24-0623 Ndoa Na Talaka

UJUMBE: 65-0221M Ndoa Na Talaka

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Safi Asiyeghoshiwa wa Neno,

Sisi ndio Bibi Wake mdogo anayependeza; asiyeghoshiwa, asiyeguswa na dhehebu la mtu ye yote, nadharia yo yote iliyobuniwa na mwanadamu. Sisi ni Bibi-arusi wa Neno asiyeghoshiwa kabisa! Sisi ndio yule binti wa Mungu aliyetiwa mimba.

Sisi ni watoto wa Neno Lake lililonenwa, ambalo ni Neno Lake la asili! Hakuna dhambi katika Mungu, kwa hivyo hakuna dhambi ndani yetu, kwa vile tulivyo mfano Wake Mwenyewe. Twawezaje kuanguka? Hilo Haliwezekani….HAIWEZEKANI! Sisi ni sehemu Yake, NENO Lake LA ASILI.

Tunawezaje kujua hili bila shaka yoyote? UFUNUO. Biblia nzima, Ujumbe huu, Neno la Mungu, yote ni Ufunuo. Hivyo ndivyo tunavyojua ukweli kati ya Sauti hii na sauti zingine zote, kwa sababu ni Ufunuo. Na Ufunuo wetu unaambatana kabisa na Neno, sio kinyume cha Neno.

Na juu ya mwamba huu” (ufunuo wa kiroho wa Neno ni nini) “Nitajenga Kanisa Langu; wala milango ya kuzimu haitaliangamiza.” Mke Wake hatashawishiwa na mwanamume mwingine. “Nitalijenga Kanisa Langu, na milango ya kuzimu haiwezi kulitikisa kamwe.”

Tutakuwa wakweli na waaminifu kwa Neno Lake na Sauti Yake, peke yake. Kamwe hatutatiwa unajisi na mwanamume mwingine na kufanya uzinzi. Tutabaki kuwa Bibi-arusi Neno Bikira Wake. Hatutaangalia, kusikiliza au kuvutiwa na neno lingine lolote.

Liko ndani ya mioyo yetu. Hatungaliweza kamwe kuwa na mume mwingine, ila MUME wetu MMOJA, Yesu Kristo, Mtu mmoja, Mungu, Imanueli. Mkewe atakuwa maelfu mara maelfu ya maelfu. Hilo linaonyesha ya kwamba Bibi-arusi hana budi kutoka katika Neno. “Bwana Yesu Mmoja, na Bibi-arusi Wake wengi, umoja.”

Lazima tukumbuke na kuelewa hili si la kila mtu, ni kundi la nabii PEKE YAKE. Wafuasi wake mwenyewe. Ujumbe huu ni kwa ajili yao tu, lile kundi dogo ambalo Roho Mtakatifu alimpa kulisimamia.

Mungu atamwajibisha yeye kwa yale anayotuambia, na Mungu atatuwajibisha sisi, waongofu wake kutoka nchini kote, wale ambao amewaongoza kwa Kristo, kuamini kila Neno Lake na kutokupatana kamwe.

Ni jambo lakupendeza sana jinsi gani kwetu kuketi na kumsikiliza Yeye akitueleza jinsi sisi tulivyo wateule wake. Jinsi Bibi-arusi Wake wa kwanza, na Bibi-arusi wa pili, walivyomwangusha; Bali sisi, Bibi-arusi Wake mkuu wa wakati wa mwisho HATUTAMWANGUSHA. Tutabaki kuwa Bibi-arusi Neno Bikira Wake wa kweli, na mwaminifu hadi mwisho.

Imani yetu katika Neno lake inakua zaidi kila siku. Tunajiweka wenyewe tayari kwa kusikiliza na kutii kila Neno Lake, kuisikia Sauti yake ikinena nasi, kuzisoma Biblia zetu, kuomba na kumwabudu Yeye siku nzima.

Tunajua Yeye anakuja upesi sana. Dakika yoyote sasa. Kama vile Nuhu, tulikuwa tukitumaini Yeye alikuwa yuaja jana; labda kesho asubuhi, adhuhuri, jioni, lakini tunajua Yeye anakuja. Nabii wa Mungu na Neno Lake hawakosei, ANAKUJA. Tunahisi ni siku ya 7, nasi tunaweza kuona mawingu yakijikusanya na matone makubwa ya mvua yakianguka; wakati umefika.

Tuko salama salimini ndani ya Safina, tukingojea kwa hamu kubwa. Njoo uungane nasi wakati tunaposikia Sauti ya Mungu ikitufariji Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, tunaposikia: Ndoa Na Talaka 65-0221M.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mt 5:31-32 / 16:18 / 19:1-8 / 28:19
Matendo 2:38
Warumi 9:14-23
Timotheo wa Kwanza 2:9-15
Wakorintho wa Kwanza 7:10-15 / 14:34
Waebrania 11:4
Ufunuo 10:7
Mwanzo sura ya 3
Mambo ya Walawi 21:7
Ayubu 14:1-2
Isaya 53
Ezekieli 44:22