25-0831 Mbona Unalialia? Nena!

UJUMBE: 63-0714M Mbona Unalialia? Nena!

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Kanisa la Mungu,

Mungu alinena na kusema, ““Mimi sitendi kazi duniani ila kupitia tu kwa mwanadamu. Mimi-Mimi- Mimi ndimi Mzabibu; nanyi ni matawi, na Mimi nitajijulisha Mweyewe tu ninapoweza kumpata mtu MMOJA, na Mimi nimemchagua yeye, William Marrion Branham. Mimi nimemtuma aje akamtoe Bibi-arusi Wangu. Nitaliweka Neno Langu kinywani mwake. Neno Langu litakuwa Neno Lake. Yeye atalinena tu Neno Langu na kusema tu yale Mimi nisemayo.”

Sauti ya Maandiko ilinena kupitia Nguzo ya Moto na kumwambia yeye, “Nimekuchagua wewe, William Branham. Wewe ndiye mtu huyo. Nilikuinua wewe kwa kusudi hili. Nitakuthibitisha kwa ishara na maajabu. Unashuka chini kule kulifunua Neno Langu na kumwongoza Bibi-arusi Wangu. Neno Langu halina budi kutimizwa na WEWE.”

Nabii wetu alikuwa anajua yeye alikuwa ametumwa kwa kusudi hilo hasa la kuzifunua siri zote za Biblia na kumwongoza Bibi-arusi wa Mungu kwenda Nchi ya Ahadi. Yeye alijua kile alichosema, Mungu angekiheshimu na kukitimiza. Nawatakeni msilisahau kamwe Neno hilo. Kile alichokisema nabii wetu, Mungu atakiheshimu, kwa maana Neno la Mungu lilikuwa ndani ya William Marrion Branham. Yeye ni Sauti ya Mungu kwa ulimwengu.

Yeye alijua alikuwa ndiye malaika-mjumbe wa saba wa Mungu aliyetiwa mafuta. Yeye alijua moyoni mwake mambo yote ambayo Mungu aliyokuwa ameyasema kumhusu yeye katika Neno Lake. Kile kilichokuwa kinawaka moyoni mwake kikawa halisi. Yeye alikuwa ametiwa mafuta na alijua alikuwa na BWANA ASEMA HIVI. Hakukuwa na kitu kingalimzuia yeye kutokwenda kulinena Neno la Mungu.

Mungu alimwambia yeye, “Neno Langu, na wewe, mjumbe Wangu, ni kitu kimoja.” Alijua yeye ndiye aliyechaguliwa kulinena Neno lisilokosea. Hilo ndilo tu yeye alilohitaji. Angeweza KUNENA, NAYE MUNGU ANGELITIMIZA.

Ufunuo wa Ujumbe huu NA mjumbe wa Mungu vimeitia mafuta imani yetu zaidi ya hapo awali. Imetupeleka katika miduara mikubwa. Hilo limetutenga na kila kitu isipokuwa Ujumbe Wake, Neno Lake, Sauti Yake, Kanda Zake.

Haijalishi sisi ni wachache jinsi gani, jinsi gani tunavyochekwa, jinsi tunavyodhihakiwa, haileti tofauti hata kidogo. SISI TUNALIONA. SISI TUNALIAMINI. Kuna kitu fulani ndani yetu. Tulichaguliwa tangu awali kuliona HILO na hakuna kitu kitakachotuzuia sisi tusiliamini HILO.

Tunakumbuka kile lile ono lilichosema, “rudi ukakihifadhi Chakula”. Hilo ghala lilikuwa wapi? Maskani ya Branham. Ni mahali gani nchini, ama ulimwenguni mahali popote, pangelinganishwa na Jumbe tulizo nazo? NDIYO Sauti pekee iliyothibitishwa na Mungu Mwenyewe kuwa Bwana Asema Hivi. SAUTI PEKEE!

Ni wapi pengine tungeweza, au tungetaka kwenda, wakati yeye alisema;

Hapa ndipo chakula kimehifadhiwa…

Umehifadhiwa hapa. Uko kwenye kanda; utaenda ulimwengu mzima katika kanda ambapo watu manyumbani mwao. Hizo kanda zitaangukia mikononi mwa wale waliochaguliwa tangu awali wa Mungu. Yeye anaweza kuliongoza Neno; yeye ataelekeza kila kitu kuelekea njia yake hasa. Hiyo ndiyo sababu Yeye alinituma nirudi nikafanye hivi. “Kihifadhi chakula hapa.”

Sisi ni Bibi-arusi Neno Wake Mkamilifu ambaye amedumu na Chakula Chake Kilichohifadhiwa. Hakuna haja ya kulialia tena, tunanena tu Neno na kusonga mbele, kwa kuwa sisi NI Neno.

Hakuna kitu cha kuhofia. Hakuna haja ya mikutano ya maombi ya usiku kucha kufunua sisi ni nani, Neno limekwishafunuliwa kwetu. Tunajijua sisi ni nani, kama vile yeye nabii wa Mungu, naye tayari amekwishatuambia ni nani ambaye angekwenda.

Kila mmoja wetu! Hata kama wewe ni mke wa nyumbani, ama u yaya mdogo, ama hata kama wewe ni mama kizee, ama kijana mwanamume, ama cho chote kile, tutaenda kwa vyo vyote. Hamna hata mmoja wetu atakayeachwa nyuma.” Amina. “Kila mmoja wetu ataenda. Hatutazuiwa na kingine chochote.”

Nena kuhusu kutupa IMANI ya Kunyakuliwa!!!

Njooni muungane na sehemu ya Bibi-arusi wa Mungu tunapokusanyika pamoja kwenye Sauti ya Mungu iliyothibitishwa, anaponena na kutuambia: Kipenzi Changu, Mteule Wangu, Bibi-arusi Wangu, Mbona Unalialia, Nena, na usonge mbele.

Ndugu. Joseph Branham

Ujumbe: 63-0714M Mbona Unalialia? Nena!

Saa: 06:00 MCHANA, Saa za Jeffersonville (ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki)

Mahali:

Bali kuna Kanisa moja tu halisi, hujiungi nalo; unazaliwa ndani yake. Waona? Na iwapo umezaliwa ukiwa ndani yake, Mungu Aliye Hai hutenda kazi kwako, akijifanya Mwenyewe ajulikane. Waona? Humo ndimo Mungu anamoishi, Kanisani Mwake. Mungu huenda Kanisani kila siku__huishi Kanisani, Yeye huishi ndani yako. Wewe ni Kanisa Lake. Wewe ni Kanisa Lake. Wewe ni hekalu anamoishi Mungu. Wewe binafsi ni Kanisa la Mungu Aliye Hai.