25-0615 Muungano Usioonekana Wa Bibi-Arusi Wa Kristo

UJUMBE: 65-1125 Muungano Usioonekana Wa Bibi-Arusi Wa Kristo

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi Mteule wa Mungu,

Hakuna njia ya kulikwepa, wewe ni Jeni ya Kiroho ya Mungu, dhihirisho la sifa za mawazo Yake, nawe ulikuwa ndani Yake kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Hatuwezi kwenda zaidi, tunafanana kabisa na punje ile ile iliyoingia ardhini. Sisi ni Yesu yeye yule, katika mfano wa Bibi-arusi, tukiwa na nguvu zile zile, Kanisa lile lile, Neno lile lile linaloishi na kukaa ndani yetu, linafikia kilele chake, TAYARI KWA UNYAKUO.

Yeye alituambia tulivunja ndoa yetu ya kwanza, kwa mauti ya kiroho, na sasa tumezaliwa mara ya pili, ama tumeolewa tena, kwenye ndoa yetu mpya ya Kiroho. Si ya maisha yetu ya kimaumbile ya kale na mambo ya ulimwengu, bali ni ya Uzima wa Milele. Ile chembe hai iliyokuwa ndani yetu hapo mwanzo, imetupata!

Hilo linamaanisha nini? Linamaanisha kitabu chetu cha zamani kimetoweka pamoja na ndoa yetu ya zamani, kimehamishwa. SASA kiko katika “Kitabu Kipya” cha Mungu; si kitabu cha uzima… la, la, la… bali katika Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo. Kile Mwanakondoo alichokomboa. Ndicho cheti chetu cha ndoa ambapo Chembechembe yetu ya kweli ya uhai ya Milele inakaa.

Je! uko tayari? Hili hapa laja. Afadhali ujifinye na kujitayarisha kupaza sauti na kupiga kelele utukufu, haleluya, Bwana asifiwe, lina mitutu miwili na risasi za mbinguni.

“Unataka kuniambia ya kwamba kitabu changu cha zamani pamoja na makosa yangu yote na kushindwa kwangu kote…”

Mungu alikiweka kwenye Bahari ya Usahaulifu Wake, nawe si tu kwamba umesamehewa, bali umehesabiwa haki…Utukufu! “Umehesabiwa haki.”

Na hilo linamaanisha nini? Linamaanisha wewe hata hukuwahi kulitenda jambo hilo Machoni pa Mungu.
Unasimama mkamilifu mbele za Mungu. UTUKUFU! Yesu, Neno, alipachukua mahali pako. Yeye alifanyika wewe, ili wewe, mwenye dhambi mchafu, upate kufanyika Yeye, NENO. Sisi ni NENO.

Hilo linatufanya sisi ile Chembechembe Yake ndogo ya uhai iliyokusudiwa tangu mwanzo. Sisi ni Neno likija juu ya Neno, juu ya Neno, juu ya Neno, juu ya Neno, nasi tunafikia kimo kikamilifu cha Kristo kusudi Yeye apate kuja kutuchukua tuwe Bibi-arusi Wake.

Nini kinachotendeka SASA HIVI?

Ni Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo wakikusanyika kulizunguka Neno, kutoka ulimwenguni kote.

Hili linaenda kote nchini. Huko New York, sasa ni saa tano na dakika ishirini na tano. Juu kule Philadelphia na karibu kote kule, hao watakatifu wapendwa wanaoketi kule wakisikiliza, sasa hivi, katika makanisa kila mahali. Huko juu kabisa, huko chini kabisa karibu na Mexico, huko juu kabisa karibu na Canada na kila mahali, kotekote. Maili mia mbili, popote pale katika bara la Marekani ya Kaskazini hapa, karibu yote, watu wako chonjo, wakisikiliza hivi sasa. Maelfu mara maelfu, wakisikiliza.

Na huo ndio Ujumbe wangu kwenu, enyi Kanisa, ninyi ambao ni muungano, muungano wa kiroho kwa Neno.

Yeye alisema ulikuwa ni muungano wa kiroho wa Kristo na Kanisa Lake, Nao UNATENDEKA SASA HIVI. Mwili unafanyika Neno, nalo Neno linafanyika mwili. Tumedhihirishwa, na kuthibitishwa; vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, Nalo linatendeka sasa, siku baada ya siku katika kila mmoja wetu.

Mungu anaenda kuwa na Kanisa adilifu. Bibi-arusi Neno Wake mkweli na mwaminifu. SISI NDIO BIBI MTEULE wa Bwana wetu Yesu Kristo.

Ni Saa Ngapi, Bwana?

Tuna ufunuo katika siku hizi za mwisho, kwa ajili ya Ujumbe wa Bwana Mungu kumkusanya Bibi-arusi Wake pamoja. Hakuna wakati mwingine ambao umeahidiwa hilo. Imeahidiwa katika wakati huu: Malaki 4, Luka 17:30, Yohana Mtakatifu 14:12. Yoeli 2:38. Ahadi hizo ni kama tu vile Yohana Mbatizaji alivyojitambulisha katika Maandiko.

Ni nani aliyeyatimiza maandiko haya?

Malaika Wake wa saba mwenye nguvu, William Marrion Branham. Daima alifanya jambo hilo kwa mpangilio. Alilifanya kila wakati kwa mpangilio. Yeye analifanya tena katika siku yetu, akimwita atoke na kumkusanya Bibi-arusi Wake mwadilifu katika siku ya mwisho kwa nabii Wake.

Ni wakati mtukufu jinsi gani ambao Bibi-arusi alionao. Kila kukusanyika kunakuwa kukuu zaidi na zaidi na kutamu zaidi na zaidi. Hakujawahi kuwa na wakati kama huu. Mashaka yote yametoweka.

Njoo uungane nasi tunapomsikia Neno lililoahidiwa la siku yetu akinena, na kutuambia sisi ni nani na kipi kinachotukia katika siku yetu. Muungano Usioonekana wa Bibi-arusi wa Kristo 65-1125.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko:

Mathayo 24:24
Luka mt. 17:30 / 23:27-31
Yohana 14:12
Matendo 2:38
Warumi 5:1 / 7:1-6
2 Timotheo 2:14
1 Yohana 2:15
Mwanzo 4:16-17 / 25-26
Danieli 5:12
Yoeli 2:28
Malaki 4