24-1006 Ufunuo Wa Yesu Kristo

UJUMBE: 60-1204M Ufunuo Wa Yesu Kristo

PDF

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Jeshi la Mungu Lisiloweza Kushindwa,

Sisi ndio wale ambao Baba aliyowachagua na kuwapa UFUNUO WA KWELI wa Yeye Mwenyewe; KANISA Lake la KWELI na pekee. Wale aliowachagua watende KAZI Yake KUBWA ZAIDI. Kwa maana kwa Roho Wake, tunaweza kuitambua na kuipinga roho ya mpinga-Kristo ya Shetani. Yeye HANA NGUVU mbele ZETU, kwa sababu sisi ni Jeshi Lake Lisiloweza Kushindwa.

Shetani anachukia ufunuo wote. LAKINI SISI TUNAUPENDA. kwa maana sisi ni wapenzi wa Neno la Mungu lililofunuliwa. Tukiwa na ufunuo wa kweli maishani mwetu, milango ya kuzimu haiwezi kutushinda, tunamshinda adui. Kila pepo yuko chini ya miguu yetu. Sisi ni Mmoja na Yeye nasi tunaweza kunena Neno, kwa maana sisi ni Neno Lake.

Bwana ameliweka hilo moyoni mwangu kwamba tujifunze na kuzisikia Nyakati Saba za Kanisa. Zitakuwa Wiki kuu sana kwa kila mmoja wetu. Atakuwa akitufunulia Neno Lake kuliko hapo awali, kwa nguvu zake za ushindi.

Huu sasa ndio wakati. Haya ndio majira yake. Atakuwa akituhuisha, akitutia moyo, kwa kutupa Changamko kwa Ufunuo, nalo Litaiwasha moto mioyo yetu!!

Ufunuo wa Yesu Kristo ni Kitabu cha kinabii ambacho kinaweza tu kueleweka na tabaka fulani la watu walio na ono la kinabii, SISI, Bibi-arusi Wake. Inahitaji Ufunuo wa KWELI kujua kwamba unasoma na kuisikia Sauti ya Mungu inayotoka kwa malaika-mjumbe Wake aliyemchagua, akitupa mafundisho ya kimbinguni.

Ni Ufunuo wa Yesu Kristo aliopewa Yohana kwa ajili ya Wakristo wa nyakati zote. Ndicho kitabu pekee katika Biblia nzima ambacho kimeandikwa na Yesu Mwenyewe, kwa kumtokea mwandishi Yeye Mwenyewe.

Ufunuo 1:1-2, “Ufunuo wa Yesu Kristo, aliopewa na Mungu awaonyeshe watumwa wake mambo ambayo kwamba hayana budi kuwako upesi; naye akatuma kwa mkono wa malaika Wake na kumwonyesha mtumwa Wake Yohana: aliyelishuhudia Neno la Mungu, na ushuhuda wa Yesu Kristo, yaani, mambo yote aliyoyaona.

Kitabu cha Ufunuo ni mawazo ya Mungu kabisa yaliyoandikwa na Mungu Mwenyewe. Lakini Yeye alituma na kumwonyesha mtumwa Wake Yohana kupitia malaika Wake. Yohana hakujua maana Yake; aliandika tu kile alichokiona na kusikia.

Lakini leo, Mungu alimtuma malaika Wake mwenye nguvu duniani kufunua Ufunuo huu Mkuu kwa Bibi-arusi Wake, ili tuweze kusoma na kusikia yale yaliyokuwa yametukia katika nyakati zote za kanisa. Tunaweza kuliona lile kundi Lake dogo lile lililodumu mwaminifu na wa kweli kwa Neno katika kila Wakati.

Mungu alinena kupitia malaika Wake na kusema ya kwamba katika siku hizi za mwisho, wakati Sauti ya mjumbe Wake wa wakati wa saba wa kanisa itakapoanza kupiga baragumu, Yeye atafunua siri za Mungu kama zilivyofunuliwa kwa Paulo. Wale wanaompokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe watapokea matokeo mema ya huduma ya nabii huyo.

Utukufu, sisi ni Bibi-arusi wa Kubonyeza Play wa Mungu ambaye tumempokea nabii huyo katika jina lake mwenyewe, nasi tunapokea matokeo mema. Tunaamini ni Sauti ya Mungu inayonena na kumwongoza Bibi-arusi Wake.

Lo, Kanisa, kile tutakachosoma na kukisikia katika wiki zijazo. Kwake Yeye, sisi tunafananishwa na dhahabu SAFI. Kile alicho Yeye, ndicho tulicho. Sisi ndio Mzabibu Wake wa Kweli. Tumeshinda. Tumefanywa wakamilifu, tumeimarishwa, tumetiwa nguvu. Tumechaguliwa kwa Upendo Wake wa Kuchagua. Hakuna cha kuogopa. Sisi ndio kundi lile lililomsikia mjumbe na Ujumbe wake na Kuutwaa na Kuuishi.

Kila wiki tutakuwa tunasema, “Je, mioyo yetu haiwaki ndani yetu wakati Yeye anaponena na kutufunulia Neno lake njiani”.

Ukitaka kuuhisi upako wa Roho Wake Mtakatifu, kupokea Ufunuo zaidi wa Neno la Mungu, na unataka kuketi katika uwepo wa Mwana kuivishwa, na kupokea Imani ya Kunyakuliwa, njoo uungane nasi Jumapili saa 6:00 Sita MCHANA, saa za Jeffersonville.(Ni saa 1:00 Moja JIONI ya Afrika Mashariki), tunapoanza somo letu kuu juu ya: Ufunuo Wa Yesu Kristo 60-1204M.

Ndugu. Joseph Branham

Ningependa kukuhimiza usikie, au kusoma, kila wiki Kitabu cha Maelezo ya nyakati za Kanisa, sura tuliyomaliza kusikiliza kila Jumapili.