UJUMBE: 62-1014M Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 25-0601 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 20-1004 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 18-1125 Kimo Cha Mtu Mkamilifu
- 16-1023 Kimo Cha Mtu Mkamilifu – Preliminari
Wapendwa, Minara Ya Ukumbusho Iliyo Hai,
Sauti tunayoisikia kwenye kanda ndio Urimu na Thumimu ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake. Hiyo sasa imemuunganisha sawasawa pamoja Bibi-arusi Wake katika moyo mmoja na nia moja kuwa kanisa halisi lililojazwa na Roho, lililojaa nguvu za Mungu, linaloketi pamoja katika katika mahali pa kimbinguni, likitoa dhabihu za kiroho, sifa za Mungu, huku Roho Mtakatifu akitembea kati yetu.
Kristo alitutumia sisi Roho Wake Mtakatifu anene kupitia malaika Wake wa saba ili atujenge sisi kama watu binafsi tufikie kiwango cha Yesu Kristo, kusudi tupate kuwa kituo cha nguvu na makao ya Roho Mtakatifu, kwa Neno Lake.
Sisi ni warithi wa kila kitu. Ni mali yetu binafsi, hiyo ni MALI YETU sisi. Ni zawadi ya Mungu kwetu, na hakuna mtu anayeweza kuichukua kutoka kwetu. NI YETU.
“Lolote mtakalomwomba Baba katika Jina Langu, hilo nitalifanya.” Nani awezaye kukana lolote hapo? “Amin, amin, nakuambia, ukiuambia mlima huu, Ng’oka, wala usitie shaka moyoni mwako, bali waamini kwamba hayo uliyosema yatatukia, lolote ulilosema litakuwa lako.” Ni ahadi zilizoje! Haziishii tu kwenye uponyaji, lakini kwa lo lote.
Utukufu kwa Mungu…LOLOTE TUOMBALO!
Tangu mwanzo wa wakati, viumbe vyote vya Mungu vimekuwa vikiugua na kuingojea siku ambayo wana wakamilifu wa Mungu watakapodhihirishwa. Siku hiyo imefika. Hii ndiyo siku hiyo. Huu ndio huo wakati. Sisi ndio hao wana na binti za Mungu waliodhihirishwa.
Sisi ni chombo kilicho hai cha Mungu anachotembelea, anachoona nacho, anachotumia kuzungumza, anachofanyia kazi. Ni Mungu akitembea kwa miguu miwili NDANI YETU.
Sisi tu nyaraka Zake zilizoandikwa zinazosomwa na watu wote. Wana na binti Zake wenye mamlaka waliochaguliwa, waliochaguliwa tangu zamani, anaowafanya kuwa mtu aliye hai, sanamu hai, kimo cha mtu mkamilifu.
Tunaanguka kifudifudi mbele ya Mungu aliye hai, nguvu zilizo hai, maarifa hai, saburi hai, utauwa hai, Nguvu hai zitokazo kwa Mungu aliye hai, zinamfanya mtu aliye hai kuwa sanamu hai katika kimo cha Mungu.
Ni Kristo, katika utu wa Roho Mtakatifu juu yetu, pamoja na ubatizo wa kweli wa Roho Wake Mtakatifu, na Wema Wake wote ukiwa umetiwa muhuri ndani yetu. Mungu, akiishi ndani yetu katika Maskani iitwayo Jengo. Maskani iliyo hai, ya mahali pa kukaa Mungu aliye hai; Kanisa kamilifu, kwa ajili ya Jiwe Kamilifu la Kifuniko la kutufunika.
Mungu alimtuma nabii kumwita Bibi-arusi Wake atoke na kumwongoza. Ilikuwa ni Adamu Wake wa kwanza aliyerejeshwa kikamilifu, kimo cha mtu mkamilifu katika siku yetu, kulifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake.
Siwezi kuondoshwa kwenye hilo. Hakuna kinachoweza kuniondosha. Sijali mtu ye yote anasema nini; halinisogezi hata kidogo. Nitashikilia papo hapo.
Nitangoja, nitangoja, nitangoja. Haileti tofauti yo yote. Inashikilia pale pale. Kisha, siku moja, nitapiga kelele pamoja na watakatifu wengine wote kwa moyo mmoja: “Tunapumzika kwa uhakika juu ya kila Neno!
Ninaahidi, asubuhi ya leo, Kwake, kwa moyo wangu wote, ya kwamba, kwa masaada Wake na kwa neema Yake, ninaomba ya kwamba nitaomba kila siku, bila kukoma, mpaka nitakaposikia kila moja ya mahitaji haya yakitiririka katika maskini mwili wangu huu, mpaka niweze kuwa dhihirisho la Kristo aliye hai.
KWANGU MIMI, kuisikiliza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndio mpango wa Mungu kwa ajili ya siku hii. Ndilo Neno lililo hai la Yesu Kristo. Ndio Yakini yangu kulingana na Neno la Mungu. Ndio njia ya Mungu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.
Hivyo, ningependa kuwaalika kuungana nami Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) ninapomsikiliza William Marrion Branham, ambaye ninaamini kuwa ndiye Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku yetu, akimfundisha Bibi-arusi wa Kristo jinsi ya kuwa: Kimo Cha Mtu Mkamilifu 62-1014M.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko ya kusoma kabla ya Ujumbe:
Mathayo 5:48
Luka Mtakatifu 6:19
Yohana Mtakatifu 1:1 / 3:3 / 3:16 / 5:14 / 14:12
Matendo 2:38 / 7:44–49 / Sura ya 10 / 19:11 / 28:19
Waefeso 4:11-13
Wakolosai Sura ya 3
Waebrania 10:5 / 11:1 / 11:32-40
Yakobo 5:14
2 Petro 1-7
Isaya 28:19