UJUMBE: 64-0719M Sikukuu Ya Baragumu
- 25-1214 Sikukuu Ya Baragumu
- 24-0310 Sikukuu Ya Baragumu
- 22-0821 Sikukuu Ya Baragumu
- 21-0328 Sikukuu Ya Baragumu
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 17-1008 Sikukuu Ya Baragumu – Preliminari
Mpendwa Bibi-arusi Mkamilifu,
Hili si jambo tu la kujibunia, enyi marafiki. Hii ni BWANA ASEMA HIVI, Maandiko.
Kila Mkristo anataka kuwa Bibi-arusi, lakini tunajua Bibi-arusi Wake watakuwa wachache tu waliochaguliwa. Tunajua Yeye anayo mapenzi ya kuruhusia, lakini Bibi-arusi Wake lazima awe katika mapenzi Yake makamilifu. Kwa hivyo, lazima tumtafute Mungu katika Neno Lake, na kisha kwa Ufunuo, tutajua mapenzi Yake makamilifu jinsi ya kuwa Bibi-arusi Wake.
Tunapaswa kuyachunguza Maandiko, kwa maana tunajua Mungu KAMWE Habadilishi mawazo Yake kuhusu Neno Lake. Mungu habadilishi mpango Wake. Yeye habadilishi CHOCHOTE. Jinsi alivyofanya mara ya kwanza ni kamilifu. Kile Yeye alichofanya jana atafanya vivyo hivyo leo.
Jinsi Yeye alivyomwokoa mwanadamu tangu mwanzo, itambidi amwokoe mtu leo kwa njia ile ile. Jinsi Yeye alivyomponya mtu wa kwanza, hana budi kufanya vivyo hivyo leo. Jinsi ambavyo Mungu alichagua kumwita na kumwongoza Bibi-arusi Wake, atafanya vivyo hivyo leo; kwa kuwa Yeye ni Mungu na hawezi kubadilika. Neno linatuambia kwamba Yesu Kristo ni YEYE YULE jana, leo na hata milele.
Kwa hivyo, wakati tunapolisoma Neno Lake, tunaweza kuona wazi kabisa Jinsi Yeye alivyochagua kumwita na kumwongoza Bibi-arusi Wake kwa kila kizazi. Yeye Alimchagua MTU MMOJA. Alisema wao walikuwa Neno la siku yao. Nabii alituambia Yeye KAMWE hakuwa na kundi la watu; wao wana njia tofauti, mawazo tofauti, na muhimu zaidi, alisema, NENO LA MUNGU HALIHITAJI KUFASIRIWA.
Kwa hivyo, kile kila nabii alichosema katika kila kizazi hakiwezi kuongezwa kwake au kuondolewa. Lazima iwe Neno kwa Neno kile ALICHONENA. Rahisi sana ukiniuliza mimi Njia ya Mungu iliyoandaliwa ni ipi….DUMU NA NABII.
Sasa, sio tu kwamba tunajua fika njia ya Mungu iliyoandaliwa tangu mwanzo vile imekuwa, bali Bwana Yeye hata atanena kupitia malaika Wake na kutuambia kile Yeye atakachofanya katika siku zijazo, ili tu kuthibitisha kwa mara nyingine tena, MUNGU HABADILISHI MPANGO WAKE.
Baada ya Bibi-arusi Wake (sisi) kuondoka hapa duniani na kuitwa kwenda kwenye Karamu ya Harusi, Mungu atawaitaje wale Wayahudi 144,000 waliochaguliwa? Kundi la watu?
Sasa, mara Kanisa hili (Bibi-arusi) limevutwa pamoja, linanyakuliwa; na ile siri ya Muhuri ya Saba, ama Muhuri ya Saba, ile siri ya kuondoka. Nao Wayahudi wanaitwa kwa siri ya Baragumu ya Saba, ambayo ni manabii wawili, Elia na Musa, nao wanarudi.
Kwa hivyo mara tu Bibi-arusi atakapovutwa pamoja, tutatwaliwa juu. Tunajua kuna kitu kimoja tu kinachoweza kumvuta Bibi-arusi pamoja, Roho Mtakatifu, Naye Roho Mtakatifu ni Neno Lake, nalo Neno Lake la siku hii ni Sauti ya Mungu, nayo Sauti ya Mungu ni…
Kama nimewaudhi kwa kusema hivyo, nisameheni, lakini, nilihisi hilo huenda lilichukiwa, bali, mimi ni Sauti ya Mungu kwenu. Mnaona? Nalisema hilo tena, wakati huo ilikuwa chini ya uvuvio, mnaona.
Naomba niingilie hapa na niseme, NUKUU hii MOJA tu kutoka kwa malaika-mjumbe wa Mungu aliyethibitishwa inapaswa kutosha kabisa kwa wote wanaojiita waaminio katika Ujumbe huu wa wakati wa mwisho wadai mchungaji wao ABONYEZE PLAY katika makanisa yao au ajiuzulu ili waweze kumpigia kura mchungaji mwenye UFUNUO WA KWELI KUTOKA KWA MUNGU.
Kwa hivyo, Baragumu ilipigwa nao manabii wawili wakatokea kwani Yeye hawezi kuwa na malaika Wake wa saba pamoja na Bibi-arusi Wake hapa duniani wakati ule ule wao wanapokuja. Kwa hivyo Yeye anawaitaje Wayahudi? Kwa njia ile ile aliyomwita Bibi-arusi Wake Mmataifa.
Nao Wayahudi wanaitwa kwa siri ya Baragumu ya Saba, ambayo ni manabii wawili…
Bibi-arusi hana budi kuondoka njiani, apate kwenda juu sasa; kusudi wale watumishi wawili, wale watumishi wawili wa Mungu, katika Ufunuo, wale manabii wawili, wapate kujitokeza, kusudi wawapigie ile Baragumu ya Saba, wawajulishe Kristo.
Ni wazi kabisa, Mungu habadilishi mpango Wake. Yeye aliwatuma manabii Wake. Kwa hivyo, Bibi-arusi Wake atadumu na njia Yake iliyoandaliwa, nabii-malaika Wake, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Kisha ili kulifanya liwe wazi kabisa, Mungu kwa mara nyingine tena anazungumza na kumwambia Bibi-arusi Wake: Mmedumu waaminifu Kwangu na njia Yangu iliyoandaliwa, kwa hivyo njia Yangu iliyoandaliwa ya siku yenu itawaambieni:
Yule malaika wa saba, mjumbe, aseme, “Tazama Mwana-Kondoo wa Mungu aichukuaye dhambi ya ulimwengu!”
SAUTI HIYO ni muhimu sana; SAUTI YA MUNGU ikinena kupitia malaika Wake wa saba kwenye kanda. Mungu ataitumia SAUTI HIYO, SAUTI YA MALAIKA WAKE WA SABA. SIO KUNDI…SIO MIMI…SIO MCHUNGAJI WAKO…SAUTI YA MALAIKA-MJUMBE WAKE WA SABA kututambulisha sisi Kwake, Bwana wetu Yesu Kristo.
Kwa hivyo, tunafahamu:
- SISI NDIO BIBI-ARUSI WAKE.
- TUKO KATIKA MAPENZI YAKE MAKAMILIFU.
- TUNAUFUATA MPANGO WAKE KWA AJILI YA SIKU HII KWA KUBONYEZA PLAY.
Sehemu ya Bibi-arusi Wake itakusanyika Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, masaa ya Jeffersonville,(ni saa 2:00 USIKU ya Afrika Mashariki) kumsikiliza mchungaji wetu, malaika- mjumbe wa Mungu, William Marrion Branham, Naye atakuwa akizungumza nasi na kutufunulia kwamba halipo kanisa lingine, hamna kundi lingine la watu tangu kuumbwa kwa ulimwengu, ambalo limewahi kupata fursa tuliyonayo ya kuungana pamoja kumsikiliza Mungu akizungumza nao moja kwa moja.
Sisi ni watu waliobarikiwa Jinsi gani. Tunayo furaha sana. Tunashukuru sana. Bibi-arusi anafanyika MMOJA na Bwana-Arusi
Ndugu Joseph Branham
Sikukuu Ya Baragumu 64-0719M.
Maandiko ya kusoma kabla ya Kusikiliza Ujumbe:
Mambo ya Malawi 16
Mambo ya Walawi 23:23-27
Isaya 18:1-3
Isaya 27:12-13
Ufunuo 10:1-7
Ufunuo 9:13-14
Ufunuo 17:8