UJUMBE: 64-0726M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 25-1228 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 24-0324 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 22-0904 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 21-0418 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 19-1110 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake (pamoja preliminari)
- 17-1015 Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
- 16-0626M Kutambua Siku Yako Na Ujumbe Wake
Mpendwa Bibi-arusi Aliyekatwa Akatolewa,
Leo, kanisa limemsahau nabii wao. Hawamhitaji yeye tena ahubiri katika makanisa yao. Wanadai wana wachungaji wao wa kuwahubiria na kuwanukulia na kuwafasiria Neno. Kuhubiri ni muhimu zaidi kuliko kuisikiliza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda katika makanisa yao.
Bali Mungu alijua Yeye hana budi kuwa na nabii Wake; hivyo ndivyo Yeye amekuwa akimwita atoke na kumwongoza Bibi-arusi Wake kila wakati. Yeye Alitukata akatutoa kutoka miongoni mwa mataifa mengine kwa Upanga Wake wenye makali kuwili, Roho Wake Mtakatifu, Sauti Yake iliyonenwa na nabii Wake.
Yeye ametukata kwa Sauti hiyo. Ndiyo maana aliirekodi na kuiweka kwenye kanda. Kwa Ufunuo tunaona jinsi Maandiko yalivyo makamilifu! Bibi-arusi hawezi kuivishwa isipokuwa Mwana aiivishe.
Haidhuru utahubiri namna gani, hata ufanye nini, haliwezi kuivishwa, haliwezi kudhihirishwa, haliwezi kuthibitishwa; ila tu na Yeye aliyesema, “Mimi Ndimi Nuru ya ulimwengu,” lile Neno.
Neno lilituambia Roho Mtakatifu Mwenyewe atatokea na kutuivisha, ili kuthibitisha, kuhakikisha na kujidhihirisha. Nuru ya jioni imekuja. Mungu akijidhihirisha Mwenyewe katika mwili ili kumwita Bibi-arusi Wake atoke.
Yeye Ndiye aliyekuita WEWE utoke kwa Roho Wake Mtakatifu, Neno Lake, Sauti Yake. Yeye Ndiye aliyekuchagua WEWE. Yeye Ndiye anayekufundisha WEWE. Yeye Ndiye anayekuongoza WEWE. Kwa kitu gani? Roho Wake Mtakatifu, Sauti Yake ikizungumza NA WEWE MOJA KWA MOJA.
Lakini kwao Hilo limepitwa na wakati sana katika siku hii. Wamepita muda wa kuzicheza kanda makanisani mwao. Wao hawalitambui. Hiyo ndiyo sababu wako katika hali waliyo nayo. Lakini kwako wewe, imefunuliwa Kuwa ndio njia ya Mungu Iliyoandaliwa, NI BWANA ASEMA HIVI KWAKO.
Kwa hiyo hakuna budi kutokee Nguvu fu—fu—fulani, Roho Mtakatifu Mwenyewe, kuivisha, ama kuthibitisha, ama kuhakikisha, ama kudhihirisha ya kwamba yale ambayo Yeye amebashiri yangetukia katika siku hii. Nuru ya jioni inaleta hilo. Ni wakati wa jinsi gani!
Sisi ndiye Bibi-arusi Neno mkamilifu ambaye nabii Wake alimwona katika ono. Sisi ndio wale ambao Yeye alimtuma nabii Wake kuwaita watoke kwa Neno Lake, na sasa tunao UAMSHO, kwa maana sasa tunajua sisi ni nani.
Kufufua, hapo, ni neno lile lile linalotumika mahali pengine popote, ndiyo kwanza nilichunguze, linamaanisha, “uamsho.” “Yeye atatufufua baada ya siku mbili.” Hiyo ingekuwa, “Katika siku ya tatu Yeye atatufufua tena, baada ya kututawanya, na kutupofusha, na kuturarua.”
Baba alimtuma nabii Wake kumwangalia Bibi-arusi Wake ili kwamba tusitoke mstarini. Kumbuka, hili lilikuwa ono!
Bibi-arusi alipitia mahali pale pale alipopitia wakati alipokuwa hapo mwanzo. Lakini nilikuwa nikimwangalia akitoka mstarini, na nikijaribu kumvuta arudi kwenye mstari.
Lakini “yeye” angewezaje kumvuta arudi mstarini leo? “Yeye”, mtu huyo, hayupo hapa duniani. KWA NENO! Neno PEKEE lililothibitishwa la wakati huu ni lipi? Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Wahudumu wameitiwa kulihubiri Neno kwa kunukuu kile hasa nabii alichosema. Kulingana na nabii mwenyewe, wao hawapaswi kusema chochote zaidi.
Kweli, wameitiwa kulifundisha na kulihubiri Neno hilo. Lakini kuna SAUTI MOJA PEKE YAKE ILIYOTHIBITISHWA NA MUNGU MWENYEWE KUWA BWANA ASEMA HIVI.
Nasema vivyo hivyo katika Jina la Yesu Kristo. Usiongeze kitu. Usiondoe—kuliwekea mawazo yako. Wewe sema tu yaliyosemwa katika kanda hizo. Tenda sawasawa kabisa na vile Bwana Mungu amekuamuru kutenda. Usiongezee Kwake!
Kama ukisema “amina” kwa kila neno ambalo mchungaji wako au mhudumu wako asemalo, umepotea. Lakini ukisema “AMINA” KWA KILA NENO AMBALO MUNGU ALILOLINENA KUPITIA NABII WAKE KWENYE KANDA, WEWE NDIYE BIBI-ARUSI NA UTAKUWA NA UZIMA WA MILELE.
Nabii wa Mungu alikuwa ndiye mtu ambaye Mungu alimchagua kuzungumza kupitia yeye. Ilikuwa ni CHAGUO LA MUNGU kumtumia yeye kulinena Neno Lake na kuliweka kwenye kanda ili kwamba Bibi-arusi angekuwa SIKU ZOTE NA BWANA ASEMA HIVI YA KUSIKIA.
Yeye hataki Bibi-arusi Wake ategemee kile watu wengine wasemacho, au fasiri yao ya Neno Lake. Yeye anataka Bibi-arusi Wake asikie kutoka kwenye midomo Yake hadi masikioni mwao. Yeye hataki Bibi-arusi Wake amtegemee mtu mwingine yeyote ila Yeye Mwenyewe.
Tunapoamka asubuhi, tunapenda Yeye atuambie, “Habari za asubuhi marafiki. Nitazungumza nanyi leo na kuwaambieni jinsi gani ninavyowapenda na jinsi ambavyo ninyi na Mimi tulivyo MMOJA. Ninao wengi ambao nitakaowapa uzima wa milele, bali ni WEWE peke yake ndiye Bibi-arusi niliyemchagua kwa mkono Wangu. WEWE peke yake ndiye niliyempa Ufunuo kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu.
Wengine wengi wanapenda kunisikia, lakini Mimi nimewachagua ninyi kuwa Bibi-arusi Wangu. Kwa maana mmenitambua Mimi nanyi mmedumu na Neno Langu. Hamjapatana, hamjabembana, bali mmedumu waaminifu na Neno Langu.
Muda umekaribia. Ninakuja kuwachukua hivi karibuni. Kwanza, mtawaona wale walio pamoja nami sasa. Loo, jinsi wao wanavyotamani kuwaona na kuwa pamoja nanyi. Msihofu enyi watoto, kila kitu kiko kikamilifu kwenye wakati unaofaa, endeleeni tu kusonga mbele.”
Kama mhudumu wa Injili, siwezi kuona jambo moja lililosalia ila kule kuondoka kwa Bibi-arusi.
Ndugu. Joseph Branham
Ujumbe: 64-0726M “Kutambua Siku Yako na Ujumbe Wake”
Muda: saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville(ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki)
Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikia Ujumbe:
Hosea: Sura ya 6
Ezekieli: Sura ya 37
Malaki: 3:1 / 4:5-6
Timotheo wa Pili: 3:1-9
Ufunuo: Sura ya 11