UJUMBE: 64-0823E Maswali na Majibu #2
- 26-0201 Maswali na Majibu #2
- 24-0505 Maswali na Majibu #2
- 22-1009 Maswali na Majibu #2
- 18-0211 Maswali na Majibu #2
Wapendwa Wana Tai,
Palipo na Mzoga, hapo ndipo Bibi-arusi watakapokusanyika. Na kwetu sisi, kuna mahali pamoja tu pa kamilifu tunapoweza kuipata hiyo nyama mbichi ya Mana: kwa kubonyeza play na kuisikia Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Nena kuhusu Mana MPYA, Je, hivi tunaweza hata kuanza kuwazia kile tulicho nacho katika ncha ya vidole vyetu? Sauti halisi ya Mungu ikizungumza na Bibi-arusi Wake mpendwa kwenye kanda, ambapo hakuna kubahatisha, hakuna kushangaa, hakuna kuhoji wala kutilia shaka kile tunachokisikia ni Mungu, akitumia sauti ya mwanadamu, kunena Bwana Asema Hivi kwa Bibi-arusi Wake.
Kwa ufunuo, tunaamini ndipo mahali PEKEE tunapoweza kwenda na kuzipumzisha nafsi zetu kwamba Maneno tunayoyasikia si neno la mwanadamu, wala fasiri yake au wazo lake halijaongezwa Kwake, bali ni Neno safi la Mungu likizungumza nasi wana tai, akilifunua Neno Lake.
Tunashiriki kwenye Neno. Tunalisoma Neno Lake katika Biblia zetu. Hata tunawasikia watu waliyowekwa wakfu na kuitwa waliojazwa na Roho Wake Mtakatifu, wakilinukuu na kulihubiri Neno la Mungu, bali katika wakati wetu, Mungu ameandaa mahali ambapo sisi tunaweza kulisikia NENO Lake KAMILIFU LIKINENWA, kwa kubonyeza Play.
Baba hata Yeye anampa Bibi-arusi Wake fursa ya kuuliza maswali yaliyokuwa mioyoni mwetu ili tupate jibu lililo kamilifu:
- Je, Shetani anaweza kutumia karama za lugha au ya unabii katika mtu aliye na Roho Mtakatifu?
- Yesu alimaanisha nini katika Mathayo 12, mstari wa 32?
- Tafadhali fafanua Wakorintho wa Kwanza 13:8-12.
- Je, wanawake wanaruhusiwa kufanya kazi katika mahali pa umma hali wakiwa na waume wenye afya na watoto?
- Je, ni kosa kwa mwanamke kusokota nywele zake?
Mungu ameandaa njia nyingi sana za kumbariki na kumtia nguvu Bibi-arusi Wake, lakini kuna mahali pamoja tu Yeye alipopaandaa ambapo Bibi-arusi Wake wanaweza kuwa na ujasiri 100% kuwa kile wanachokisikia ni NENO LAKE KAMILIFU. Chemchemi Moja ya Maji ya Uzima ambapo Wana tai wanapoweza kunywa ambapo hakuna uwezekano wa vimelea vyovyote. BONYEZA PLAY.
Ninakualika uje kunywa kutoka kwenye Chemchemi hiyo Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(Ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) ambapo tutasikia 64-0823E “Maswali na Majibu #2.”
Ndugu Joseph Branham