UJUMBE: 63-0630E Je! Maisha Yako Yanaistahili Injili?
- 25-0914 Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili?
- 23-1008 Je, Maisha Yako Yanaistahili Injili?
- Pasaka 2022
- 22-0415 Je! Maisha Yako Yanaistahili Injili?
- 22-0414 Kutoka kwa Tatu na Kutawadhana Miguu
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
Ndugu na Dada Wapendwa,
Ninampenda Bwana, Neno la Mungu, Ujumbe huu, Sauti Yake, nabii Wake, Bibi-arusi Wake, zaidi ya uhai wenyewe. Wote ni KITU KIMOJA KWANGU MIMI. Sitaki kamwe kupatana kwenye yodi moja, nukta moja ndogo, ama NENO MOJA ambalo Mungu aliloandika katika Neno Lake ama alilolinena kupitia nabii Wake. Kwangu mimi, Yote ni Bwana Asema Hivi.
Mungu aliliwaza, kisha akalinena kwa manabii Wake, nao wakaliandika Neno Lake. Ndipo akamtuma malaika Wake mwenye nguvu, William Marrion Branham, duniani katika siku yetu ili Yeye aweze kujifunua Mwenyewe katika mwili wa mwanadamu kwa mara nyingine tena, kama alivyofanya kwa Ibrahimu. Kisha Yeye akanena kupitia nabii Wake awe Sauti ya Mungu kwa ulimwengu, kufunua na kuzifasiri siri zote ambazo zimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu kwa Bibi-arusi Wake aliyechaguliwa tangu zamani.
Sasa, Bibi-arusi Wake, NINYI, mnakuwa Neno lililofanyika mwili; Mmoja na Yeye, Bibi-arusi Neno Wake aliyerejeshwa kikamilifu.
Najua ninaeleweka vibaya kwa kile ninachosema na ninachoandika. Naomba niseme kwa unyenyekevu kama nabii wetu alivyosema, mimi sina elimu nami najua siwezi kuandika ama kuzungumza kwa usahihi kile ninachojisikia moyoni mwangu. Ninakubali inaonekana kama ninaandika kwa ukali sana wakati mwingine. Ninapofanya hivyo, sio kuonyesha kutoheshimu, au kuwa na mtazamo mbaya ama kumhukumu mtu fulani, bali kinyume chake. Ninafanya hivyo kwa upendo ulio moyoni mwangu kwa Neno la Mungu.
Ninataka kila mtu aukubali na kuuamini Ujumbe huu Mungu alioutuma kumwita Bibi-arusi Wake atoke. Sijawahi kamwe kuhisi moyoni mwangu au akilini kwamba wahudumu hawapaswi kuhubiri tena; ingekuwa ni kwenda kinyume na Neno la Mungu. Mimi nina bidii tu kwa ajili ya Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ninaamini ndiyo Sauti muhimu sana WAHUDUMU WOTE wanayopaswa kuiweka Kuwa ya KWANZA mbele ya watu. Hii haimaanishi kuwa hawawezi kuhubiri, nataka tu kuwatia moyo kuzicheza kanda katika makanisa yao wakati watu wamekusanyika chini ya upako huo.
Ndiyo, ningependa kuufanya ulimwengu mzima usikilize Ujumbe ule ule kwa wakati mmoja ulimwenguni kote. Si kwa sababu “Mimi” nilisema hivyo, au kwa sababu “Mimi” niliichagua kanda ya kusikiliza, bali ninahisi hakika Bibi-arusi angeona Jinsi gani Mungu ameifanya njia kwa jambo hili kutendeka katika siku yetu.
Kama tungekuwa na rekodi za Yesu akinena leo kwenye kanda, si maandishi ya Mathayo, Marko, Luka au ya Yohana ya yale Yesu aliyosema (kwa maana wote walilisema tofauti kidogo), bali tungeweza kuisikia Sauti ya Yesu, utu Wake, aiko, pepa, na dafuta Zake kwa masikio yetu wenyewe, je! wahudumu leo wangeliambia kanisa lao, “Hatutaicheza rekodi ya Yesu kanisani mwetu. Mimi nimeitwa na nimepakwa mafuta kuihubiri na kuinukuu. Ninyi isikilizeni mwendapo nyumbani.” Je! watu wangelisimamia hilo? Inasikitisha kusema hivyo, lakini hivyo ndivyo wao wanavyofanya leo hii. HAKUNA TOFAUTI, haijalishi jinsi gani wanavyolipaka chokaa.
Kwangu mimi, Ndugu Branham alitupa kielelezo. Alipenda wakati makanisa yote, majumba, au popote pale walipokuwa, walipokuwa kwenye muunganisho wa simu ili waweze kuusikia Ujumbe wote kwa wakati mmoja. Yeye alijua wangeweza, na wangezipata, kanda na kuisikiliza baadaye, lakini yeye aliwataka waungane na kuusikia Ujumbe wote kwa wakati mmoja….KWANGU MIMI HUYO ALIKUWA NI MUNGU AKIMUONYESHA BIBI-ARUSI WAKE NINI KITATOKEA KATIKA SIKU YETU NA KIPI CHA KUFANYA.
Kila mhudumu mwaminio wa kweli wa Ujumbe atakubali hakuna kitu kilicho kikuu zaidi ya kukaa chini ya upako wa Sauti ya Mungu, ambayo imerekodiwa na kuwekwa kwenye kanda. Bibi-arusi ataamini, na kuwa na Ufunuo, ya kwamba Ujumbe huu ndilo Neno la Mungu la wakati huu. Ninaweza tu kuhukumu kwa Neno, lakini mtu ye yote ambaye hangesema Ujumbe huu ndiyo Yakini yao, hana Ufunuo wa Neno la wakati huu, kwa hivyo, wangewezaje kuwa Bibi-arusi Wake?
Siyo tu kulinukuu, kulihubiri au kulifundisha, bali kulisikia kwenye kanda ndipo MAHALI PEKEE ambapo Bibi-arusi anaweza kusema ninaliamini kila Neno. Ujumbe huu ni Bwana Asema Hivi. Kile ninachohubiri au ninachofundisha si Bwana Asema Hivi, bali yale Sauti ya Mungu isemayo kwenye kanda NDIYO…hiyo ndiyo Sauti PEKEE iliyothibitishwa na Nguzo ya Moto.
Ninajua kuna ndugu na dada wanaosema, na kuhisi, ati “Kama hamsikilizi Ujumbe ambao Maskani ya Branham inaoutuma, hamzisomi barua za Tai Wanakusanyika, na kusikiliza majumbani mwenu wakati ule ule wewe si Bibi-arusi,” ama, “Ni makosa kwenda kanisani, inakubidi ukae nyumbani kwako.” HILO NI KOSA SANA. Sijawahi KAMWE kuwaza hivyo, kusema hivyo, ama kuamini hivyo. Hilo limesababisha utengano hata na zaidi, fikra ngumu, na kuondoa ushirika miongoni mwa Bibi-arusi naye adui anatumia jambo hilo kuwatenganisha watu.
Sitaki kamwe kumtenganisha Bibi-arusi, nataka kumuunganisha Bibi-arusi kama vile Neno lilivyosema LAZIMA TUUNGANE TUWE KITU KIMOJA. Hatupaswi kubishana sisi kwa sisi, lakini hakuna kabisa kitu kingine chochote kile kinachoweza kutuunganisha ila Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Hatupaswi kuzozana na kuwaambia watu WANAPASWA WAFANYE nini la sivyo wao sio Bibi-arusi, ninyi fanyeni jinsi BWANA ANAVYOWAONGOZA. Wao bado ni ndugu na dada zetu. Tunahitaji kupendana na kuheshimiana mmoja kwa mwingine.
Sasa, usibishane. Unaona? Hasira huzaa hasira. Muda si muda wajua, unamhuzunisha Roho Mtakatifu anakuacha, utarudisha ubishi tena. Ndipo Roho Mtakatifu anaruka anaenda zake. Hasira huzaa hasira.
Kwa kile nabii alichosema hapa, sitaki kamwe kumhuzunisha Roho Mtakatifu. Sitaki kubishana kamwe. Tunaweza kusemezana kwa upendo, lakini si kubishana. Ikiwa nimesema jambo lolote ambalo limemuudhi yeyote katika yale niliyoyaandika ama kusema, tafadhali nisamehe, haikuwa kusudi langu.
Kama nilivyoeleza hapo awali, ninauhisi wito maishani mwangu kutoka kwa Bwana kuwaelekeza watu kwenye Sauti ya Mungu kwa ajili ya siku hii. Wahudumu wengine wana miito mingine na pengine wanaona mambo tofauti, Bwana asifiwe, wanafanya kile WAO wanachojisikia wanaongozwa na Roho Mtakatifu. Huduma yangu ni kumwambia tu Bibi-arusi, “BONYEZA PLAY” na “Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda ndiyo Sauti iliyo muhimu zaidi mnayoweza kuisikia.” “Ninaamini kwamba wahudumu wanapaswa kuicheza Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda katika makanisa yao.”
Barua ninazoziandika kila wiki ni za sehemu ya Bibi-arusi wale wanaojisikia kuwa ni sehemu ya Maskani ya Branham. Najua wengine wengi huzisoma, Lakini mimi ninawajibika tu kufanya vile ninavyojisikia kuongozwa kwa ajili ya kanisa letu. Kila kanisa linajitawala lenyewe; hawanabudi kufanya vile wanavyojisikia wanaongozwa na Bwana kufanya, hilo ni Neno 100%. Mimi siwapingi wao, tunatofautiana tu. Mimi na Maskani ya Branham, tunataka tu kuisikia Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.
Ninaualika ulimwengu kuungana nasi kila wiki. Ninawatia moyo ikiwa hawawezi kuungana nasi, wachague kanda, kanda yoyote, na kubonyeza play. Watatiwa mafuta kuliko hapo kabla. Hivyo, ninawaalika wiki hii muungane nasi Jumapili saa 06:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1 JIONI ya Afrika Mashariki) tunapoungana pamoja na kusikia, 63-0630E Je! Maisha Yako Yanaistahili Injili?
Ndugu Joseph Branham