25-0727 Unyakuo

UJUMBE: 65-1204 Unyakuo

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Bibi-arusi Wa Bila Masharti,

Bwana alitupa wakati mzuri sana kambini wiki iliyopita alipotufunulia Neno Lake. Alithibitisha, kwa Neno Lake, ya kwamba Yakini yetu ni: Neno Lake, Ujumbe Huu, Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda; wote ni mmoja, Yesu Kristo ni yeye yule jana, leo na hata milele. 

Tulisikia jinsi ambavyo shetani anavyojaribu kuutenganisha Ujumbe kutoka kwa mjumbe, lakini Bwana Yesu asifiwe, Mungu Mwenyewe alinena kupitia malaika Wake Mwenye nguvu na kutuambia:

Tunaona ya kwamba mtu anapokuja, ametumwa kutoka kwa Mungu, amechaguliwa na Mungu, akiwa na BWANA ASEMA HIVI ya kweli, ujumbe huo na mjumbe huyo ni mmoja na kitu kimoja. Kwa sababu yeye ametumwa kuwakilisha BWANA ASEMA HIVI, Neno kwa Neno, kwa hiyo yeye pamoja na ujumbe wake ni mmoja.

Huwezi kuutenganisha Ujumbe na mjumbe, wao ni kitu kimoja, BWANA ASEMA HIVI. Haijalishi kile mpakwa mafuta yeyote wa uongo anachosema, Mungu alisema wao ni mmoja na hawawezi kutenganishwa.

Kisha akatuambia hatuhitaji tambara la chujio ili kuwashika wadudu wowote wakati tunapozisikiliza kanda, kwa maana hakuna wadudu ama utomvu wa mdudu katika Ujumbe Huu. Ni kisima Chake kinachofoka maji ambacho daima kinatiririka kisafi na cheupe. Hububujika daima, hakikauki kamwe, kinaendelea tu kusukuma na kusukuma, kikitupa Ufunuo zaidi na zaidi wa Neno Lake.

Yeye alitukumbusha KAMWE TUSISAHAU kwamba agano Lake na sisi ni lisilopingika, halibadiliki, lakini zaidi ya yote, halina Masharti.

Iwe ni upendo, usaidizi au kujisalimisha, ikiwa jambo lisilo na masharti ni YAKINI nalo halijatii sheria na masharti yoyote maalum: litatendeka bila kujali ni nini kingine kitakachotokea.

Kisha akataka kuushindilia msumari, kwa hivyo akatuambia kwamba leo hii Maandiko Yake yanatimizwa mbele ya macho yetu.

J-u-a lile lile lipambazukalo mashariki ndilo j-u-a lile lile litualo magharibi. Na M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyetokea mashariki na kujithibitisha Mwenyewe kama Mungu aliyefanyika mwili ndiye M-w-a-n-a yule yule wa Mungu aliyeko katika kizio cha magharibi cha dunia ambaye anajitambulisha Mwenyewe kati ya kanisa usiku huu, Yeye yule jana, leo, na hata milele. Ile Nuru ya jioni ya Mwana imekuja. Leo Maandiko haya yametimia mbele yetu.

Yule Mwana wa Adamu amekuja tena katika mwili wa mwanadamu katika siku yetu, kama vile tu Yeye alivyoahidi angefanya, kumwita Bibi-arusi atoke. Ni Yesu Kristo akizungumza nasi moja kwa moja, na haihitaji fasiri yoyote ya mwandamu. Kitu pekee tunachohitaji, kitu pekee tunachotaka, ni Sauti ya Mungu inayonena kwenye kanda kutoka kwa Mungu Mwenyewe.

Ni ufunuo wa dhihirisho la Neno likifanywa halisi. Nasi tunaishi katika siku hiyo; Mungu asifiwe; Ufunuo wa siri ya Yeye Mwenyewe.

Ni wakati mtukufu jinsi gani Bibi-arusi aliyonao, akiwa amekaa kwenye uwepo wa Mwana, akiivishwa. Ngano imeirudia ngano tena, na hakuna chachu miongoni mwetu. Ni Sauti ya Mungu safi tu ikinena nasi, ikitufinyanga na kutufanya kuwa sura ya Kristo, aliye Neno.

Sisi ni wana na binti za Mungu, sifa Yake ile aliyoichagua tangu zamani ije katika wakati huu, wakati ulio mkuu sana katika historia ya ulimwengu.  Yeye alijua sisi hatungeshindwa, hatungepatana, bali tungekuwa Bibi-arusi Neno Wake mkweli na mwaminifu, Uzao Wake Mkuu wa Kifalme wa Ibrahimu ulioahidiwa ambao ungekuja.

Unyakuo umekaribia. Wakati umefika mwisho. Yeye anakuja kumchukua Bibi-arusi Wake ambaye amejiweka mwenyewe tayari bali amekaa kwenye Uwepo wa Mwana, akiisikia Sauti Yake ikimvika Bibi-arusi Wake. Hivi karibuni tutaanza kuwaona wapendwa wetu walioko ng’ambo ya pazia la wakati, ambao wanatungojea na kutamani sana kuwa pamoja nasi.

Kanda ndiyo njia iliyoandaliwa na Mungu ya kumkamilisha Bibi-arusi Wake. Kanda hizi ndicho kitu pekee kitakachomuunganisha Bibi-arusi Wake. Kanda hizi ndiyo Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake.

Ninawalika mje muungane nasi, sehemu ya Bibi-arusi Wake, Jumapili hii saa 6:00 MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia kila kitu kuhusu kile kinachokaribia kutukia hivi karibuni: Unyakuo 65-1204. 

 
Ndugu. Joseph Branham