25-0525 Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #4

UJUMBE: 60-0522E Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #4

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waongofu,

Kwa Kubonyeza Play, tunalisikiliza Neno la Mungu lisilokosea. Ni kila Neno Kweli, kila kifungu Chake. Tumeitwa na kuhifadhiwa, tumejazwa na kutengwa; tumejazwa na Roho Mtakatifu, na sasa tayari tuko katika Nchi ya Kanaani. Hatuogopi cho chote…LO LOTE LILE, tunajua sisi ni nani.

Kwa sababu tumedumu na Neno Lake, kama alivyotuamuru kufanya, Anaenda kutuambia kwamba alituachia sisi urithi. Ulilifanya jambo hilo lini, Baba? Nilipowachagua ninyi na kuyaweka majina yenu kwenye Kitabu cha Uzima cha Mwana-Kondoo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Wakati utimilifu wa wakati ulipowadia, nilimtuma Yesu Mwana-Kondoo, Aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, ili muupate urithi wenu wa kuwa wana na binti Zangu, miungu wadogo.

Ilinibidi niwakague mitikisiko na sehemu zilizolegea kabla sijawaweka mahali penu.

● “Je! Unaamini kuicheza Sauti Yangu iliyo kwenye kanda kanisani ni makosa?”

● “Ndiyo, hupaswi kuzicheza kanda kanisani.”

● “Analikataa. Unatikisika.”

● “Je! Unaamini Neno Langu lililo kwenye kanda linahitaji kufasiriwa?”

● “Ndiyo, Linahitaji mtu fulani kulifafanua.”

● “Unatikisika. Lipige teke nje. Bado hauko tayari.”

Ukiwa tayari, utasema, “Amina” kwa kila Neno.

● “Je! Mnaamini kwamba Mimi ni yeye yule jana, leo na hata milele?”

● “Amina.”

● “Je! Mnaamini kuwa Sauti Yangu iliyo kwenye kanda ndio SAUTI ILIYO MUHIMU KULIKO ZOTE mnayopaswa kuisikia?”

● “Amina.”

● “Je! Mnaamini Sauti Yangu iliyo kwenye kanda ndio itakayomuunganisha Bibi-arusi?”

● “Amina.”

● “Je! Mnaamini kwamba malaika Wangu mwenye nguvu ndiye atakayewatambulisha ninyi Kwangu Mimi?”

● “Amina.”

Mmeanza kukazika sasa. Nimewakagua mtikisiko na maeneo yaliyolegea. Niko tayari kuufunga mlango. Nitauweka Muhuri Wangu juu yenu. Mmefuzu ukaguzi Wangu.

Sasa hebu niwaambieni jambo fulani, Enyi Watu Wangu wapendwa na wa thamani mlio katika nchi za kanda; huko nchi za ng’ambo na popote mlipo, msiogope. Kila kitu ni sawa. Niliwajua ninyi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Nilijua mambo yote yatakayotukia.

Ninakuja kuwachukua ninyi hivi karibuni na kuwapeleka Mahali ambapo Hakuna mauti, hakuna huzuni, hakuna wivu, hakuna kitu cho chote; Ni ukamilifu tu, upendo mkamilifu.

Hadi wakati huo, msisahau kamwe, Ninawapa Neno Langu, NINYI NI NENO LANGU lililofanyika mwili. Kama mnahitaji JAMBO LOLOTE, Linene, kisha Liaminini; Ni urithi wenu.

Nitawatumia ninyi Sauti Yangu tena Jumapili hii na kuwafafanulia jambo Hilo Lote. Nitawaambia kwa mara nyingine tena ninyi ni nani, wapi mnakoelekea, na jinsi gani kulivyo kule ng’ambo, sasa hivi.

Njooni muungane na Bibi-arusi Wangu ninapowafanya wao waketi pamoja katika mahali pa Mbinguni Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) na mnisikie Mimi nikiwaweka ninyi mahali penu kwa Neno Langu. 60-0522E Kufanywa Wana Wenye Mamlaka #4

Ndugu. Joseph Branham