NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI

24-0721

54-0411 – Imani Yako Imekuokoa

Ndugu, dada, nasema hivi kwa unyenyekevu na si kwa kuomba au kujaribu kuonewa huruma. Nguo nilizo nazo ni nguo ambazo watu hunipa. Suti niliyovaa, Ndugu Moore alikuwa pamoja nami, nami niliipata miaka minne iliyopita huko Sweden. Jozi ya viatu, mke wangu alininunulia. Nilipata suti nyingine kule nilipewa huko Florida. Nyingine niliipata Finland; mbili 0nilizipata Ujerumani, au si Ujerumani, bali Afrika. Hapo ndipo nguo zinatoka. Ni zile ambazo watu hunipa. Baadhi yao zilikuwa zao wakanipa mimi. Hiyo ni kweli. Nilipata suti kutoka California yapata miaka mitano iliyopita na nimekuwa nikiivaa tangu wakati huo. Na ni—ni yapata miaka sita, saba nilipoipata. Lakini ni nini? Inatosha. Yeye Hakuwa ila na vazi moja tu naye akaazima kaburi la mtu ili alazwe humo.

Ningekuwa na hali nzuri sana kama ningechukua pesa zote ambazo watu walikuwa wamenitolea, lakini ninataka kuwa maskini kama vile wale wanaokuja kuombewa. Sisi ni raia wenza wa Ufalme wa Mungu. Sisemi hivyo kwa kusema tu. Ninasema hivyo kwa sababu ninataka mjue, Enyi marafiki, kwamba Ufalme wa Mungu si utajiri au mavazi ya kifahari. Ni moyo uliojisalimisha kwa Mungu, ndipo Mungu anapofanya kazi.

MKATE WA KILA SIKU

Na Bwana anataka nini kwako, ila kutenda haki, na kupenda rehema, na kwenda kwa unyenyekevu na Mungu wako? Mika 6:8

24-0720

59-1128 – Mlango wa Moyo

Sasa, hebu tuangalie ndani ya moyo wa mwanadamu, ikiwa una milango ndani ya mlango. Sasa, watu husema, “Yesu, njoo moyoni mwangu, kwa sababu sitaki kwenda kuzimuni ninapokufa. Ninataka kukukubali Wewe kama Mwokozi wangu, lakini sitaki Wewe uwe Bwana wangu.”

Sasa, hapo kuna tofauti kabisa. Anaweza kuwa Mwokozi wako na bado asiwe Bwana wako. Wakati Yeye ni Bwana, Yeye ni Bwana juu ya yote. Kila sehemu yako, Yeye ni Bwana, amekaribishwa mahali popote moyoni mwako.

MKATE WA KILA SIKU

Tazama, nasimama mlangoni, nabisha; mtu akiisikia sauti yangu, na kuufungua mlango, nitaingia kwake, nami nitakula pamoja naye, na yeye pamoja nami. Ufunuo 3:20

24-0719

55-1110 – Maisha Yaliyofichwa Katika Kristo

Asubuhi moja, je, uliwahi kuamka asubuhi na mapema sana, kutoka nje mapema sana na kuinusa hewa hiyo safi, jinsi ilivyo na jinsi kila kitu kinavyoburudisha? Umande umeshuka.

Loo, ndugu, dada, kama jambo pekee unalojua ni kwenda kanisani, kama jambo pekee unalojua kwamba ulijiunga au ulibatizwa, ama kitu kama hicho, kwa nini usiyafiche maisha yako kwa Kristo. Kaa peke yako katika utulivu, mbali na ulimwengu na mahangaiko yake yote, na utulie na kutazama ni burudiko lililoje litakalokuja.

Unajua, Isaya alinena habari zake wakati mmoja. Alisema, “Amri juu ya amri, na kanuni juu ya kanuni, huku kidogo na huku kidogo. Shikilia lililo jema. Kwa midomo ya watu wageni na kwa lugha nyingine nitasema na watu hawa. Na hii ndiyo Sabato (au burudiko) ambayo inapaswa kutoka katika Uwepo wa Bwana.”

MKATE WA KILA SIKU

Na mfanywe wapya katika roho ya nia zenu Waefeso 4:23

24-0718

56-0405 – Kufufuka Kwa Yesu

Mungu hataki ukunje uso. Mungu anataka uwe na furaha. Moyo wa mwanadamu ulifanywa kuwa na furaha. Hofu itasababisha kansa. Hasira itasababisha kansa. Usikasirike kamwe. Tembea tu katika upendo Wake. Amina. Ukijua kwamba unatembea ndani Yake, na hakuna kitu kinachoweza kukudhuru. Hakuna kitu kinachoweza kukudhuru. Hakuna nguvu, mambo yaliyopo, mambo yajayo, hakuna kinachoweza kututenganisha naye. Tuko ndani Yake. Na kamwe hatuingii kwa mapenzi yetu wenyewe. Yeye, kwa hiari yake, alituchagua sisi na kutuleta kwake. Amina. Kwa hiyo ni kazi Yake kushughulikia kile alichojichukulia Mwenyewe. “Hakuna mtu awezaye kuwatoa katika mikono ya Baba Yangu, maana Yeye ndiye mkuu kuliko wote.” Amina. Ni Baba Anayelishughulikia. Ni nani aliye na nguvu zaidi ya Mungu? Kwa hivyo wewe una nguvu ya aina gani juu yako ya kukushughulikia? Nguvu zote zilizoumba ulimwengu. Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Enyi watu wote, pigeni makofi, Mpigieni Mungu kelele kwa Sauti ya shangwe. Zaburi 47:1

24-0717

56-0101 – Kwa Nini Watu Wana Rushwa Huku na Huku?

Mkristo harushwi huku na huku. Mkristo hakimbii kutoka sehemu moja hadi nyingine. Mkristo habishani na kukasirika, na kuhofia mambo. Mkristo anapumzika. Yote yamekwisha. Yote yalikwisha, kwa mwaminio, pale Kalvari. Hiyo ni kweli. Loo, magonjwa yanaweza kuja, na kukatishwa tamaa, lakini Mkristo amepumzika, akijua jambo hili, ya kwamba Mungu anaweza kutekeleza yale aliyofanya. Tukijua, ya kwamba, haidhuru kitu hicho ni nini na jinsi kinavyoonekana, hakuna magonjwa, huzuni, kifo, hakuna njaa ama cho chote kile, ambacho kinaweza kututenganisha na upendo wa Mungu ulio ndani ya Yesu Kristo. Tumepumzika. Acha tu hiyo meli ya kale ijirushe kwa njia yoyote inayotaka; nanga inashikilia.

MKATE WA KILA SIKU

Ili tusiwe tena watoto wachanga, tukitupwa huku na huku, na kuchukuliwa na kila upepo wa elimu, kwa hila ya watu, kwa ujanja, tukizifuata njia za udanganyifu. Waefeso 4:14

24-0716

53-0614A – Kuishindania Kwa Bidii Imani Waliokabidhiwa Watakatifu Mara Moja.

Mbona ndugu, Unaokolewa kwa imani. Hiyo ni kweli? Lakini sikiliza. Katika kukubali imani yako, Mungu huthibitisha imani yako kwa ubatizo wa Roho Mtakatifu. Ukisema unaamini, na hupati ubatizo wa Roho Mtakatifu, basi huna, ni—ni—imani yako haikubaliwi machoni pa Mungu. Una imani ya kiakili na badala ya imani ya moyoni. Hiyo ni kweli.

Unapomwamini Mungu kweli, Mungu yuko anawajibika kumwaga Roho Mtakatifu juu yako. Na basi kama akikumiminia Roho Mtakatifu…Unasema, “Vema, ninaye Roho Mtakatifu pia.” Vema, ukifanya hivyo, huna budi kuamini katika ishara na maajabu ya kimbinguni, kwa sababu umeongezwa kwake. Hiyo ndiyo imani.

MKATE WA KILA SIKU

Aaminiye na kubatizwa ataokoka; asiyeamini, atahukumiwa. Marko 16:16

24-0715

63-1116B – Uwekezaji

Katika Ufunuo 3, tunasoma hili, kwamba Kanisa la Laodikia, tumechorwa mojawapo ya picha zenye huzuni kuliko picha zote za Biblia nzima, Ufunuo 3, kwenye Kanisa la Laodikia. Makanisa mengine yote, kupitia Wakati wa Luther, na Nyakati Saba za Kanisa, kila mmoja, haikuninii, kasema kuhusu Yesu kuwa ndani ya kanisa, “Yeye aliye ndani ya kanisa.” Lakini katika Laodikia, Yeye alikuwa nje, akibisha, akijaribu kurudi ndani. Ni kitu cha kusikitisha namna gani kuwazia, kwamba, “Mwana wa Mungu, akibisha katika kanisa Lake Mwenyewe, akijaribu kurudi ndani.”

Lakini utajiri wa ulimwengu huu umepofusha macho yao. Si tu tajiri wa pesa, bali tajiri katika umaarufu, tajiri katika mambo ya ulimwengu, mahangaiko ya maisha, mpaka mmechangamana, na watu wenye elimu wameingia ndani na kuondolea mbali hiyo Punje, ile—ile Lulu yenye thamani kubwa. Lakini Mungu aliwachagua watu kimbele kuwa huko; mtu fulani anaenda kuwepo huko. Bali wao wanaikataa Hiyo. Si wote watakaofanya hivyo; baadhi yao wataipokea Hiyo. Sasa walimweka nje ya upendo wao, upendo wao wa Neno Lake.

MKATE WA KILA SIKU

Wamtumainio Bwana ni kama mlima Sayuni, Ambao hautatikisika, wakaa milele. Zaburi 125:1

24-0714

63-1110M – Nafsi Zilizo Kifungoni Sasa

Yesu alidai ya kwamba Yeye hajafanya kitu mpaka Baba alipomwonyesha. Naye Baba ni Roho Mtakatifu, tunatambua jambo hilo. Ni ofisi tu ya Mungu. Kama sivyo ilivyo, basi ni yupi kati yao aliye Baba ya Yesu Kristo? Yesu alisema Mungu alikuwa ndiye Baba Yake, nayo Biblia ilisema Roho Mtakatifu alikuwa Baba Yake. Naam, huwezi kumfanya awe mwana haramu, kwa hiyo Roho Mtakatifu ni Mungu, kwa hiyo Yesu alikuwa Mungu. Kwa hiyo, Mungu, Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu ni…Ni nini hii…Hivyo ni ofisi tatu za Mungu mmoja. Ni sifa tatu, Mungu yule yule.

Wewe ni sehemu ya Mungu, nami ni sehemu ya Mungu, unaona; lakini mimi si Mungu mzima, wala wewe si Mungu mzima. Unaona? Unaona? Ni sifa za Mungu juu yetu, kama wana waliofanywa wana na Yesu Kristo. Ambapo, Mungu Mwenyewe alifanyika mwili, apate kufa kwa ajili yetu.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana wako watatu washuhudiao [mbinguni, Baba, na Neno, na Roho Mtakatifu, na watatu hawa ni umoja. 1 Yohana 5:8

24-0713

61-0827 – Ujumbe Wa Neema

Kwa hiyo ilimbidi Mungu kufanyika mtu, Naye alikufa katika mwili wa binadamu, katika umbo la mtu aliyeitwa “Yesu Kristo,” na Huyo alikuwa Ndiye Masihi aliyeahidiwa aliyeinunua neema. Hapo ndipo unapoona ya kwamba Mungu na Kristo ni Mtu yule yule, Mungu akiishi katika Kristo. “Mimi na Baba Yangu ni Mmoja, Baba Yangu anaishi ndani Yangu; si Mimi ninayenena Neno, bali ni Baba Yangu anayeishi ndani Yangu.” Mungu katika Kristo! Hakika.

Neema iliahidiwa katika bustani ya Edeni, nayo neema ikaja, neema kwa Adamu na Hawa. Hakuna mahali pa kwenda, hakuna njia ya kugeukia na hata hivyo neema ilifanya njia!

Hebu niseme jambo hili, rafiki yangu mwenye dhambi. Huenda ukawa hapa asubuhi ya leo kahaba, huenda ukawa hapa asubuhi ya leo mwandama wanawake, huenda ukawa hapa mlevi ama mcheza kamari, ama mwuaji. Huenda ukawa hapa kama mume mchafu, mke mchafu. Huenda ukawa ndiye mwenye dhambi aliye mchafu kuliko wote. Unasema, “Nimepita kiwango hicho cha ukombozi.” La, hujapita, la sivyo usingekuwa kanisani asubuhi ya leo. Neema itakufanyia njia katika saa hii ya giza kama utaikubali. Ilimbidi Adamu kuwa radhi kuipokea, nawe pia. Ikubali.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa maana dhambi haitawatawala ninyi, kwa sababu hamwi chini ya sheria, bali chini ya neema. Warumi 6:14

24-0712

56-0406 – Neno La Mungu Lisiloweza Kukosea

Mungu, kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu, alitazama chini katika mkondo wa wakati naye akaona kila kitu kitakachokuwepo. Na kwa hiyo, Yeye angeweza kuwaita na kuwachagua wale ambao Yeye alijua kwamba angewaweka katika jengo Lake. Hiyo ni kweli. Na kama umeitwa usiku wa leo na Roho Mtakatifu na kupewa nafasi ya kuingia katika Ufalme wa Mungu, unapaswa kuwa na furaha. Amina.

Ikiwa uko katika Ufalme wa Mungu, na wewe ni sehemu ya mwili wa Kristo, Mungu ashukuriwe. Unaishi maisha hayo. Unafanya mambo yaliyo sahihi. Na kumbukeni, hili laweza kuzama kwa ukali kidogo tu linaposhuka, lakini liache limeng’enye kwa muda. Ikiwa uko katika mwili wa Kristo, Yeye hana kukata viungo kokote. Hapana, mwili Wake ni mkamilifu, hauhitaji kukatwa viungo vyovyote. Amina. Whew. Hiyo ni kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Kristo atakapofunuliwa, aliye uhai wetu, ndipo na ninyi mtafunuliwa pamoja naye katika utukufu. Wakolosai 3:4

24-0709

53-0405S – Nendeni, Mkawaambie Wanafunzi Wangu

Ilikuwa mapema asubuhi moja. Waliuweka mwili Wake ardhini, siku ya Sabato, ambayo ilikuwa ni desturi kwamba hawakufanya lolote siku ya Sabato. Kwa hiyo alikufa Ijumaa alasiri, saa tisa, akafufuka mapema Jumapili asubuhi.

Sasa nataka kutatua swali hili, wakati mkiwa hapa asubuhi hii katika ibada hii ya mapambazuko. Watu wengi wanasema, “Imekuwaje basi kwamba Yeye alisema ya kwamba angelala…Alikuwa kaburini, siku tatu mchana na usiku?” Kamwe hakusema angefanya hivyo.

Alisema, “Katika siku hizi tatu nitaufufua mwili Wangu.” Mnaona? Sasa, sababu ya Yeye kufanya hivyo ni kwa sababu Daudi alikuwa amesema, mahali pamoja katika Maandiko, “Sitaiacha nafsi Yake katika kuzimu, wala sitamwacha Mtakatifu Wangu aone uharibifu.” Naye alijua ya kwamba uharibifu huingia katika mwili wa mwanadamu baada ya saa sabini na mbili, siku tatu usiku na mchana. Na wakati fulani ndani ya hizo siku tatu mchana na usiku, Mungu alikuwa amfufue. Kwa hiyo alikufa Ijumaa alasiri saa tisa, na kufufuka mapema Jumapili asubuhi.

MKATE WA KILA SIKU

Maana hutakuachia kuzimu nafsi yangu, Wala hutamtoa mtakatifu wako aone uharibifu. Zaburi 16:10

24-0708

61-1119 – Uweza Mkamilifu Kwa Udhaifu Mkamilifu

Na, ndugu, kifuniko cha kuzimu kimeondolewa. Hiyo ni kweli. Na mitiririko ya nguvu za pepo inamwagika kutoka kila mahali. Imeyashinda mataifa. Imezishinda siasa mpaka zimeoza kabisa. Imeyashinda makanisa hata hawajui kitu ila madhehebu.

Unasema, “Hivi wewe ni Mkristo?”

“Mimi ni Mmethodisti.”

“Wewe ni Mkristo?”

“Mimi—mimi ni Mpentekoste.”

Hilo halimaanishi zaidi ya kuwa nguruwe, kama nilivyosema hivi majuzi, ama nguruwe mwitu, ama farasi, ama chochote kile. Hilo halina uhusiano wowote Nalo. Wewe ni Mkristo wakati unapozaliwa mara ya pili na kujazwa na Roho Mtakatifu, si kabla ya hapo, na umejitolea kabisa kwa Roho. Kama hujajitolea kwa Roho, basi hujazaliwa mara ya pili wala huna Roho Mtakatifu.

MKATE WA KILA SIKU

Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali. Isaya 13:11

24-0707

60-0304 – Kuonea Kiu Uzima

Mara nyingi nimesema kama ningeweza kuwa kijana wa umri wa miaka ishirini na mitano, kama Mungu angetokea jukwaani usiku wa leo, na kusema, “Nitakugeuza uwe na umri wa miaka ishirini na mitano, utabaki hivyo kwa miaka milioni moja, nami nitakufanya uwe mfalme juu ya ulimwengu wote, kila kitu kitakuwa chini ya amri yako; ama nitakupa miaka mia ya taabu na ole, na shida, na huzuni, lakini mwisho wa hiyo miaka mia moja, nitakupa Uzima wa Milele, lakini mwisho wa hiyo miaka milioni moja, upotee.”

Loo, ningesema, “Bwana Mungu, sihitaji kungoja zaidi kufanya chaguo langu: Acha niwe na miaka mia ya taabu na ole, aina yo yote ya kifo utakachonichagulia nife, Bwana, nipe tu Uzima wa Milele. Kwa maana ingawa ninamiliki ulimwengu wote na nilikuwa mfalme kwa miaka milioni moja, mwisho wa hiyo miaka milioni moja, ninakuwa kiumbe wa kuzimu kwa Milele yote. Bali haidhuru hali yangu ni mbaya jinsi gani hapa, mwishoni mwa maisha yangu, kama nina Uzima wa Milele, nitaendelea kuishi katika Uwepo uliobarikiwa wa Mungu milele na milele.”

MKATE WA KILA SIKU

Yeye aipendaye nafsi yake ataiangamiza; naye aichukiaye nafsi yake katika ulimwengu huu ataisalimisha hata uzima wa milele. Yohana 12:25

24-0706

57-0901E – Waebrania, Mlango Wa Nne

Hampaswi kumhoji kitu chochote, Mungu. “Kwa kuwa hatua za mwenye haki zinaongozwa na Bwana.” Na kila jaribio linawekwa juu yako, kukuthibitisha. Na Biblia ilisema, “Yana thamani zaidi kwako kuliko dhahabu.” Kwa hiyo kama Mungu aliruhusu mateso machache mepesi yakupate, kumbuka, ni kwa ajili ya kukurudi wewe. “Kila mwana amjiaye Mungu hana budi kurudiwa na Mungu kwanza, na kujaribiwa, apate mafunzo ya mtoto.” Hakuna asiyerudiwa. “Kila mwana ajaye.” Mateso haya yanafanywa ama kusababishwa—kusababishwa, kuona utachukua msimamo gani. Unaona? Ni Mungu, kwenye mahali hapa pa kujaribia. Hiyo ni dunia nzima, ni mahali pa kujaribiwa, na mahali Yeye anapojaribu kukujaribu.

MKATE WA KILA SIKU

Pande zote twadhikika, bali hatusongwi; twaona shaka, bali hatukati tamaa; 2 Wakorintho 4:8

24-0705

62-0909E – Katika Uwepo Wake

Mwangalie maskini yule kahaba kule chini Samaria siku ile, mwanamke huyo. Alikuwa katika hali mbaya kiakili na kimwili. Tunajua jambo hilo. Lakini mara alipoiona hiyo ishara ikifanywa, ya Masihi, alisema, “Tunajua Masihi yuaja kufanya jambo hili. Huna budi kuwa ni nabii Wake.”

Akasema, “Mimi Ndimi huyo Masihi aliyeandikiwa atakuja.”

Alitambua jambo hilo. Kamwe hakuuliza swali lingine zaidi. Alianza jukumu mara moja, kujua ya kwamba kama alikuwa amepata jambo hilo na akaja katika Uwepo wa Mungu, alikuwa anawajibika kumwambia mtu mwingine kuhusu jambo hilo. Haleluya! Kweli. Mtu yeyote anayekuja katika Uwepo wa Mungu anawajibika mbele za Mungu, tangu dakika hiyo na kuendelea, kumwambia mtu mwingine. Hebu mwangalie Ibrahimu, mwangalie Musa, mwangalie Petro, mwangalie Paulo. Mara walipokuja katika Uwepo wa Mungu, walijitambua ni “wenye dhambi,” na kuutia muhuri ushuhuda wao kwa maisha yao. Hebu mwangalie maskini mama huyo, asingeweza kukaa zaidi, alienda mjini na kuwaambia wanaume, “Njoni, mwone Mtu aliyeniambia mambo ambayo nimefanya. Yamkini huyu siye yule Masihi?” Wasingeweza kukanusha jambo Hilo, kwa sababu lilikuwa ni la Kimaandiko. Hakika. Naam, hawana budi kufanya jambo hilo, mtu, wakati tukiwa na jukumu la kuwaambia wengine kama vile Musa alivyofanya, kama vile Petro alivyofanya, kama vile Paulo alivyofanya. Baada ya mambo haya, umeliona na ukaja katika Uwepo Wake, wewe unawajibika kwa Ujumbe kumfikia mtu mwingine. Kamwe huwezi tu kuketi kitako nao. Huna budi kumpelekea mtu mwingine.

MKATE WA KILA SIKU

Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. Marko 16:15

24-0704

63-1222 – Karama Za Mungu Daima Hupata Mahali Pao

Mariamu, mama wa Yesu, katika mji wa Nazareti, mji duni kuliko yote uliokuwapo nchini, bali kutoka pale Mungu alichagua mama mdogo kumzaa Mwana Wake; kiangulio, tumbo la uzazi ambalo ilibidi…ilibidi Mtoto azaliwe kwalo. Alimchukua mtu kama huyo kufanya hivyo. Mungu hufanya kazi kupitia wanadamu kuwakomboa wanadamu. Anaweza kukuchukua, afanye kazi kupitia wewe ili kukomboa wanadamu, iwapo utasalimisha kabisa kila kitu ulicho.

Kama wewe ni msichana, salimisha maadili yako. Wewe ni kijana mwanamume, salimisha maadili yako, salimisha nia yako, salimisha mawazo yako, salimisha moyo wako, salimisha nafsi yako, salimisha yote uliyo! Na umwache Kristo afanye kazi kupitia hayo. Ni jambo tukufu jinsi gani!

MKATE WA KILA SIKU

…simameni imara katika Bwana, wapenzi wangu. Wafilipi 4:1

24-0703

60-0626 – Kweli Zisizoshindwa Za Mungu Aliye Hai

Yesu alimleta Mungu kwa maisha ya wanadamu. Mungu alifanyika mwanadamu. Wakati Yesu alipozaliwa, Mungu alifanyika mwanadamu, ili aweze kushirikiana na mwanadamu na katika mwanadamu, kufikia (nini?) kutimiza kusudi moja, ambalo ni, kumletea mwanadamu kile Mungu alicho; sio kile kanisa lilicho, lakini kile Mungu alicho. Yesu alikuja apate kumwasilisha Mungu kwa mwanadamu. Wala mwanadamu hakutaka.

Roho Mtakatifu huja siku hizi, vivyo hivyo, kuwasilisha Mungu kwa mwanadamu; lakini mwanadamu anataka kwenda kanisani. I—i—inanyamazisha mawazo ya—ya—yake. Hawezi—hawezi kuelewa Hilo. Nasi hatuna budi kujua kwamba Mungu hajulikani kwa dhana za kiakili. Mungu anajulikana kwa Kuzaliwa upya, na Roho Mtakatifu, si kwa njia nyingine yoyote. Yesu, Biblia imenukuu wazi kwamba, “Hakuna mtu anayeweza kumwita Yesu Kristo, isipokuwa kwa Roho Mtakatifu.” Na ikiwa hujawahi kumpokea Roho Mtakatifu, hujui kwamba Yeye ndiye Kristo, kwa kuwa hiyo ndiyo njia pekee anayojifunulia.

MKATE WA KILA SIKU

Mungu amemtuma Mwanawe pekee ulimwenguni, ili tupate uzima kwa yeye. 1 Yohana 4:9

24-0701

65-1125 – Muungano Usioonekana Wa Bibi-Arusi Wa Kristo

Mungu mpendwa, tumeketi kwa kicho sasa, kweli hii ni siku ya kutoa shukrani, Bwana. Ninashukuru, Bwana, kwamba ninaishi katika siku hii. Hii ndiyo siku iliyo kuu sana. Mtume Paulo alitamani kuiona siku hii. Wale watu mashuhuri wa zamani walitamani kuiona. Manabii walitamani kuiona. Waliitazamia siku hii. Ibrahimu aliitazamia siku hii, kwa kuwa aliutafuta Mji ambao Mwenye Kuujenga na Mwenye Kuubuni alikuwa ni Mungu; unaning’inia moja kwa moja juu yetu, usiku wa leo. Yohana aliona Roho wa Mungu akishuka kutoka Mbinguni, alishuhudia, alijua ya kwamba huyo alikuwa ni Mwana wa Mungu. Na, wazia sasa, Yeye anamchagua Bibi-arusi Wake.

Mungu mpendwa, kote huko nje nchini, nena na moyo wao. Wewe ndiwe tu unayeweza kuubadilisha moyo wao. Kama hiyo haikuwa ni Mbegu iliyowekwa humo ndani hapo mwanzo, kamwe hawataliona, Bwana. Wao ni ninii tu…“Kipofu atamwongoza kipofu mwenziwe. Wataanguka shimoni,” hakika kabisa, kwa kuwa Neno Lako linasema wataanguka.

MKATE WA KILA SIKU

Ingieni malangoni mwake kwa kushukuru; Nyuani mwake kwa kusifu; Mshukuruni, lihimidini jina lake. Zaburi 100:4

24-0630

59-0412E – Unasikia Nini, Eliya?

Mara zote si mambo yenye kelele yaliyo mambo makuu. Sio mambo yenye kelele. Gari la mizigo laweza kwenda shambani; linapopakuliwa litadunda, na kunguruma, na kutoa kelele nyingi, linaweza kurudi moja kwa moja juu ya matuta yale yale likiwa limesheheni vitu vizuri, na hata halitatoa mlio. Kwa nini? Limepakiwa. Kile kanisa linachohitaji usiku wa leo ni kupakiwa, kujazwa na upendo wa Mungu.

Jua linaweza kuvuta galoni milioni za maji kwa kelele kidogo kuliko tunavyoweza kusukuma glasi iliyojaa kutoka kwenye pampu. Hiyo ni kweli. M—mbingu zinaweza kunyunyiza umande duniani kote kwa kelele kidogo kuliko unavyoweza kunyunyizia nyasi zako za upande wa mbele. Hakika. Je, umewahi kusikia sayari zikizunguka? Mambo makuu ni mambo ya kimya kimya.

Mwangalie Roho Mtakatifu anapoingia usiku wa leo, jinsi Anavyopata kila kitu kwa ukimya. Lakini sisi tunaendea misisimko, tukikimbilia mambo madogo, tukishindwa kuisikia Sauti hiyo.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini BWANA yumo ndani ya hekalu lake takatifu; dunia yote na inyamaze kimya mbele zake. Habakuki 2:20

24-0629

57-0407M – Mungu Hutimiza Neno Lake

Imani yangu imetulia juu ya Mwamba huo imara. Hakuna kitu kinachoweza kudhuru wakati umetia nanga kwenye Mahali hapo. Dhoruba zinaweza kutikisa na kuipiga, lakini nanga yangu inashikilia ndani ya pazia. Wakati mwanamume au mwanamke ametia nanga na kuikubali. Hakuna kitu kinachoweza kukuyumbisha kutoka kwayo.

Kama vile wakati wao ulivyokuwa wa ukombozi, nao wakakosa kuuona, ndivyo ulivyo wakati wa ukombozi, amri za kuondoka kwa Kanisa. Umekaribia.

Angalia, rafiki yangu. Walikuwa na nini? Kwanza, Neno. Pili, nabii. Tatu, Malaika wa kuwaongoza, awaongoze. Kila mmoja alikubaliana na mwenzake; hao watatu. Neno lilikubaliana na nabii; naye nabii akakubaliana na Neno; Malaika alikubaliana na wote watatu, wote. Neno; nabii; Malaika! Walikuwa tayari kwa safari.

Loo, Jina la Bwana Mungu libarikiwe! Tuko kwenye wakati wa mwisho; Neno, nabii, na Malaika, wote watatu pamoja, ushuhuda mmoja mkuu. Mungu alisema kila wakati, “Kwa vinywa vya mashahidi wawili au watatu, kila neno na lithibitike.” Naye nabii wa kweli daima atakubaliana na Neno; na Malaika yeyote atashuhudia Kweli. Amina. Tuko tayari kwa maagizo ya kuondoka. Hakika.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini Yeye aonywaye, ataiokoa roho yake. Ezekieli 33:5

24-0627

62-0610E – Kushawishika Kisha Kuhusika

Nimeshawishika kwamba Yeye ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Nimeshawishika, katika hii huduma na huu Ujumbe, ninaohubiri, nimeshawishika kwamba ni Kweli. Nimeshawishika ya kwamba maono haya yanatoka kwa Mungu. Nimeshawishika tunaishi katika siku za mwisho. Nimeshawishika ya kwamba Roho yuyu huyu aliye juu yangu ni Roho Mtakatifu. Utukufu!

Nimeshawishika kabisa. Nimeshawishika kwamba njia ya Roho Mtakatifu ni ya kweli. Nimeshawishika ya kwamba njia ya Biblia ni ya Kweli. Nimeshawishika ya kwamba Huyu ni Yesu Kristo hapa sasa. Nimeshawishika. Kama tukimwamini dakika hii, nimeshawishika kwamba Yeye angeponya kila mtu mgonjwa katika dakika moja, kufumba na kufumbua jicho. Nimeshawishika Yeye angemwaga Roho Mtakatifu juu ya mahali hapa, mpaka kungekuwako na kelele kubwa mno, hata ingekuwa ni vigumu kujua yale yangetukia.

Nimeshawishika. Ninaliamini kwa moyo wangu wote…

MKATE WA KILA SIKU

Yeye tu ndiye mwamba wangu na wokovu wangu, Ngome yangu, sitatikisika sana.          Zaburi 62:6

24-0626

58-0609 – Ujumbe kwa Kanisa la Laodikia

Nami kwa kweli ninawazia jambo hili, ya kwamba mara nyingi kanisa katika ulegevu wake huanza kufanya mambo, na kuwaza mambo, na—na kuchukua mambo jinsi tu yalivyo, wakati inatupasa kupima kile tunachofanya na kusema. Tunapaswa kulitafakari kabla ya kulizungumza.

Mama yangu mzee wa kusini alizoea kuniambia, “Fikiria mara mbili na uzungumze mara moja.” Ni mambo madogo, wakati mwingine, ambayo tunaacha bila kufanywa, ambayo yana maana sana kwetu. Tunakuwa na haraka sana ya kushindana na mambo katika wakati huu wa msongo tunaoishi. Ingetupasa sisi, kama kanisa la Mungu usiku wa leo, kusimama na kungoja kidogo, tuone tulipo.

MKATE WA KILA SIKU

Basi, jiangalieni, mioyo yenu isije ikalemewa na ulafi, na ulevi, na masumbufu ya maisha haya; siku ile ikawajia ghafula, kama mtego unasavyo Luka 21:34

24-0625

62-0622B – Kutoa Presha

Wazia jambo hilo, Mungu, katika Siku ya Pentekoste, ile Nguzo ya Moto ilitengana na Ndimi za Moto zikatua juu ya kila mmoja wao, Mungu akijitenga Mwenyewe, akijigawanya Mwenyewe, miongoni mwa watu Wake. Tunakuwa Uzima wa Mungu Mwenyewe ndani yetu, kisha tumekufa kwa mambo ya ulimwengu, na tumefufuka pamoja na Kristo na tumeketi katika ulimwengu wa Roho, tukitazama nyuma tulikotoka.

Inatosha kwamba tungeweza kuliwazia jambo hilo, nalo linaondoa presha, linaondoa presha, tunapotambua nafasi ambayo sasa tunashikilia katika Kristo kwa kupokea Roho Mtakatifu, Uhai wa Mungu Mwenyewe, neno la Kiyunani, Zoe, ambalo linamaanisha Uzima wa Mungu Mwenyewe, ukikaa ndani yako nawe huwezi kufa kama vile Mungu asivyoweza kufa. Sisi ni wa Milele pamoja na wa Milele, amina, tukingojea ule wakati mtukufu wa kukombolewa kwa mwili.

Na sasa tumekufa tayari, nayo maisha yetu yamefichwa ndani ya Mungu kupitia Kristo na kutiwa muhuri na Roho Mtakatifu. Ibilisi yuko nje ya picha kabisa.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini Mungu na ashukuriwe atupaye kushinda kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 1 Wakorintho 15:57

24-0624

53-0906A – Unayasadiki Hayo?

Mungu atanena, na hakuna kitu kinachoweza kuliondoa Neno la Mungu. Neno la Mungu linadumu milele. Mungu anapolinena, limethibitishwa mbinguni milele. Liko papo hapo tayari, Kama vile tu limekwisha tendeka, wakati Mungu anapolinena.

Loo, ili sisi tupatikanao na mauti tuweze kusema, “BWANA ASEMA HIVI; imekwisha,” kumchukua Mungu kwenye Neno Lake na kusimama hapo haidhuru kitu gani kitakachokuja, ni njia ngapi zinazosukuma kando. Tunakaa moja kwa moja na Neno la Mungu. “Mungu alisema hivyo. Ninaliamini. Hilo latosha.” Amina.

MKATE WA KILA SIKU

Jumla ya neno lako ni kweli, Na kila hukumu ya haki yako ni ya milele. Zaburi 119:160

24-0623

54-0719E – Mungu Akitoa Uponyaji Kwa Kizazi Hiki

Udongo unapaswa kupokea ngano ili kuzaa uhai. Nawe huna budi kulipokea Neno la Mungu moyoni mwako ili kuzaa kile ambacho Neno linasema kitakuwa. Kila Neno la Mungu ni Mbegu. Yesu alisema lilikuwa. Mpanzi alitoka akipanda mbegu; Alisema mbegu ni Neno la Mungu.

Na sasa angalia, hindi litazaa hindi, ngano ngano, shayiri shayiri. Vyovyote itakavyokuwa, itazaa. Na kama Neno la Mungu ni Mbegu, kama Yesu alivyosema lilikuwa, na limewekwa ndani ya moyo wa mwanadamu, na pale, likitiwa maji kwa imani, litazaa chochote ambacho Mungu alisema katika Neno Lake kwamba lingefanya. Litazaa. Kama unahitaji wokovu, “Njooni Kwangu ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nitawapumzisha.” Kama unahitaji uponyaji, “Alijeruhiwa kwa makosa yako, na kwa kupigwa kwake umeponywa.” Mungu ametoa dhabihu kwa ajili ya dhambi na magonjwa. Na wasiwasi, na shida, na huzuni, na mambo haya yote, Mungu ametoa Dhabihu. Yeye yuko hapa usiku wa leo.

MKATE WA KILA SIKU

Naye aliyepandwa penye udongo mzuri, huyo ndiye alisikiaye lile neno, na kuelewa nalo; yeye ndiye azaaye matunda, huyu mia, na huyu sitini, na huyu thelathini. Mfano wa Magugu katikati ya Ngano Mathayo 13:23

24-0622

47-0412 – Imani Ni Kuwa Na Hakika

Na watu huniambia wana imani na kusema hawawezi kuamini katika uponyaji wa Kiungu? Enyi marafiki, kama huamini katika uponyaji wa Kiungu, umepotea. Hiyo ni kweli. Utafanyaje, kama huwezi kuwa na imani ya kutosha kwa Mungu kuuweka kiraka mwili huu ili kumtukuza ndani yake, ni jinsi gani utakuwa na imani zaidi ya kuamini ya kwamba Mungu atauchukua huu wa kale upatikanao na mauti kuufanya usiopatikana na mauti kutoka kwake kuutwaa juu? Huo ni uponyaji wa Kiungu wa moja kwa moja. Loo, jamani, kutakuwa na mambo ya kutisha ya kukatisha tamaa katika siku ya hukumu, kwenye ufufuo. Hiyo ni kweli.

MKATE WA KILA SIKU

Ila na aombe kwa imani, pasipo shaka yo yote; maana mwenye shaka ni kama wimbi la bahari lililochukuliwa na upepo, na kupeperushwa huku na huku. Yakobo 1:6

24-0621

63-0714M – Mbona Unalialia? Nena!

Imani hailioni hili hapa. Imani hutazama kuona yale Mungu anayotaka, na kutenda kulingana na hayo. Hivyo ndivyo imani ifanyavyo. Inaona mahitaji ya Mungu, na yale Mungu anayotaka na imani hutenda kazi kupitia hayo.

Imani ni uonaji wa mbali. Haifupishi upeo wake. Hushikilia ionacho. Amina! Mpiga bunduki mzuri ye yote ajua hayo, Waona? Hiyo hulenga mbali; ni darubini kubwa, ni darubini ya macho ambayo haioni humu karibu; hutumii darubini ya macho kutazama ni saa ngapi. Waona? Huitumii hiyo, bali hutumia darubini ya macho kutazama mbali kabisa, nayo imani hufanya hivyo. Imani huitwaa darubini ya macho ya Mungu, zote mbili, pande zote mbili, Agano Jipya na Agano la Kale na kuona kila ahadi aliyoifanya, nayo imani huiona kule ng’ambo. Na imani huchagua hiyo, bila kujali wakati uliopo usemavyo hapa. Yeye hutazama kule mwisho.

Yeye hashushi darubini yake na kutazama upande huu; hutazama kule ng’ambo. Yeye huweka kipini cha kulengea shabaha katikati ya Neno kabisa. Hivyo ndivyo imani ifanyavyo.

MKATE WA KILA SIKU

Maana twaenenda kwa imani, si kwa kuona: 2 Wakorintho 5:7

24-0620

64-0206E – Njia Iliyowekwa Na Mungu Kwa Ajili Ya Siku Hii

Mmea wa haibridi, inakubidi kuubembeleza na kuupiga dawa, na kuwafukuza wadudu na mende watoke kwake. Bali huo si mmea halisi wenye afya; wenyewe ni imara, una nguvu, wala hakuna wadudu wowote wanaouvamia. Una ya kutosha ndani yake kumfukuza mdudu toka kwake.

Na ndivyo ilivyo na Mkristo halisi! Haikubidi kumbembeleza na kumdekeza, na kumwambia hivi, vile, ama vinginevyo. Ana kitu ndani yake, ubatizo wa Roho Mtakatifu, ambao hutupilia mbali mengine yote. Haikulazimu kumsihisihi, kwa kuwa yeye ni mmea halisi wa Mungu. Ana kitu ndani yake kinachopigana vita. Mkristo hupigania sehemu yote ya nchi anayosimama. Inampasa kufanya hivyo, kama anatarajia kuishi. Na, kwa kufanya jambo hilo, kuna kitu Fulani ndani yake kinachomlinda.

Hawa alijaribu kuhaibridi Neno, hapo mwanzo. Mungu alimwambia, “Siku utakayokula, siku hiyo utakufa.” Alijaribu kulizalisha na maarifa aliyopewa na Shetani. Na alipofanya hivyo, akapoteza jamii nzima ya binadamu, pale pale, kwa ibilisi, alipojaribu kuchanganya Neno la Mungu lisiloghoshiwa na maarifa. Halitolewi na maarifa ya Neno.

Linatolewa na nguvu za Roho Mtakatifu!

MKATE WA KILA SIKU

Si kwa uwezo, wala si kwa nguvu, bali ni kwa roho yangu, asema BWANA wa majeshi. Zekaria 4:6

24-0619

61-0216 – Alama Ya Mnyama Na Muhuri Wa Mungu #1

Habili alifia juu ya mwamba uleule pamoja na mwana-kondoo wake. Kila mwamini hana budi kufanya jambo lile lile, kufa juu ya mwamba pamoja na Mwana-Kondoo wako.

Mwana-kondoo hana ila kitu kimoja tu, nacho ni Manyoya, naye hana budi kupoteza vyote alivyo navyo, haanzishi ubishi kuhusu hilo. Umchukue maskini jamaa huyo na kumtupa juu kule, ni kama ilivyosemwa, mwana-kondoo unyamaza mbele ya wamkatao manyoya yake. Yeye hukatwa manyoya, yeye habishanii hilo. Kitu pekee alicho nacho, anakipoteza, kwa utashi.

Nasi tunasema sisi ni Wakristo. Mtu fulani aliniandikia barua ndogo hivi majuzi, na, noti ndogo, naye akaiweka ndani, nami nikaipata pale chini, kasema, “Nina haki, mimi ni raia wa Marekani, ninavaa nguo za aina yoyote ninazotaka.”

Wewe endelea tu, ni sawa, hiyo inaonyesha wewe ni mbuzi. Hiyo ni kweli. Wewe endelea tu na uzivae kama unataka. Lakini kumbuka, kama wewe ni mwana-kondoo, unayo haki kwa. Jambo hilo, bali unazipoteza haki zako kwa ajili ya Kristo.

Nina haki ya kulewa usiku wa leo, pia, mimi ni raia wa Marekani; Nina haki ya kuvuta sigara, mimi ni raia wa Marekani, unayo pia, lakini tunapoteza haki zetu, tunanyolewa kutoka katika mambo hayo. Tendeni kama waungwana, kama mabibi, vaa hivyo, na utende hivyo, na uishi hivyo, poteza haki zako.

MKATE WA KILA SIKU

Basi, ndugu zangu, nawasihi, kwa huruma zake Mungu, itoeni miili yenu iwe dhabihu iliyo hai, takatifu, ya kumpendeza Mungu, ndiyo ibada yenu yenye maana. Warumi 12:1

24-0618

58-0928E – Uzao Wa Nyoka

Ni nani aliye na nguvu zaidi ya wote, nimesema, Mwokozi ama mwenye dhambi? Ni nani aliye na nguvu nyingi kupita wote? Basi, ilimbidi aliye na nguvu zaidi amruhusu asiye na nguvu sana, Naye hufanya jambo hilo tu kwa ajili ya utukufu Wake. Alipomfanya Lusifa, Yeye alijua angekuwa ibilisi. Ilimbidi kumwacha aweko kuonyesha ya kwamba Yeye alikuwa Mwokozi, yule Kristo. Ilimbidi kuacha jambo hilo litukie namna hiyo.

Naam, hivi Biblia haisemi, ya kwamba, “Mambo yote hutendeka kwa manufaa ya hao wampendao Mungu”? [Kusanyiko, “Amina.”—Mh.] Basi mnaogopa nini?

Na tuamke tukatende kazi,

Tujitie moyo katika mzozo wo wote.

Msiwe kama ng’ombe bubu wanaosukumwa, hawana budi waombwe na kubembelezwa!

Na mwe shujaa!

Ninapenda hilo. Simameni!

MKATE WA KILA SIKU

Nasi twajua ya kuwa katika mambo yote Mungu hufanya kazi pamoja na wale wampendao katika kuwapatia mema, yaani, wale walioitwa kwa kusudi lake. Warumi 8:28

24-0617

56-1209A – Mungu Akifanya Ahadi Yake

Na kwa hivyo, inatubidi sisi kama waamini, kwa kweli kutoyaendea mawazo fulani ya kiakili au juu ya hisi fulani, au jambo fulani la ajabu lililotokea: “Tulifanya hili au tulifanya lile.” Kwa maana shetani anaweza kuiga mambo hayo yote. Lakini njia pekee ambayo tutajua kwamba tumeokolewa ni wakati tumetimiza masharti ya Mungu. Unaona, unaona? Huokolewi kamwe kwa hisi zako; umeokolewa kwa imani yako. Unaona? Daima Unaokolewa kwa imani. Imani yako inalifanya hilo halafu maisha yako yanathibitisha ikiwa ulilipokea au la.

Sasa, kama unajaribu tu kuliiga, basi una—unafanya tu—unajifanya tu—mnafiki wewe mwenyewe. Unaona? Maana wewe—huwezi kufanya hivyo. Ukristo ni jambo linalopaswa kutoka moyoni.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini mwenye haki wangu ataishi kwa imani; Naye akisita-sita, roho yangu haina furaha naye. Waebrania 10:38

24-0616

55-1003 – Imani Kazini

Nguzo ile ile ya Moto iliyowaongoza wana wa Israeli nyikani, Malaika yule yule wa Mungu aliyekuja kwenye—mahali pale na kumkomboa Petro kutoka kizimbani, Bwana Yesu yeye yule aliyesimama mbele ya Paulo na kutuma ile nuru inayong’aa iliyompofusha macho yake. Na wanaume waliokuwa karibu naye hawakuweza kuona nuru yoyote. Lakini Paulo; ilimpofusha macho. Naye alikuwa kipofu naye ilimbidi aongozwe kwa mikono hadi mjini, nuru ilikuwa inawaka kwa nguvu sana kumzunguka. Nuru iyo hiyo, Bwana Yesu Kristo yuko hapa usiku wa leo katika Utu wa kufufuka Kwake na akijithibitisha Mwenyewe kwa ishara na maajabu yasiyoweza kukosea ya kwamba Yeye yuko hapa.

Enyi watu, wekeni imani yenu kazini. Msiwe na hofu. Mbona, aibu kwenu; msiogope. Simama imara katika uhuru ambao Kristo amekuweka huru. Usijitie mwenyewe ndani ya kizimba cha ndege tena. Njoo toka humo. Zivunje kuta. Kristo alivunjilia mbali viambaza vya katikati vinavyotenganisha, akatuweka huru. Tuko tayari kuruka zetu. Amina. Nalipenda hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Sitawaacha ninyi yatima; naja kwenu. Yohana 14:18

24-0615

60-1204E – Ono La Patimo

Si ni vizuri sana wakati unapoweza kweli kuitia nanga nafsi yako katika Kristo, kufikia mahali ambapo unaweza kutulia mbele Zake? Na kusikia Sauti Yake ikisema nawe, “Mimi ndimi Bwana nikuponyaye. Mimi ndimi Bwana nikupaye Uzima wa Milele. Ninakupenda. Nilikujua kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Niliandika jina lako kwenye Kitabu, wewe ni Wangu. Usiogope, ni Mimi. Usiogope, niko pamoja nawe.” Ndipo ninaimba:

Nimetia nanga nafsi yangu katika mahali pa raha,

Sitaabiri bahari zenye tufani tena;

Huenda tufani ikakipiga kilindi cha bahari yenye dhoruba;

Lakini katika Yesu mimi ni salama milele.

Kumbukeni, Sauti ile ile inayokuzungumzia kwa utamu, itamhukumu mwenye dhambi. Gharika ile ile iliyomwokoa Nuhu, ilimwangamiza mwenye dhambi. Mnaona ninalomaanisha?

MKATE WA KILA SIKU

Tuliyo nayo kama nanga ya roho, yenye salama, yenye nguvu,… Waebrania 6:19

24-0614

55-0223 – Ayubu

Kuna habari za kukaribisha kwako usiku wa leo. Wakati Mungu, akijivua Mwenyewe, akitoka katika majumba ya kifalme, akijitwalia yeye mwenyewe umbo la mwili wenye dhambi, kujinyenyekeza ili ashuke, kuwa Jamaa wa karibu wa maskini ombaomba aliyeko ulimwenguni usiku wa leo, apate kuwa Jamaa yake. Yehova Mwenyewe, alijifanya wa jamaa aliye wa karibu kwa ombaomba. “Mbweha wana mapango, na ndege wana viota, lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kulaza kichwa chake.” Amezaliwa horini, amevikwa nguo za kitoto, hata hivyo ndiye Mkuu wa Utukufu, Mapambazuko kutoka juu. Akijinyenyekeza, kujishusha mwenyewe, akishuka, kuja kufanywa Jamaa wa karibu wa mwenye dhambi. Wazieni hilo, enyi watu. Unawezaje kukataa upendo huo usio na kifani?

Ilikuwa ni kitu gani? Wakati Mungu alipofanyika mwenye dhambi, kuzichukua dhambi zetu. Yesu alifanyika mimi, ili mimi nipate kuwa Yeye. Mwana-Kondoo wa Mungu asiye na hatia, Asiyejua dhambi, alifanyika mwenye dhambi, ili mimi nifanywe mwana wa Mungu.

MKATE WA KILA SIKU

Alikuwako ulimwenguni, hata kwa yeye ulimwengu ulipata kuwako, wala ulimwengu haukumtambua. Yohana 1:10

24-0613

63-1216 – Tumeiona Nyota Yake Na Tumekuja Kumsujudia

Pia wakati mwingine tunafikiria kwamba, mizigo yetu. Huenda nikaingiza hii papa hapa, kwamba, tunafikiria mizigo yetu ni mizito sana wakati mwingine, kwamba hakuna kitu kama huo ulimwenguni. Je! unajua kwamba mambo hayo yote ni mazuri kwako? Yote ni ya kukufinyanga wewe, kukuumba wewe. Manabii na wenye hekima walifinyangwa upande wa nyuma ya jangwa, kwenye jua kali, linalowaka, kupitia dhiki na majaribu, na mateso. Na mambo haya tuliyo nayo leo hii, hakuna kitu kilichotendeka kwetu ambacho hakijawahi kuwatendekea Wakristo wengine, hapo kabla. Wakristo wengine imewabidi kustahimili katika wakati wa giza kama huu, na hata kulishwa simba, kwa ajili ya ushuhuda wao.

MKATE WA KILA SIKU

Ili kwamba kujaribiwa kwa imani yenu, ambayo ina thamani kuu kuliko dhahabu ipoteayo, ijapokuwa hiyo hujaribiwa kwa moto, kuonekane kuwa kwenye sifa na utukufu na heshima, katika kufunuliwa kwake Yesu Kristo. 1 Petro 1:7

24-0612

62-0621E – Thibitisho Na Ushahidi

Kumbukeni, ya kwamba haitupasi kamwe kuja kanisani kuigiza dini. Haitupasi kuja, kuninii tu, kujivalisha tendo la kidini tupate kwenda kanisani, hatuna budi kuja kuabudu katika Roho na katika kweli, hatuna budi kuwa waaminifu sana, lazima kweli tumaanishe kile kilichotuleta hapa. Siku zinazidi kuwa ovu, wakati ni mwovu, nasi tunataka—tunataka kutumia kila dakika, na hasa sana tunapokuwa katika nyumba ya Bwana.

MKATE WA KILA SIKU

Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake. Mathayo 4:10

24-0610

62-0117 – Kudhania

Mtu fulani alisema, “Hebu achia akili yako iwe tupu tu sasa. Angalia tu moja kwa moja juu angani. Achia akili yako iwe tupu. Utapata tukio.” Na hapana shaka utapata. Hiyo ni kweli. Lakini, unapata tukio, ila ni tukio gani? Unaona, unapofanya jambo hilo, unamfungulia tu Shetani nafsi yako. Atakupa kitu fulani. Hiyo ni kweli.

Lakini, nafikiri, mtu anapomjia Kristo anapaswa kuja na akili yake yote waliyo nayo, na wakinukuu niani mwao, wanapomjia Yeye, kila ahadi katika Maandiko. Weka akili yako macho, unapomjia Kristo. Usiache iwe tupu. Ibilisi atakufanya ufanye jambo lolote. Unaona? Watakupa mhemuko. Anaweza kufanya hivyo, pia. Lakini unataka tukio, jambo ambalo Biblia inafundisha, jambo ambalo ni halisi.

MKATE WA KILA SIKU

…kwa maana namjua yeye niliyemwamini, na kusadiki ya kwamba aweza kukilinda kile nilichokiweka amana kwake hata siku ile. 2 Timotheo 1:12

24-0609

55-0312 – Muhuri Wa Kristo

Watu wengine huja kanisani kwa ajili ya sehemu ya kihisia tu. Watu wengine huja kanisani ili kuimba tu. Baadhi ya watu huja kanisani kufurahia tu uimbaji mzuri, hiyo ni sawa. Baadhi ya watu huja kanisani, na kujiunga na kanisa ili tu kuficha ubaya wao, kujitengenezea jina bora zaidi katika ujirani. Wengine huja kanisani kwa uaminifu, lakini hawana mguso wowote kutoka kwa Mungu. Lakini Mungu anapomwita mtu, “Hakuna mtu awezaye kuja Kwangu asipovutwa na Baba Yangu kwanza. Na kila ajaye nitampa Uzima wa milele, nitamfufua siku ya mwisho.”

Loo, natumai unaliona. Ndugu, ni kazi ya Roho Mtakatifu kumfunulia mtu huyo binafsi, si kwa hisia fulani, si juu ya jambo fulani unalopaswa kufanya, ama usilopaswa kufanya, ama hili, lile, ama linginelo. Mambo hayo yote ni sawa, mienendo na vitendo, na kupiga kelele na kucheza, na kunena kwa lugha; mambo hayo yote ni sawa. Lakini jambo la kwanza, haina budi kuwa ufunuo wa kiroho ambao Mungu amempa mtu binafsi, ya kwamba Yesu Kristo ni Mwana wa Mungu, anayeita. Hiyo ni kweli. Bila hivyo, ndugu, unaiga tu, unajifanya tu.

MKATE WA KILA SIKU

Yeye aliye wa Mungu huyasikia maneno ya Mungu. Yohana 8:47

24-0608

 63-0803E – Ushawishi

Vema, yule Malaika alipokutana na Mariamu asubuhi hiyo akielekea kisimani, na akamwambia angepata “mtoto, bila kumjua mwanamume ye yote,” ilimfanya aanze kutenda kazi. Akaondoka haraka, akimwambia kila mtu ya kwamba yeye angepata “mtoto, bila kumjua mwanamume ye yote.” Hakujali ingemaanishaje kwa yale watu waliyosema. Yeye hakika aliisha kukutana na Malaika wa Mungu, na hiyo ikamfanya aanze kutenda kazi. Yeye alikuwa anajua ya kwamba Roho Mtakatifu alikuwa juu yake, akiumba uhai ndani yake.

Lo, laiti tungalifahamu hivyo, kwamba, Roho Mtakatifu huyo yuko juu yetu, akiumba imani ndani yetu, akijaribu kujionyesha Mwenyewe katika njia nyingi mbali mbali pamoja na vipawa, kuumba imani ya kunyakuliwa kwa Kanisa. Inapaswa kutufanya kuanza kutenda kazi.

MKATE WA KILA SIKU

Lakini iweni watendaji wa neno, wala si wasikiaji tu, hali mkijidanganya nafsi zenu. Yakobo 1:22

24-0607

24-0606

 59-0125 – Uwe Na Hakika Na Mungu

Huko Ujerumani siku moja naliona picha, na daima ilidumu mawazoni mwangu. Mchoraji Mjerumani amechora ile—picha ambayo ambayo inaitwa “Nchi ya Mawingu.” Na unapoiangalia ukiwa mbali, ni utusitusi wa kuchukiza sana uliopata kuona, mfungamano tu wa mawingu unapoyaangalia kutoka mbali. Bali unapoyakaribia sana, yanabadilika; ni mabawa ya malaika yanayopigapiga pamoja, wakimwimbia Bwana haleluya. Kwa hivyo hivyo ndivyo utusitusi ulivyo wakati mwingine. Ukiiangalia toka mbali, inaonekana yenye utusitusi na giza; bali mchukue Mungu kwa Neno Lake na uhakikishe ya kwamba Yeye ni Mungu, nawe usonge mbele karibu nalo; utapata ya kwamba ni mabawa ya malaika yakipigapiga pamoja.

MKATE WA KILA SIKU

Maana Wewe umekuwa msaada wangu, Na uvulini mwa mbawa zako nitashangilia. Zaburi 63:7

24-0605

 62-0408 – Kudhania

Usidhanie, kaa na Neno. Usikubali jambo lo lote tofauti, kaa moja kwa moja na Lile Mungu alilosema ukae nalo, kaa na Neno. Amina.

Mungu anao wajibu, Mungu anawajibika kwa Neno lake, na Neno likiwa ndani yako, Yeye anawajibika kwako wewe kwa Neno lake. Lakini unapofanya kama Hawa, kushuku chembe moja Yake na kuingiza kitu fulani badala yake, uko nje, papo hapo. Kaa na Neno. Hebu tusidhanie chochote, hebu na tuchukue tu Kile Neno linachosema na kuliamini. Je, utafanya hivyo?

MKATE WA KILA SIKU

Kesheni, simameni imara katika Imani, fanyeni kiume, mkawe hodari. 1 Wakorintho 16:13

24-0604

  61-1224 – Mabwana, Sisi Tunataka Kumwona Yesu

Ujumbe wangu wa Krismasi, ni, hebu niwaelekeze usiku wa leo kwenye msalaba. Amina. Nanyi, enyi punje ya ngano, angukeni ndani ya Kristo kule mpate kufa. Humo mtapata Uzima Wake katika Neno Lake, akiwa ni yeye yule jana, leo, na hata milele. Acha huo uwe ndio Ujumbe wangu wa Krismasi kwenu. Siwaelekezi horini, kwenye kitanda kidogo, kwenye kanisa, kwenye dhehebu. Lakini, “mabwana, sisi tunataka kumwona Yesu,” ndipo nitawaelekeza Kwake. Yeye anawaelekeza kwenye mauti Yake, kuzikwa na kufufuka. Nanyi muache punje yenu ya ngano ianguke mle ndani, na mliache Neno Lake liwe halisi ndani yenu, nanyi mtaona ya kwamba Yeye ni yule yule jana, leo, na hata milele. “Mabwana, sisi tunataka kumwona Yesu.” Ni yeye yule jana, leo, na hata milele.

MKATE WA KILA SIKU

Yesu Kristo ni yeye yule, jana na leo na hata milele. Waebrani 13:8

24-0603

58-0406S – Najua Mkombozi Wangu Yu Hai

Ni kusudi la Mungu kutupa Roho Mtakatifu aliyebarikiwa. Ni kusudi la Mungu kutuonyesha ishara na maajabu na miujiza. Ni kusudi la Mungu, na hakuna kinachoweza kuliharibu. Nguvu zote za kuzimu zinaweza kupigana nayo, lakini itashinda. Tuna ahadi ya Milele ya Mungu. Kunaweza kuwa na walimu, kunaweza kuwa na itikadi kuinuka, kunaweza kuwa na mipango mikubwa kuinuka, kunaweza kuwa na mambo ambayo yanaonekana kama kwamba ingeharibiwa, lakini haiwezi kuharibiwa kamwe. Ni kusudi la Mungu kuona kwamba itashinda. Kisha, sio juu yangu, na sio juu yako, ikiwa itaharibiwa au la. Ni juu ya Mungu. Nasi tunaweza kuwa na uhakika juu yake, ya kwamba Mungu hataacha urithi wetu uharibiwe, kwa maana ni kusudi Lake kutupa sisi.

MKATE WA KILA SIKU

Ndiye BWANA; na afanye alionalo kuwa ni jema. 1 Samweli 3:18

24-0602

63-0120E – Mara Nyingine Moja Tu, Bwana

Mungu aliliinua kanisa lipate kuwa ni mnara wa taa, kuziachilia nguvu Zake, kuwaponya wagonjwa, kuwafufua wafu, kuwatoa pepo, kuishi kitakatifu, kuihubiri Injili yote, kuidhihirisha, bali tunaanza kujipenyeza ndani na kushusha viwango.

Tulichukua mifano mibaya. Wanawake walimwiga mke wa mchungaji. Yeye alimwachilia aingie wazimu, kukata nywele zake, kuvaa namna yoyote ya nguo za kizinifu, kamwe hakumkemea. Nao hao wanawake wengine wanasema, “Kama Dada Nanii anaweza kufanya hivyo, mimi pia ningeweza.” Usimfanye huyo mfano wako. Unaona? Mungu alikwambia jambo la kufanya, dumu na Hilo.

MKATE WA KILA SIKU

Maana Mungu hakutuitia uchafu, bali tuwe katika utakaso. 1 Wathesalonike 4:7

24-0601

57-0922E –  Waebrania, Mlango Wa Saba #2

Na ninyi watu mlio na hasira hizi kali za kumwaga damu, ambao daima mnamfokea mtu fulani, hamwezi kuvumilia, na mambo kama hayo. Iweni waangalifu. Una hatia kama ukisema neno (dhidi ya ndugu yako) ambalo si sahihi, lisilo jema, ukizunguka na kumharibia jina. Si lazima umchome mtu kisu mgongoni upate kumwua. Unaweza kumharibia jina na kumwua, kuua ushawishi wake. Ukimsengenya mchungaji wako hapa, useme jambo fulani baya kumhusu yeye, afadhali hata ungalimpiga risasi. Kama ulisema kitu ambacho hakikuwa ni cha kweli juu yake, vema, kitaharibu ushawishi wake kwa watu na vitu kama hivyo, nawe una hatia ya jambo hilo. Ndivyo Yesu alivyosema.

MKATE WA KILA SIKU

Askari nao wakamwuliza, wakisema, Sisi nasi tufanye nini? Akawaambia, Msidhulumu mtu, wala msishitaki kwa uongo;         Luka 3:14

24-0531

59-0813 – Kwa nini?

Ikiwa kuna dhambi maishani mwako, iondoe. Ikiwa kuna hukumu, iondoe. Ikiwa kuna shaka, iondoe. Mpaka uweze kuona kikamilifu kwamba ni mapenzi ya Mungu, ni mpango wa Mungu, nawe umejumuishwa katika hilo, kisha useme, “Ugonjwa, katika Jina la Yesu Kristo, ondoka kwangu.” Na kumbuka, unaweza usijisikie vizuri wiki nzima. Lakini mara tu uliposema neno hilo, jambo fulani lilitukia. Mungu hana budi kulitimiza Neno Lake. Ugonjwa huo unatetemeka, naye anaanza kuachia. Ataondoka ikiwa tu utaamini hilo. Usitie shaka.

Kama Petro akitembea juu ya maji, alisema, “Kwa nini uliona shaka? Lo, Enyi wa imani haba.” Kwa sababu tu alikuwa anazama, hilo halikuwa na uhusiano wowote nalo. Kristo alikuwa amemwamuru, na Neno Lake lilitosha. Hivyo ndivyo tunavyopaswa kuliwazia pia.

MKATE WA KILA SIKU

Na mlishike sana ungamo la tumaini letu, lisigeuke;… Waebrania 10:23

24-0430

An Independent Church of the WORD,