UJUMBE: 64-0802 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 26-0111 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 24-0414 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 23-0312 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 22-0918 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 21-0502 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 19-1103 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
- 17-0924 Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi Wa Mbinguni Na Bibi-Arusi Wa Duniani
Mpendwa Kipenzi Cha Moyo Wangu,
Nakupenda sana. Wewe ni mwili wa mwili Wangu, na mfupa wa mfupa Wangu. Hata kabla sijaziumba nyota, mwezi, ulimwengu Wangu wote, nilikuona nami nilikupenda wakati huo. Nilijua wewe ulikuwa sehemu Yangu, Kipenzi Changu cha pekee. Wewe na Mimi tulikuwa MMOJA.
Ile siku ambayo nimeitamani na kuisubiri tangu nilipowaona hatimaye imefika. Sasa ninawaita na kuwaunganisha kutoka mashariki na magharibi, kaskazini na kusini, kwa Sauti Yangu. Ninyi ni mawazo Yangu, Neno Langu, Bibi-arusi Wangu, aliyedhihirishwa.
Nimetamani sana kuwaambia kila kitu kilicho moyoni Mwangu, kwa hivyo Nililiandika kupitia manabii Wangu na nimelilinda kwa maelfu ya miaka. Wengi wamelisoma, na kuliamini kwa karne nyingi, lakini nimeyaweka mambo mengi kuwa siri hadi NINYI MLIPOFIKA. Ninyi ndio WATU PEKEE nitakaowaambia.
Wao walitamani kuyajua na kuyasikia mambo haya yote ya ajabu ambayo nimeyaficha, lakini kama vile nilivyokuahidi, nimesubiri na kuyaweka kuwa siri hadi hivi sasa, kwa ajili yako WEWE tu, WANGU MMOJA NA WA PEKEE.
Nilikuahidi Mimi ningekuja na kujifunua Mwenyewe tena katika mwili wa mwanadamu, ili niweze kukuambia, na kukufunulia mambo haya yote. Nilitaka uisikie SAUTI YANGU ikizungumza nawe moja kwa moja.
Nimewatia mafuta wengine wengi kwa Roho Wangu Mtakatifu kukuambia kuhusu upendo Wangu, lakini kama nilivyofanya siku zote, Nami kamwe siwezi kubadilika, nilimchagua mtu mmoja: Malaika Wangu, Nabii Wangu, awe Sauti Yangu ili niweze kunena Bwana Asema Hivi kwako.
Nilitaka kukuambia, wewe hukuokolewa siku yoyote Maalum. Daima ulikuwa umeokolewa. Nilikuja tu kukukomboa. Uliokolewa tangu mwanzo kwa maana ulikuwa na Uzima wa Milele, kwanza. Kwa hivyo, machoni Pangu, dhambi zako zote haziwezi hata kuonekana Nami, kitu pekee ninachosikia ni sauti yako. Ninauona tu uwakilisho wako.
Jinsi gani nimesubiri kwa hamu kukuambia mambo mengi. Moyo wangu unabubujika kwa shauku. Jinsi gani nimeisubiri kwa hamu Karamu yetu ya Harusi, Miaka elfu moja ya Utawala wetu Wa Miaka Elfu tukiwa pamoja. Nikikuambia kwa undani kuhusu Makao Yetu ya Baadaye pamoja; Jinsi nilivyokuandalia kila kitu, kila kitu jinsi tu unavyopenda hasa.
Kipenzi Changu, ikiwa unaona ni vizuri mno sasa hivi kuisikiliza Sauti yangu ikizungumza nawe, subiri tu, hiki ni kivuli tu cha jinsi itakavyokuwa wakati tutakapoishi Katika ule Mji pamoja. Nabii wako yeye hata ataishi karibu nawe; atakuwa jirani yako.
Tutatembea kwenye barabara hizo za dhahabu na kunywa kutoka kwenye chemchemi pamoja. Tutatembea katika paradiso za Mungu huku Malaika wakiizunguka dunia, wakiimba nyimbo za sifa….Itakuwa ni Siku ya namna gani!
Najua njia inaonekana inaparuza, na wakati mwingine inakuwa ngumu kwako, lakini itakuwa kitu kidogo sana, kidogo sana, Tutakapokuwa pamoja.
Kwa sasa, nitakukusanya Kwa mara nyingine tena na kuzungumza nawe Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville, (ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) na kukuambia kila kitu kuhusu “Makao Ya Baadaye Ya Bwana Arusi wa Mbinguni na Bibi-arusi wa Duniani”. Nasubiri kwa hamu kuungana nawe wakati huo.
Kumbuka, na kamwe usisahau, nakupenda sana.
Kwa niaba Yake,
Ndugu Joseph Branham
Maandiko:
Mathayo Mt. 19:28
Yohana Mt. 14: 1-3
Waefeso 1:10
2 Petro 2:5-6 / Sura ya 3
Ufunuo 2:7 / 6:14 / 21:1-14
Walawi 23:36
Isaya Sura ya 4 / 28:10 / 65:17-25
Malaki 3:6