UJUME: 63-0630M Kutoka Kwa Tatu
- 25-0907 Kutoka Kwa Tatu
- 23-1001 Kutoka Kwa Tatu
- Pasaka 2022
- 22-0414 Kutoka kwa Tatu na Kutawadhana Miguu
- 21-0718 Kutoka kwa tatu
- NUKUU YA LEO KWA KISWAHILI
Mpendwa Bibi-arusi Wa Kutoka Kwa Tatu,
Ikiwa huna jicho la kiroho, hulipati. Lakini jicho la kiroho linaweza kuona Nguvu za Mungu zikitenda kazi maana hilo liko kwenye Neno kikamilifu. Ni Neno, nalo Neno la Mungu halibadiliki kamwe. Kile Yeye alichokifanya hapo mwanzo, anafanya vivyo hivyo sasa nalo jicho la kiroho linaliona, linaliamini, na KULISIKIA.
Ulimwengu unaweza kutokukubaliana nami katika kile ninachoamini kuwa ndiyo njia ya Mungu iliyoandaliwa Kwa ajili ya wakati huu: Sauti iliyo muhimu sana unayopaswa kuisikia ni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ni lazima mzicheze kanda makanisani mwenu, lakini KAMA kweli mnauamini Ujumbe huu, basi hamwezi kupingana na kile nabii wa Mungu anachosema.
Jumapili hii tutakusanyika kama wale wana wa Kiebrania walivyofanya ili kuipata mana ile iliyokuwa imeandaliwa kwa ajili yao usiku kucha, ambayo ingewahifadhi siku inayofuata. Sisi tutakusanyika kwa ajili ya Mana yetu ya Kiroho itakayotutia nguvu kwa ajili ya kule Kutoka kwetu kukuu kunakokuja hivi karibuni.
Hakuna njia bora zaidi kuliko kumruhusu Sauti ya Mungu yeye aliseme hilo Mwenyewe, kumhusu yeye Mwenyewe, nao Ujumbe huu tunaoenda kuusikia UMESHEHENI!
Mungu alimpeleka mtu mmoja nyikani, akamfunza. Kisha akamrudisha, na kukipeleka kitu hicho huko, kisha akawatoa hao watu. Mnaona ninalomaanisha? Yeye hawezi kubadilisha mpango Wake. Yeye ni Mungu.
Kwa hivyo hapa Yeye anatuambia waziwazi Yeye kamwe habadilishi mpango Wake. Kile Yeye alichokifanya tangu mwanzo, atakifanya tena mwishoni, Yeye aliahidi. Kwa hiyo sasa ni lazima tujue Mpango Wake ulikuwa nini wakati ule kwani utakuwa ni Mpango ule ule hivi sasa.
Kamwe hatashughulika na kundi. Kamwe hajafanya hivyo. Yeye hushughulika na mtu mmoja; na alifanya hivyo, na atafanya hivyo. Na aliahidi, hata katika Malaki 4, angefanya hivyo.
Yeye kamwe hashughuliki na kundi. Kwa hivyo, Yeye aliahidi katika wakati wetu kwamba angemtuma mtu Mmoja, Malaki 4, akiwa na Bwana Asema Hivi.
Hiyo ni kweli. Kwa hiyo kuna ahadi Yake, kwamba Yeye alikuwa ni nani; ahadi ya kile alichosema Yeye angekifanya, na basi tumewasili. Tunapaswa kuwa ni watu wenye furaha jinsi gani; akiwapa ishara, kwa ishara ya Neno Lake lililoahidiwa, Neno lililoahidiwa. Aliahidi angefanya hivyo.
Mungu alichagua kumwongoza Bibi-arusi Wake namna gani wakati ule?
Mungu alichagua, katika siku za kule kutoka, Yeye aliliita kundi moja litoke. Na kutoka kwenye kundi hilo, ninawataka muone jambo fulani, Yeye alipata tu wawili walioingia kwenye nchi ya ahadi. Yeye alichagua kuwatoa kwa kutumia nini?
Hili hapa. Hili ni muhimu sana kwa wenye nia ya kiroho kuweza kulishika. Mungu alichagua kumwongoza na kumpeleka Bibi-arusi kwenye Nchi ya Ahadi namna gani?
Siasa? dhehebu? Yeye alichagua nabii, akiwa na ishara ya kimbinguni ya Nguzo ya Moto, watu wasije wakakosea. Yale nabii aliyosema yalikuwa ni Kweli. Na Mungu alishuka, Nguzo ya Moto, na kujithibitisha Mwenyewe, akaonyesha Neno Lake. Hiyo ni kweli? Hiyo ndiyo aliyoileta, kutoka Kwake kwa kwanza. Kutoka Kwake kwa pili…
Kwa hiyo, ili kuhakikisha kwamba watu hawangekosea, Yeye aliwatumia nabii akiwa na ishara ya kimbinguni ya Nguzo ya Moto kwa ajili ya kule kutoka kwao kukuu.
Yeye alifanya nini, kule kutoka kwa kwanza? Alimtuma nabii, aliyetiwa mafuta kwa Nguzo ya Moto, naye akawaita watu wakatoka. Huko kulikuwa ni kutoka Kwake kwa kwanza…
Kutoka kwa pili, Yeye alimleta Nabii, aliyetiwa mafuta, ambaye alikuwa ni Mwanawe, Mungu-Nabii. Musa alisema Yeye angekuwa ni Nabii; Naye alikuwa na Nguzo ya Moto, na akafanya ishara na maajabu…
Na hapa Yeye aliahidi jambo lile lile katika kule kutoka katika siku za mwisho, wala hawezi kulibadili…
Wengi watakubali kwa kusema, naam, Yeye alimtuma nabii kumwita Bibi-arusi atoke, lakini sasa hivi Roho Mtakatifu Yeye atamwongoza Bibi-arusi kupitia wahudumu; lakini Yeye hakusema hivyo…hebu na tuendelee kusoma.
Angalieni ile Nguzo ya Moto iliyowaita watoke, ikawaongoza kwenye nchi ya ahadi, chini ya upako wa nabii. Nguzo ya Moto ambayo wangeweza kuiangalia, iliwaongoza kwenye nchi ya ahadi, chini ya nabii aliyetiwa mafuta. Nao daima walimkataa. Hiyo ni kweli? Hakika.
Nguzo ii hii ya Moto inawaongoza watu tena kwenye Nchi ya ahadi, ule Utawala wa Miaka Elfu.
Ile Nguzo ya Moto, chini ya uongozi wa Mungu…Mungu alikuwa ni ule Moto, na ile Nguzo ya Moto ilimtia mafuta tu yule nabii. Ile Nguzo ya Moto ilikuwa isimame kama ushahidi wa Mbinguni kwamba Musa alikuwa ameitwa atoke.
Sasa, kumbukeni, Musa hakuwa hiyo Nguzo ya Moto. Yeye alikuwa ni kiongozi aliyetiwa mafuta, chini ya hiyo Nguzo ya Moto, na hiyo Nguzo ya Moto iliuthibitisha tu Ujumbe wake kwa ishara na maajabu.
Hakuna kosa, enyi marafiki. Si yale ninayosema mimi; mimi ni ndugu yenu tu. Lakini, ni yale Mungu anayowathibitishia, ndiyo yanayolifanya Kweli. Nguzo ile ile ya Moto aliyoitumia kwenye kule kwingine kuwili, Yeye ameileta miongoni mwenu leo, na kuithibitisha kisayansi.
Mungu kamwe habadilishi mpango Wake. Mungu anayo njia iliyoandaliwa kwa ajili ya Bibi-arusi Wake leo: ile Nguzo ya Moto, chini ya uongozi wa Mungu… Mungu alikuwa ni ule Moto, na ile Nguzo ya Moto ilimtia mafuta tu nabii.
Kuna Sauti moja tu, nabii mmoja, aliye na Bwana Asema Hivi, William Marrion Branham. Yeye si ile Nguzo ya Moto, bali yeye ni kiongozi aliyetiwa mafuta chini ya hiyo Nguzo ya Moto.
Sote tunataka kuwa katika Mapenzi MAKAMILIFU ya Mungu. Neno Lake NDIYO mapenzi Yake Makamilifu. Neno lililothibitishwa la wakati wetu ni Ujumbe huu. Nabii Wake ndiye aliyechaguliwa kumwongoza Bibi-arusi Wake. Kama huliamini hilo, huwezi kuwa Bibi-arusi Wake.
Njooni mjiandae kwa ajili ya kule Kutoka kwetu kuu kwa kulisikia Neno Kamilifu la Mungu pamoja nasi Jumapili saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia: Kutoka Kwa Tatu 63-0630M.
Ndugu. Joseph Branham