UJUMBE: 63-0317M Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 25-0302 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 23-0709 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 22-0116 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 21-0110 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 19-0317 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo
- 17-0318 Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo – Preliminari
Wapendwa Mayungiyungi Ya Kidimbwi,
Mnamo tarehe 28, mwezi Februari, 1963, Ilinguruma. Whiu-whiiiu, Malaika Saba walikuja kutoka umilele nao wakamtokea Malaika-mjumbe wa Saba wa Mungu. Alinyakuliwa katika piramidi ya lile kundi. Kisha, wingu la kimbinguni likatokea angani juu ya Arizona. Ilikuwa ni ishara, Mungu alikuwa akimtuma malaika Wake wa saba arudi Jeffersonville ili kuifungua ile Mihuri Saba.
Tarehe 28 mwezi Februari, 2025, sayari saba zajipanga mstari angani. Bibi-arusi anajiweka mwenyewe tayari kukusanyika na kuisikia ile Mihuri Saba.
Unaalikwa, na Bwana Mwenyewe, kukusanyika pamoja na Bibi-arusi kutoka ulimwenguni kote, kuisikia Sauti ya Mungu ikifunua Ufunuo wa ile Mihuri Saba.
Ile siku ambayo manabii na wenye hekima waliitamani na kuingojea tangu mwanzo wa wakati, inatukia. Yule malaika mwenye nguvu ambaye Mungu alisema angemtuma duniani katika siku za mwisho amekuja kufungua na kuzifunua siri za Mungu zilizofichwa, ili Bwana wetu Yesu aweze kurudi kwa ajili ya Bibi-arusi Wake mwaminifu na kutupeleka kwenye Karamu yetu ya Arusi.
Wajibu wangu wa kwanza, nilipokuwa ninakuja kwenye kanisa hili jipya, niliwaunganisha katika ndoa kijana mwanamume na mwanamke wakiwa wamesimama ofisini. Na iwe ni mfano, ya kwamba nitakuwa mhudumu mwaminifu kwa Kristo, kumtayarishia Bibi-arusi kwa ajili ya sherehe ya Siku hiyo.
Leo hii, Neno hili limetimia. Mungu ananena kupitia malaika Wake, akimtayarisha Bibi-arusi Wake kwa ajili ya sherehe ya Siku hiyo. Tunafuata maagizo yake vilivyo kabisa. Bibi-arusi amejiweka mwenyewe tayari kwa KUDUMU NA SAUTI YA MUNGU ILIYO KWENYE KANDA.
Tumesikia kitu gani kwa ndoto na maono? Kile Chakula, HIKI HAPA, mahali penyewe ni hapa. Sauti ikamwambia, “Lete Chakula. Kihifadhi mle ndani. Hiyo ndiyo njia pekee ya kuwaweka hapa, ni kuwapa Chakula.”
Wengi wanaamini kwamba yeye anamaanisha tu, “dumuni tu na Neno,” na hiyo NI KWELI, anasema hivyo; lakini Bibi-arusi pia atasoma katikati ya mistari wakati Bwana-arusi anazungumza na Bibi-arusi Wake.
Hata yale maono ambayo Mungu anayaonyesha hapa mahali hapa, yanafahamika vibaya sana. Hiyo ndiyo sababu mnanisikia mimi kwenye kanda, nikisema, “Sema vile kanda zinavyosema. Sema vile maono yanavyosema.” Sasa, kama mko macho kabisa, mtaona kitu fulani. Mnaona? Natumaini si lazima nikishike mkononi mwangu na kuwaonyesheni.”
Hata maono yalieleweka vibaya, hata baada ya yeye kuwapa fasiri. Hilo ndilo yeye alilokuwa akituambia, ikiwa hutaki kupata mkanganyiko, au kuelewa vibaya, Bonyeza Play na usikie kile hasa Sauti ya Mungu inachosema.
Najua Neno lina maana zaidi ya moja, lakini hii ndiyo fasiri yangu: Ndoto na maono yote yalisema kitu kile kile; dumuni na kanda. Kama una swali, nenda kwenye kanda. Kanda hizo ni Chakula cha Mungu kilichohifadhiwa. Sema tu kile kilicho kwenye kanda; usiongeze chochote Kwake. Kanda hizo ni Bwana Asema Hivi kwa Bibi-arusi. Neno humjia nabii, peke yake. Nabii ndiye mfasiri PEKEE wa Kiungu wa Neno. Nabii alikuwa ndiye wa kumwita Bibi-arusi atoke na kumwongoza. Nitahukumiwa kwa kile kilichonenwa kwenye KANDA.
Kila kitu kinanielekeza kwenye KANDA.
Wapendwa wangu Mayungiyungi ya Kidimbwi, kwangu mimi, KUBONYEZA PLAY NDIO MUNGU KWA URAHISI KWA AJILI YA LEO HII.
Kila wiki napata changamko sana; ni kitu gani kinachoenda kufunuliwa leo wakati Bibi-arusi Wake atakapokusanyika ili kuusikia Ujumbe? Ninajua Roho Mtakatifu atakuwa akimtia mafuta kila mmoja wetu anapolifunua Neno Lake kuliko hapo awali. Ninahisi, wakati wowote tu, Yeye atakuja na kututwaa kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi.
Sisi ni, wana na binti za Mungu. Sisi ni, uzao uliotoka kwa Mungu. Sisi ni, urithi wa dunia. Tutatawala maumbile. Tutanena na iwe. Sisi ni Bibi-arusi!
Hebu na tujiweke wakfu upya kwa ajili ya kazi, na tujiweke wakfu kwa Kristo.”
Ndugu. Joseph Branham
Tarehe: 2 Machi, 2025
Ujumbe: Mungu Akijificha Kwa Urahisi, Halafu Akijifunua Kwa Jinsi Hiyo 63-0317M
Muda: saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville.(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki)