24-0609 Leo Maandiko Haya Yametimia

UJUMBE: 65-0219 Leo Maandiko Haya Yametimia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Uzao Maalum wa Kiroho wa Kifalme,

Hakuna kusubiri tena, hakuna kushangaa tena, TUMEFIKA! Sisi NDIYE yule Bibi-arusi Uzao maalum wa Kiroho wa Kifalme. Uzao wa Kiroho kwa Mwana yule wa Kifalme aliyeahidiwa. Sio kundi fulani katika siku zijazo; si kizazi kijacho; tunaishi katika siku ya mwisho, sisi ndio kizazi kile kitakachomwona Yesu Kristo akirudi duniani.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Injili ile ile, Nguvu zile zile, Mwana wa Adamu YULE YULE aliyekuwako jana, yupo leo, na atakuwako milele.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Marafiki wapendwa huko Arizona, California, Texas, kote nchini Amerika Na ULIMWENGUNI KOTE mnaosikiliza kanda hii hewani kwenye muunganiko wa simu; M-w-a-n-a wa Mungu yule yule aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili, ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu katika kizio cha magharibi cha dunia hapa, ambaye anayejitambulisha Mwenyewe kati ya kanisa usiku huu, yeye yule jana, leo, na hata milele. Ile Nuru ya jioni ya Mwana imekuja.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Sauti ya Masihi, aliyekuwa akisimama na kunena jukwaani katika siku Yake, akijitambulisha Mwenyewe na Neno la ahadi la wakati huo, ndio Sauti ile ile ya Masihi, inayonena na Bibi-arusi Wake leo ulimwenguni kote kwenye kanda, ikituambia: Mimi ni yeye yule jana, leo na hata milele. MIMI NI Sauti ya Mungu Kwenu. WEWE NI BIBI-ARUSI WANGU UZAO WA KIROHO WA KIFALME ambaye amekaa na Neno Langu.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Kuna msukosuko mwingi kati ya watu siku hizi hata wanashindwa kuiona Kweli ya Mungu. Ni kwa sababu kuna mafafanuzi mengi sana ya Neno la Mungu yaliyotengenezwa na wanadamu. Mungu hahitaji mtu yeyote afafanue Neno Lake. Yeye Mwenyewe ndiye mfafanuzi. Alimtumia Bibi-arusi Wake nabii-malaika wa siku za Sauti wa Ufunuo 10:7 kulifafanua Neno Lake. Ni BWANA ASEMA HIVI.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Unasema, “kama ningalikuwa wakati ule Yesu alipokuwa duniani, ningalifanya hivi na hivi.” Vema, hicho hakikuwa kizazi chako. Lakini, hiki ndicho kizazi chako, huu ndio wakati wako. Ni Sauti gani unayosema ndio Sauti ya Mungu? Ni Sauti gani ndio iliyo muhimu sana kwako?

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Ibilisi anaenda huku na huko kuliko hapo nyuma kumshambulia Bibi-arusi Wake. Anaweza kukufanya ufikiri kuwa una maradhi au aina fulani ya ugonjwa, au kuishambulia familia yako. Wakati mwingine Mungu huruhusu mambo kuwa meusi sana hata huwezi kuona juu, kando—kando, au penginepo pote, na ndipo Yeye huja kutengeneza njia kupitia kwayo, ili uweze kusema,
“Mimi si uzao wa Hajiri, mimi si uzao wa Sara, mimi hata si uzao wa Mariamu, mimi ni Uzao wa Kiroho wa Mungu wa Kifalme wa Ibrahimu. Ninalichukua Neno la Mungu lililoahidiwa kwa ajili yangu, Ni Bwana Asema hivi. sitatikiswa. Haidhuru inaonekanaje, shetani anasema nini. Chochote ninachohitaji, nitamchukua Mungu katika Neno Lake.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Sauti ya Mungu imesema. Nimekihifadhi Chakula chote cha Kiroho mnachohitaji. Semeni TU yale yaliyo kwenye kanda hizo. Mimi ni Sauti ya Mungu kwenu. Neno Langu halihitaji fasiri. Msibishane au kupigana, pendaneni, BALI kaeni na NENO LANGU.

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Usijikunyate. Usiwe na huzuni. Usimruhusu Shetani akunyang’anye FURAHA yako. Kumbuka wewe NI NANI, kule uendako, itakuwaje kwenye Karamu hiyo kuu ya Arusi. Kuishi katika mji huo mzuri aliyokujengea wewe tu. Ambamo utakuwa Milele yote pamoja Naye na wale wote waliyotangulia.

Hakuna ugonjwa tena. Hakuna huzuni tena. Hakuna kifo tena. Hakuna vita tena. Uzima wa Milele tu pamoja Naye. Ndipo tutasema:

Leo, Maandiko haya Yametimia!

Hebu tusiwe na huzuni na kusema, “Nimechoswa sana na mahali hapa, nataka kutoka hapa. Hebu na tuliseme namna hii: Anakuja dakika yoyote sasa, KWA AJILI YANGU…UTUKUFU! Siwezi kusubiri. Nitawaona wapendwa wangu wote. Watatokea mbele yangu, ndipo nitajua, IMEKWISHA, TUMEFIKA.

Kisha, chini ya dakika moja ya kufumba na kufumbua, sote tutakuwa pamoja ng’ambo ya pili.

Hebu tufurahi na tupige shangwe, kwa kuwa ile arusi ya Mwana-Kondoo i karibu, na Bibi-arusi Wake… Bibi-arusi Wake amejifanya tayari!

Kama ungependa kupiga shangwe, na kuwa kwenye Arusi ya Mwana-Kondoo pamoja nasi, njoo ujiweke tayari Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia:

Leo, Maandiko Haya Yametimia 65-0219

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma:

Yohana Mt Sura ya 16
Isaya 61:1-2
Luka Mt 4:16