UJUMBE: 64-0830M Maswali na Majibu #3
- 26-0208 Maswali na Majibu #3
- 24-0512 Maswali na Majibu #3
- 22-1016 Maswali na Majibu #3
- 18-0218 Maswali na Majibu #3
Wapendwa Aliomzalia Kristo,
Mtu anawezaje kuuweka katika maneno matupu ya kibinadamu upendo na furaha iliyo mioyoni mwetu kuujua Ufunuo wa kweli wa Neno Lake kwa ajili ya siku yetu? Kuwazia, hatukuwa na uhusiano wowote nalo, lakini YEYE, Yule MIMI NIKO aliye Mkuu, kwa uchaguzi Wake Mwenyewe, Yeye alituchagua SISI kimbele kuwa na kitu kikubwa zaidi ambacho angeweza kutupa, UFUNUO WA NENO LAKE KWA AJILI YA WAKATI WETU.
Yeye alingoja, hadi utimilifu wa wakati ulipotimia, atupulizie pumzi ya uhai ndani yetu, ili tuweze kumsikia Yeye akizungumza nasi na kusema:
Sasa, nimejaribu kadiri niwezavyo ku—ku—kuwaarifu ninyi watu na kuwaongoza kama baba angewaongoza watoto wake. Ninyi mu watoto wangu; nimewazaa katika Kristo kwa Injili hii ninayohubiri. Ona? Nami—ni—ni—ninawatakeni mkuze watoto waliokomaa vilivyo, au—au watoto. Nami nataka kuwakabidhini Kristo siku hiyo, kama vile Paulo alivyosema, “Bikira safi.” Hakuna kitu katika Neno ila lile moyo wako utaitikia kwa “amina.”
Mungu, akinena kupitia malaika Wake mwenye nguvu, anatuelekeza na kutuongoza, Bibi-arusi wa Yesu Kristo. Sisi ndio bikira Wake safi, watoto waliyokomaa. Na kwa neema Yake ya ajabu, tunaliitikia kila Neno tunalosikia kwa AMINA! Ndio fasiri kamilifu ya Neno lenye thibitisho la Kiungu!
• Ikiwa Sauti tunayoisikia kwenye kanda ndio: fasiri kamilifu ya Neno, ni kitu gani kingine ambacho Bibi-arusi wa Yesu Kristo anachohitaji?… HAKUNA!
Yeye ametuchagua SISI, kundi Lake dogo alilolichagua kwa mkono Wake, ili tuwe na Ufunuo wa kweli wa Neno Lake la wakati wetu. Sisi ndio aliowachagua kuwapo duniani, katika miili ya nyama, wakati wa ile miaka elfu moja ya Utawala wa Miaka Elfu.
Enyi marafiki, hebu tulizungumzie hilo kwa dakika moja.
Tutakuwa na mwili uliotukuzwa papa hapa duniani. Tutakuwa tukila, tukinywa, tukijenga majumba, tukiishi kama tunavyoishi sasa kwa miaka elfu moja. Itakuwa ni fungate yetu ambapo Bibi-arusi (SISI) na Bwana harusi (Bwana Yesu Kristo) wamefanyika MMOJA.
Tunakesha na kungoja wakati huu mtukufu kila dakika ya kila siku. Uko karibu sana kiasi kwamba inaonekana kama tunaweza kuugusa. Ninaamini, kwa moyo wangu wote, hili ndilo linalotendeka kwetu sisi leo:
Loo, huo muungano wa kiroho wa Kristo na Kanisa Lake sasa, wakati mwili unapofanyika Neno, nalo Neno linafanyika mwili, linadhihirishwa, linathibitishwa. Vile vile hasa Biblia ilivyosema ingetendeka katika siku hii, inatendeka, siku baada ya siku. Mbona, inalundikana upesi sana huko nje, katika yale majangwa, na mambo yanayotendeka, hata nisingeweza kufuatilia jambo hilo. Tuko karibu na kule Kuja kwa Yesu, kuunganishwa na Kanisa Lake, ambapo Neno linafanyika Neno.
Kwa kila Ujumbe tunaosikia, ndivyo Yeye anavyozidi kutupata Ufunuo zaidi. Unalundikana upesi sana hivi kwamba hata hatuwezi kufuatilia jambo hilo. Tunaliona Neno likifanyika Neno zaidi ya wakati wowote. Hakuna shaka moja hata chembe; kwa Ufunuo, tunajua sisi ni nani haswa.
Yeye anamuunganisha Bibi-arusi Wake kama vile tu alivyosema angefanya, nasi tu sehemu ya hilo. Tunaliona likitendeka kwa macho yetu wenyewe. Wengine huenda wasilione ama kulielewa. Hilo si kwa ajili yao, NI KWA AJILI YETU SISI, WATOTO WAKE ALIOWAZAA.
Bibi-arusi walikuwa na maswali ya kumuuliza nabii.
Je, inatosha kusikiliza Sauti ya Mungu PEKE YAKE kwenye kanda? Mungu alijibu na kusema: NDIYO!!
Je, watoto wetu pia wanaweza kupata kila kitu wanachokihitaji ili kuwa Bibi-arusi wa Kristo kwa kusikiliza kanda tu: NDIYO!!
Kwa hivyo, Kila kitu Bibi-arusi anachokihitaji kipo KWENYE KANDA.
Pia tunajua Mungu ameziandaa njia zingine nyingi kwa ajili ya watoto Wake.
“Kwa kupigwa Kwake wewe uliponywa.” Sasa, kwanza Neno linasema hivyo, hilo linapaswa kutosha, lakini ikiwa huliamini katika Neno, basi kuna karama Kanisani, kama vile wanaume waliovuviwa kujua jinsi ya kufundisha hilo, hilo litafanya liwe wazi kwako, ndilo, na imani ya kuamini.
Tunashukuru mno Mungu amewaandaa wanaume waliovuviwa kujua jinsi ya kufundisha uponyaji na Neno Lake ili kulifanya wazi kwa wengine, lakini Bibi-arusi Wake anataka NJIA YAKE KAMILIFU ILIYOANDALIWA ITOSHELEZAYO. Ndiyo tu TUNAYOHITAJI.
Ningependa kuwaalika muungane na Maskani ya Branham Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) tunaposikia: Maswali na Majibu #3 64-0830M.
Ni jambo la kupendeza vipi kuwa na Ufunuo wa Neno Lake na kujua kwamba sisi ni Neno lililofanyika mwili.
Ndugu Joseph Branham