UJUMBE: 65-0217 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana
- 26-0222 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana
- 24-0526 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana
- 22-1030 Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana
Wapendwa Wana-kondoo,
Ni heshima na majaliwa yaliyoje kusema, “Sisi ni wana-kondoo wa Mungu, ambao Yeye alimtuma malaika-mjumbe Wake wa saba kuwaita na kuwalisha Mana Yake iliyohifadhiwa na iliyofichwa.”
Tumeridhika na tunaamini Ujumbe huu ni Sauti ya Mungu ambayo imetumwa kumkamilisha Bibi-arusi Wake. Tunaamini kapi linajiondoa kwenye ngano, na sasa Bibi-arusi Wake amekaa katika Uwepo wa Mwana, AKIBONYEZA PLAY apate kuiva.
Na hilo ndilo kusudi letu la kuwa hapa, rafiki, kukaa katika Uwepo wa Mwana hata kundi letu dogo la watu hapa, hata litakapoiva sana kwa ajili ya Kristo, liwe mkate kwenye meza Yake. Hivyo ndivyo ninalitaka lifanye.
Yeyote ambaye haamini kwamba KUBONYEZA PLAY na kuisikia Sauti ya Mungu iliyothibitishwa ikinena ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi unayopaswa kuisikia, ni mtu anayejiepusha na uso wa Bwana.
Hamna budi kulikabili, ama kufanya jambo fulani juu yake.Una jukumu, kila mtu analo, nawe huna budi kukabiliana na mambo haya.
Jinsi gani nukuu hii ilivyo ya kweli na muhimu kwa ajili ya siku hii. Kuna mgawanyiko mwingi miongoni mwa walioitwa watoke wa Mungu. Je, ni muhimu zaidi kuzicheza kanda kanisani ili kuisikia Sauti ya Mungu, au hivi sasa ni muhimu zaidi wahudumu kulihudumu Neno?
Mungu amewaita na kuwaweka wahudumu hapa ili kulidumisha Neno mbele ya watu. Wao ni Wachungaji. Neno linafundisha hili. Wanapaswa kuheshimiwa na kutambuliwa kama watu ambao Mungu amewaita na kuwaweka.
Hatuwezi, na hatupaswi, kusema kamwe wao si Bibi-arusi. Hilo ni KOSA na si kulingana na kile nabii alichotufundisha. Nimesikia watu wakisema: “Kama hawachezi kanda makanisani mwao, wao ni wapinga Neno.” Haupaswi kamwe kusema kitu kama hicho. Hilo linanionyesha una roho asiye sahihi.
Nimesikia wengine wakisema, “Wote lazima wasikilize hewani pamoja na BT la sivyo wako nje ya mapenzi ya Mungu”. Haupaswi kamwe kusema kitu kama hicho. Mungu peke yake ndiye anayejua ni nani aliye Bibi-arusi na ni nani asiye. Hiyo si roho ya Bibi-arusi kusema kitu kama hicho.
Hata baadhi ya watu wanaosikiliza hewani pamoja na BT wanasema, “ukienda kanisani kusikiliza kanda na usisikilize hewani nyumbani mwako umekosea!” Hilo si sahihi ndugu na dada. Kama unasema hivyo, ACHA, umekosea. Kila mmoja lazima wafanye vile WANAVYOJISIKIA WANAONGOZWA NA BWANA KUFANYA.
Wahudumu wengi wanahisi kuhubiri ndio njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya siku hii. Sisi tunaona tu mambo tofauti, hiyo ni sawa. Ni mara ngapi Ndugu Branham alifanya ulinganisho huu uleule? Tumetoka kumsikia kwenye Maswali na Majibu, watu walipokuwa wakizungumza kuhusu Ndugu Jackson kuwa amekosea, aliwakemea kusema lolote dhidi yake na kanisa lake.
Mimi ndo nahubiri hivyo kwa njia ya barua hii kile Mimi ninachoamini ndio njia iliyoandaliwa na Mungu kwa ajili ya Maskani ya Branham. Wao ni ndugu na dada zetu. Wanampenda Bwana na Ujumbe huu. Hivyo ndivyo wanavyohisi Bwana anawaongoza. Bwana asifiwe.
Wao wanaliona kwa njia moja na sisi tunaliona kwa njia nyingine, hilo ni sawa. Mimi siwezi kuliona kwa njia yao nao hawawezi kuona yangu. Nionavyo mimi, kuna njia nyingi ambazo Mungu ameandaa, lakini kuna NJIA MOJA TU KAMILIFU, NA KWANGU MIMI, HIYO NI KUBONYEZA PLAY.
Natumai sieleweki vibaya hapa. Kuweka mikono na kuwaombea watu ni 100% kulingana na Neno. Kupakwa mafuta na kuwaombea wagonjwa ni Neno la Mungu kulingana na Maandiko. Ndugu Branham alituhubiria na kutufundisha yote kuwa ni Neno. Lakini Mimi naitaka NJIA KAMILIFU YA MUNGU ALIYOIANDAA….KUAMINI TU KWA SABABU MUNGU ALISEMA HIVYO. Hilo ndilo ninalojitahidi kufanya.
Lakini sasa kwa ajili ya uponyaji, ni rehema ya Mungu tu kwamba Yeye, “Kwa kupigwa Kwake wewe uliponywa.” Sasa, kwanza Neno linasema hivyo, linapaswa kutosha, lakini ikiwa huliamini katika Neno, basi kuna karama Kanisani, kama vile wanaume waliovuviwa kujua jinsi ya kufundisha hilo, hilo litalifanya liwe wazi kwako, ndilo, na imani ya kuamini.
Ninaamini katika huduma 5. Ninaamini katika watu walioitwa na Mungu kuhubiri na kulifundisha Neno. Lakini, naamini kuisikia Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio NJIA KAMILIFU YA Mungu KWANGU MIMI.
Katika kuzisikiliza kanda, sihitaji hata kuelewa, NAAMINI TU KILA NENO NINALOSIKIA. Hakuna mtu, hakuna mhudumu, hakuna mahali pengine ninapoweza kwenda ambapo ninaamini KILA NENO na kukiweka kikomo changu cha Milele, isipokuwa kanda.
Haijawahi kutokea tangu mwanzo wa wakati Mungu kuwapa watu Wake fursa na uwezo wa kuisikia Sauti Yake wao wenyewe ikizungumza mdomo kwa sikio. Kila siri inafunuliwa kwenye kanda. Kila swali linajibiwa kwenye kanda. Kila kitu Bibi-arusi anachokihitaji ili kukamilishwa kiko kwenye kanda.
Kila Neno lililonenwa kwenye kanda ni Neno la Mungu. Huenda nisielewe ama nisiweze kuelezea kila kitu, lakini si lazima nifanye hivyo. Yeye ananitaka tu niseme AMINA KWA KILA NENO, nazo KANDA ndio mahali PEKEE ninapoweza kufanya hivyo.
Bali inapo—inapokulazimu kufanya jambo ambalo ni tofauti, wakati inapokulazimu kutetea unayoamini kuwa ni Kweli, hiyo ndiyo sehemu iliyo ngumu, hapo ndipo mkwaruzo unapokuja, papo hapo.
Ninaamini kwa yote yaliyo ndani yangu, tuko katika Mapenzi makamilifu ya Mungu na katika meli inayoelekea Ninawi. Ningependa ulimwengu wote uje usafiri pamoja nasi katika meli yetu Jumapili hii saa 6:00 MCHANA,. Masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) tunapomsikia Mungu akizungumza na Wana-kondoo Wake.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 65-0217 “Mtu Anayejiepusha Na Uso Wa Bwana”
Maandiko ya kusoma:
Yona 1:1-3
Malaki 4
Yohana Mtakatifu 14:12
Luka 17:30