26-0308 Leo Maandiko Haya Yametimia

UJUMBE: 65-0219 Leo Maandiko Haya Yametimia

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Uzao Mkuu Wa Kifalme,

Ule wakati ambao tumekuwa tukiusubiri kwa hamu na kuutamani umewadia. Tumewasili. Tunauona ukijifunua mbele ya macho yetu. Kila siku unabii unatimia, nasi tunaweza kusema: LEO MAANDIKO HAYA YAMETIMIA MBELE YA MACHO YETU.

Ni changamko la Ufunuo lililoje linalotukia kwa Bibi-arusi. Kwa kila Ujumbe tunaousikia, tunahisi ndani ya mioyo na roho zetu, ” Linawezaje kuwa kubwa zaidi ya hapa na la ajabu zaidi kuliko hivi, Bwana?” Ndipo Yeye anakuja miongoni mwetu kwa mara nyingine tena na kututia mafuta tunapoisikia Sauti Yake ikituita na kusema, “Wewe ni Kipenzi Changu. Nilikuchagua wewe uwe Bibi-arusi Wangu. Kama vile nilivyokuahidi, ninakuja kukuchukua. Niko njiani. Hivi karibuni Tutakuwa pamoja milele.”

Tunapaza sauti kutoka kote ulimwenguni, tukivumisha Mbingu kwa haleluya zetu, utukufu, sifa, na kuabudu kwetu Kwake. Shetani ameshindwa. Baba ameyaondolea mbali mashaka yetu yote, kutokuwa na uhakika kwetu kote, kudhania kote. Tunaweza kutangaza kwa mioyo na roho zetu zote, SISI NDIO ule Uzao Mkuu wa Kifalme wa Ibrahimu. Bibi-arusi wa Kifalme kwa Mwana yule wa Kifalme aliyeahidiwa.

Uwepo wa Bwana umekuwa wa ajabu mno kwa anavyotufunulia Neno Lake kuliko hapo awali. Yeye amemuunganisha Bibi-arusi Wake pamoja na Neno Lake, na kutuweka katika Nia moja kwa umoja kama jamii moja, tukiisikiliza Sauti ya Mungu ikinena na kutukamilisha kwa Neno Lake.

Kila Ujumbe tunaousikia ni kama vile kisima kinachofoka maji kinachofurika ndani ya nafsi zetu; kikitiririka, kikisukuma, na kububujika kutoka kwenye Kiti cha Enzi cha Mungu. Tunakunywa, kunywa na kunywa, yakiziburudisha nafsi zetu.

Ndugu na Dada zangu, sisi ndio utimilifu wa Maandiko yanayosema Yeye atakuwa na Bibi-arusi Neno bikira. Sisi ndio: Leo Maandiko haya yametimia.

Mungu Mwenyewe alinena kutoka Mbinguni na malaika Wake wa saba na kusema, “Kama vile Yohana Mbatizaji alivyotumwa kutangulia Kuja kwa kwanza kwa Kristo, Ujumbe wako utatangulia Kuja Kwake kwa pili, duniani kote.” Bibi-arusi anaweza kusema: Leo Maandiko haya yametimia.

Je, hivi tunaweza kuelewa kwamba Sauti ya Mungu halisi imenena katika siku yetu kupitia midomo ya mwanadamu, ikarekodiwa, ikahifadhiwa, na kutunzwa ili Yeye aweze kunena na kila mmoja wetu, Bwana Asema Hivi? Yeye ameliwezesha hilo ili tusichukue neno la mtu yeyote, mawazo ya mtu yeyote, fikra za mtu yeyote, ni sisi kuketi tu na kuisikiliza Sauti Yake ikinena nasi moja kwa moja Neno Lake Safi.

NI KITU GANI KINACHOTENDEKA LEO?

Na M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili, ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyeko katika kizio cha magharibi cha dunia, ambaye anajitambulisha Mwenyewe kati ya kanisa usiku huu, Yeye yule jana, leo, na hata milele. Ile Nuru ya jioni ya Mwana imekuja. Leo Maandiko haya yametimia mbele yetu.

JE! TUKO KATIKA MAPENZI MAKAMILIFU YA MUNGU KWA SISI KUSEMA NA KUAMINI KUWA: “KUZICHEZA KANDA NDIO NJIA ILIYOANDALIWA NA MUNGU KWA AJILI YA BIBI-ARUSI WAKE”?

JE! KUNA KITU KILICHO KIKUU ZAIDI YA KUZISIKILIZA KANDA?

Kila mara katika utatu kama nilivyosema usiku uliopita Mungu huwakilishwa. Pale kulikuwako Wasodoma. Walutu, na Waibrahimu. Ni hali ile ile usiku huu, ulimwengu ukikaa tu hivyo!
Tazama, Yule aliyekaa pamoja na Ibrahimu alikuwa Mungu Mwenyewe; na wale wengine wawili walikuwa Malaika wajumbe.

KWA HIVYO NI NANI ANAYEZUNGUMZA NASI KWENYE KANDA?

Hebu niwaulizeni kitu fulani. Tazama utaratibu huu sasa. Ibrahimu alimwita huyu aliyeongea naye, “Elohim.” Neno la Kiebrania Elohim maana yake ni “Yule aridhishaye kwa vyote. Yeye yule Aliye wa Milele,” Elohim, Mungu Mwenyewe!

NI MUHIMU JINSI GANI KUBONYEZA PLAY?

…“wakati mmoja Roho Mtakatifu atakuja na kufanya mambo yale yale, na kunena tu neno moja dhidi Yake hautasamehewa kamwe. Hiyo ni siku hizi, ambapo kila neno yapasa liunganike pamoja. Nena neno dhidi Yake, halitasamehewa katika dunia hii wala dunia ijayo.”

Haleluya zetu za wiki iliyopita na kumsifu Bwana zilikuwa ni maandalizi tu ya kutuandaa kwa ajili ya kile kitakachotendeka Jumapili hii, Kwani Bibi-arusi kwa mara nyingine tena anaungana na kumsikiliza MUNGU akitutia moyo na kutuhakikishia kwamba sisi ndiyo wateule Wake, Naye anakuja hivi karibuni kutupeleka kwenda kwenye Karamu yetu kuu ya Harusi, kisha Makao yetu ya Baadaye.

Siku hii ndiyo aliyoifanya BWANA; tutashangilia na kuifurahia.

Ndugu Joseph Branham

Ujumbe: 65-0219 – “Leo Maandiko Haya Yametimia”

Maandiko:
Yohana Sura ya 16
Isaya 61:1-2
Luka 4:16