nguvu duniani kumwita Bi. Yesu Kristo Wake atoke, kunena na kumwambia, “Wewe NDIYE niliyemchagua. Wewe NDIYE ninayempenda. Wewe ndiye Bibi-arusi Neno bikira Wangu Mkamilifu. Sisi ni MMOJA.”
Kuyasikia maneno hayo tu, mioyo yetu inaruka kwa furaha. Kuwazia, katika ulimwengu wote, pamoja na mamilioni na mamilioni yake ya watu, kuna Bi. Yesu Kristo MMOJA tu, na WEWE ndiye Huyo, YULE anayemjia.
Kuna mahali PAMOJA tu palipochaguliwa pa kuabudia. Kuna Ujumbe MMOJA tu mkamilifu uliochaguliwa. Kuna BIBI-ARUSI MMOJA tu MKAMILIFU aliyechaguliwa…NASI NDIO!!
Baba ana mahali PAMOJA peke yake alipopachagua pa kuabudia, Bwana Yesu Kristo; Yeye ni Neno. Leo, kuna mahali PAMOJA peke yake ambapo mauti ya kiroho haiwezi kupiga: Neno. Mauti haiwezi kulipiga Neno, kwa sababu ni Neno la Mungu lililo Hai.
Ufunuo kamili wa Neno hilo lililo Hai umefunuliwa kwa Bi. Yesu Kristo peke yake. Kuna mahali PAMOJA tu palipochaguliwa ambapo Bi. Yesu Kristo anaweza kwenda na kulisikia NENO KAMILIFU LIKINENWA. Kuna nabii MMOJA tu aliyechaguliwa kuwa Sauti ya Mungu. Kuna mahali PAMOJA tu ambapo Bi. Yesu anapoweza kwenda na kuisikia, BWANA ASEMA HIVI: KUBONYEZA PLAY.
Kutakuweko Nuru mnamo wakati wa jioni, mahali pekee alipopachagua Mungu pa kuabudia. Loo, Ujumbe huu umefika wapi, Yeye atafanya nini? Na katika siku yake itakuweko Nuru wakati wa jioni, na (nini?) kuwakaribisha watoto Wake wanaporudi nyumbani kwenye Nchi ya kweli ya ahadi, kwa ishara ile ile ya Nguzo ya Moto ambayo iliwaongoza wana wa Israeli kupitia nyikani.
Jinsi gani Bibi-arusi Wake anavyopaswa kuwa mwangalifu kuifuata na kuisikia Sauti ya Mumewe ikizungumza Naye. Kuna mahali PAMOJA tu tunapoweza kwenda na kuwa na hakika 100%. Kuna Sauti MOJA tu tuliyoiwekea kikomo chetu cha Milele.
Bi. Yesu Kristo anaamini kwamba Maneno anayoyasikia kwenye kanda ni Maneno ya Mumewe. Yeye anaamini Neno Lake halihitaji fasiri yoyote. Kwa hivyo, Yeye anaamini kuna mahali PAMOJA tu palipoandaliwa ambapo Yeye anapoweza kwenda na kusema AMINA kwa kila Neno, Sauti ya Mumewe iliyo kwenye kanda.
Kwa mara nyingine tena, Bi. Yesu Kristo, kutoka kote ulimwenguni, anaweza kusema, “Leo, Neno hili lililonenwa, linatimizwa”.
Mungu Mpenzi, huko chini kuvuka majangwa kule Tucson, huko mbali California, juu huko Nevada na Idaho, kwenda hadi Mashariki na kila mahali, chini huko Texas; wakati mwaliko huu unatolewa, watu wamekiketi katika—katika makanisa madogo, vituo vya mafuta, majumbani, wakisikiliza.
Umealikwa kuja kusikiliza pamoja na Maskani ya Branham saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapomsikia Mungu akizungumza na Bibi-arusi Wake mteule, Ujumbe: “Mahali Alipopachagua Mungu Pa Kuabudia” 65-0220.
Ndugu Joseph Branham
Maandiko: Kumbukumbu la Torati 16:1 hadi 3.