UJUMBE: 64-0726E Mabirika Yavujayo
- 26-0104 Mabirika Yavujayo
- 24-0407 Mabirika Yavujayo
- 22-0911 Mabirika Yavujayo
- 21-0425 Mabirika Yavujayo
- 19-1117 Mabirika Yavujayo
- 17-1022 Mabirika Yavujayo na Prelimininari
- 16-0626E Mabirika Yavujayo
Wapendwa Wanywaji Wa Kisima Kinachofoka Maji,
Ni Krismasi na Mwaka Mpya ulioje tuliokuwa nao. Tumezikubali na kuzifungua zawadi za Mungu alizomtumia Bibi-arusi Wake. Zawadi yetu ya kwanza ilikuwa ni Zawadi kuu kuliko zote ya Krismasi iliyowahi kufungwa. Mungu Mwenyewe alijifunga Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu na akakituma kifurushi hicho duniani. Ilikuwa ndio Zawadi Yake kubwa sana ya kwanza ya kumrejesha Bibi-arusi Wake.
Kisha Mungu akakituma kifurushi kingine kikubwa kwa Bibi-arusi Wake. Yeye alitupenda sana hivi kwamba alikuja na kujifunua Mwenyewe katika mwili tena ili aweze kuzungumza nasi mdomo kwa sikio. Alitaka Yeye na Bibi-arusi Wake wawe Mmoja.
Na sasa, enyi marafiki, msinielewe vibaya. Naomba niliseme hili kwa heshima moyoni mwangu, nikijua kwamba mimi ni mtu ninayeelekea kwenye Umilele ambaye nitasimama mbele ya Hukumu siku moja: Maelfu ya watu wanaikosa zawadi yao waliotumiwa. Unaona? Hawawezi kuielewa. Nao wanaangalia, na kusema, “Loo, yeye ni mtu tu.” hiyo ni kweli. Je, ilikuwa ni Mungu au Musa aliyewaokoa wale watu? Ilikuwa ni Mungu ndani ya Musa. Unaona? Wao walimlilia mkombozi. Na wakati Mungu alipowatumia huyo mkombozi, walishindwa kuliona, kwa sababu ilikuwa kupitia mtu, lakini haikuwa huyo mtu, ilikuwa ni Mungu ndani ya mtu huyo.
Leo, kwa mara nyingine tena, maelfu ya watu wanaikosa zawadi yao na kusema, “huna haja ya kusikiliza kanda, hivi sasa kuna watu wengine waliotiwa mafuta,” ambayo ni kweli, lakini wao wanashindwa kutambua kuwa hiyo ndio Sauti PEKEE iliyothibitishwa na Mungu, inenayo Bwana Asema Hivi kupitia mtu huyo. Sauti hiyo ndio Urimu na Thumimu ya Mungu, Yakini Yake ya wakati huu.
Tunapoisikiliza Sauti Yake iliyo kwenye kanda tunakunywa kweli kutoka kwenye Kisima cha Mungu kinachofoka maji, ambacho hakihitaji kuvuta kwa mashine, kuvuta, kujiunga, kuteka; sisi tunaamini tu na kutegemea kila Neno Linalonenwa.
Kwa sisi kuisikiliza Sauti hiyo iliyo kwenye kanda, kulingana na Yesu Mwenyewe, tunao ushahidi wa kweli wa Roho Mtakatifu katika siku yetu.
Kwa hiyo huo hapo ushahidi halisi wa Roho Mtakatifu! Yeye hajaniambia bado jambo lo lote ambalo si sahihi. Ya kwamba, “Ni ushahidi wa Roho Mtakatifu, ni yeye yule anayeweza kuliamini Neno.” kama unaweza kulipokea.
Mungu ametuandalia Chemchemi tunayoweza kuinywea kila dakika ya kila siku. Daima ni safi. Si kitu fulani kilichooza, Ni Chemchemi Yake isiyokauka, inayojitegemea; unatakiwa tu Ubonyeze Play.
Tukinena kuhusu ZAWADI kutoka kwa Mungu, Je, unaweza kuwazia kweli jinsi gani Zawadi hii ilivyo KUU? Kwa Kubonyeza play tu na kuisikiliza Sauti Yake iliyo kwenye kanda, ndiyo pekee… SAUTI PEKEE duniani ambayo huhitaji chujio, kichujio, au chochote kile. Unatakiwa tu kusikiliza, kuamini, na kusema amina kwa kila Neno.
Mungu Mwenyewe ameiandaa njia hii, NJIA YAKE PEKEE, ya kupokea uzima wa milele, na muhimu zaidi, YA KUWA BIBI-ARUSI WAKE. Tunaweza tu kulala kifuani Mwake na kuzinyonya nguvu zetu kwa kuisikiliza Chemchemi Yake, Sauti Yake, El Shaddai akizungumza na Bibi-arusi Wake.
Hebu mwaka huu na uwe ndio mwaka atakaokuja kutuchukua, sisi Bibi-arusi Wake mpendwa. Tunatazamia na kungoja kwa matarajio makubwa. Siku yoyote hivi sasa tutawaona wale ambao tumetamani kuwaona wakitokea. Tutatambua, Katika kufumba na kufumbua jicho, tutakuwa tumetoka mahali hapa, tumeitwa kwenda kwenye Karamu yetu ya Harusi.
Bwana, tuonapo meza hiyo kubwa imetandazwa pale kwa ajili ya hiyo karamu, maelfu ya maili, tukitazamana, askari wa vita walio na majeraha, machozi ya furaha yakitiririka mashavuni mwetu… Mfalme akijitokeza katika uzuri Wake, utakatifu, ashuke mezani na kuchukua mikono Yake Mwenyewe na kuyafuta machozi kutoka machoni mwetu, akisema, “Msilie tena, yote yamekwisha. Ingieni katika raha za Bwana.” Taabu za safarini hazitaonekana kuwa kitu wakati huo, Baba, tutakapofika kwenye mwisho wa njia.
Njoo unywe, unywe, unywe, unywe pamoja nasi kutoka kwenye Chemchemi iliyoandaliwa na Mungu ya siku hii Jumapili hii saa 06:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville. (ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) Ndio mahali PEKEE ambapo unaweza kupumzika kabisa na kusema AMINA kwa kila Neno usikialo. Ndicho kisima Chake kinachofoka maji kilichoandaliwa ili Bibi-arusi Wake apate kukinywea.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 64-0726E Mabirika Yavujayo
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikiliza Ujumbe:
Zaburi 36:9
Yeremia 2:12-13
Yohana 3:16
Ufunuo Sura ya 13