26-0322 Ndoa Na Talaka

UJUMBE: 65-0221M Ndoa Na Talaka

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Aliyechaguliwa, Mteule, na Aliyekusudiwa Kimbele:

Nakumbuka nilipokuwa kijana mdogo nikikua, nikijaribu kuchagua kanda ya kusikiliza. Nilipokuwa nikisoma majina ya jumbe daima Niliwaza, sitasikiliza Ndoa na Talaka, kwani huo hauna uhusiano wowote nami; ni kwa watu waliooa tu.

Kisha siku moja, nilipokuwa nikisikiliza Ndoa na Talaka, Baba akanipa Ufunuo wa Ujumbe huo. Upako Wake ulikuja moyoni mwangu. Yeye anazungumza nami. Ujumbe huu NI kwa ajili yangu. ANANIAMBIA Alinichagua mimi kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu. Huu ndio sherehe yangu ya arusi. Simtaki mtu mwingine ila Yeye. Mimi ni mkweli na mwaminifu Kwake, na kwa Neno Lake, na kwa Sauti Yake, PEKE YAKE. Sisi ni MMOJA.

Kwa kweli Ujumbe huu ulikuwa kwa ajili ya ndugu na dada wengi waliokuwa wameoana na sasa wamepeana talaka, na Yeye akiwaambia kile wanachopaswa kufanya; Lakini hapo kulikuwa na maana KAMILI NA KUBWA zaidi, iliyo kuu zaidi, yenye nguvu zaidi.

Kulikuwa na Mume mmoja, na Yeye alikuwa akiwaita na kuzungumza na Bibi-arusi Wake wengi, waliochaguliwa.  SAUTI YA MUNGU ILIKUWA IKIMWITA ATOKE BIBI-ARUSI MSAFI, NENO BIKIRA WAKE, ASIYEGHOSHIWA. Yule ambaye hajaguswa au kuchafuliwa na mwanamume. Yule ambaye ni mkweli na mwaminifu Kwake na kwa Neno Lake peke yake. Yule ambaye aliyeridhika kabisa Naye na Sauti Yake.

Kwa Neema na Rehema Zake, leo tunaweza kusema, bila shaka yoyote, SISI NDIYE BIBI-ARUSI NENO BIKIRA WAKE. UTUKUFU!!

Yeye alitaka kuhakikisha kuwa hakutakuwa na mambo yaliyoachwa linapokuja suala la kumwita Bibi-arusi Wake, kwa hivyo Yeye alikuja Mwenyewe na kuishi katika mwili wa mwanadamu ili kulifunua Neno Lake na kumwita Bibi-arusi Wake Kwake. Yeye alikuwa ndiye Eliezeri ambaye angemchagua Bibi-arusi Wake mwenyewe.

Ili kuhakikisha kuwa hakukuwa na njia ambayo tungechanganyikiwa ni nani aliyekuwa akituchumbia, Yeye Mwenyewe alikithibitisha chombo Chake kiteule kwa kuzungumza naye kutoka katika kisulisuli kilichokuwa kikining’inia kwenye mti. Kisha akazungumza naye waziwazi kule chini kwenye Mto Ohio mbele ya maelfu.

Yeye hata alipigwa picha pamoja naye ili kuuonyesha na kuuambia ulimwengu, NILIWAAMBIA NITARUDI TENA NA KUISHI KATIKA MWILI.  YEYE NDIYE NILIYEMCHAGUA KUISHI NDANI YAKE, KUWAITA NINYI MTOKE ILI MUWE BIBI-ARUSI WANGU. SI YEYE; NI MIMI NINAYENENA KUPITIA YEYE. NINAITUMIA SAUTI YAKE TU KUWA SAUTI YANGU KWENU. MIMI NDIYE NILIYEWAITA NA KUWAKAMILISHA ILI MUWE BIBI-ARUSI WANGU MKAMILIFU.

Ufunuo wa Ujumbe Huu, Neno Lake, Sauti Yake, na sasa SISI ni NANI yapita maneno ya mwanadamu kujaribu kueleza. Najua mnajua hasa kile ninachosema. Imani ya kunyakuliwa inatendeka. Bibi-arusi anajiweka Mwenyewe tayari kwa kuketi katika uwepo wa Mungu Mwenyewe, akikamilishwa.

Ni fursa iliyoje dunia iliyonayo kuisikia Sauti ya Mungu ikizungumza nao; kuketi na kulisikiliza Neno kwa Neno anaponena na kulifunua Neno Lake na kutuambia sisi ni nani. Hakuna cha kufananisha na kuketi katika uwepo Wake, kwa hivyo njooni muungane nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapomsikia Yeye akizungumza na Bibi-arusi Wake, Ujumbe, “Ndoa Na Talaka” 65-0221M.

Ndugu Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:

Mathayo Mt 5:31-32 / 16:18 / 19:1-8 / 28:19

Matendo 2:38

Warumi 9:14-23

Timotheo wa Kwanza 2:9-15

Wakorintho wa Kwanza 7:10-15 / 14:34

Waebrania 11:4

Ufunuo 10:7

Mwanzo sura ya 3

Walawi 21:7

Ayubu 14:1-2

Isaya 53

Ezekieli 44:22