25-0413 Muhuri Wa Tano

UJUMBE: 63-0322 Muhuri Wa Tano

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Wapumzikao,  

Tumewasili. Tumefika. Kule Kuthibitishwa kwa Neno kumethibitisha ya kwamba Ufunuo wetu wa Ujumbe Huu unatoka kwa Mungu. Tuko katika MAPENZI Yake MAKAMILIFU kwa kudumu na Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. 

Kubonyeza Play ni muhimu jinsi gani? Maneno tunayosikia kwenye kanda ni muhimu sana, matakatifu sana, hivi Mungu Mwenyewe hata asingeweza kumwamini kumpa hayo Malaika…hata kwa mmoja wa Malaika Wake wa Mbinguni. Ilibidi yafunuliwe na kuletwa kwa Bibi-arusi Wake na nabii Wake, kwa maana huyo ndiye Neno la Mungu humjia, nabii Wake, PEKE YAKE.

Mungu aliichana ile Mihuri, akaikabidhi kwa malaika-mjumbe Wake wa saba wa duniani, na kumfunulia Kitabu chote cha Ufunuo. Kisha, Mungu akanena kupitia malaika Wake wa duniani na kufunua KILA KITU kwa Bibi-arusi Wake. 

Kila maelezo madogo yamenenwa na kufunuliwa kwetu. Mungu ametujali sana hivi kwamba Yeye hakutuambia tu mambo ambayo yametukia hapa duniani tangu mwanzo wa wakati, bali alinena kupitia malaika Wake na kutuambia mambo yanayoendelea katika mahali kama paradiso sasa hivi.

Yeye hakutaka tuhangaike, ama tusiwe na hakika juu ya kile wakati ujao unachoshikilia kwa ajili yetu wakati tuiachapo maskani hii ya kidunia. Kwa hiyo, Mungu Mwenyewe alimchukua malaika Wake wa saba mwenye nguvu ng’ambo ya pazia la wakati, kusudi aweze kuliona, kulihisi, hata azungumze nao kule ng’ambo. Haikuwa ono, alikuwepo KULE.  

Mungu alimpeleka huko ili yeye aweze kurudi na kutuambia: “Nilikuwa huko, nililiona. Linatukia SASA HIVI… Mama zetu, baba zetu, kaka zetu, dada zetu, wanetu, mabinti zetu, wake, waume, babu, Musa, Eliya, WATAKATIFU ​​WOTE ambao waliotangulia huko wamevalia mavazi meupe, wakipumzika na wakitungojea SISI”.

Hatutalia tena, maana Itakuwa ni furaha tupu. Hatutakuwa na huzuni tena, maana itakuwa furaha tupu. Hatutakufa kamwe, maana yote ni Uzima mtupu. Hatuwezi kuzeeka, maana sote tutakuwa vijana milele.  

Ni ukamilifu…kuongeza ukamilifu…kuongeza ukamilifu, nasi tunakwenda huko!! Na kama vile Musa, hatutaacha hata ukwato, SOTE TUNAKWENDA…FAMILIA YETU YOTE.

Ni muhimu jinsi gani KUMPENDA huyo malaika wa saba mwenye nguvu? 

Nayo ikalia, ikasema, “Vyote ulivyowahi kupenda…” thawabu ya huduma yangu. Sihitaji thawabu yo yote. Akasema,“Vyote ulivyowahi kupenda, na wote waliowahi kukupenda,Mungu amekupa.

Hebu tulisome hilo tena tafadhali:  Amesema nini?….Mungu amekupa WEWE!! 

Nasi tutaungana nao na kupaza sauti, “Tunategemea Jambo Hilo”

Tumekitegemeza kikomo chetu cha milele juu ya nini? KILA NENO LILILONENWA KWENYE KANDA. Ninamshukuru sana Bwana kuwa ametupa Ufunuo wa Kweli kwamba Kubonyeza Play ndilo jambo lililo MUHIMU SANA ambalo Bibi-arusi analopaswa kufanya.

Je! ungependa kupumzika pamoja nasi? Njoo uungane nasi Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) tunaposikia yote yahusuyo wakati ujao unachoshikilia, wapi tunakoenda, na jinsi ya kufika huko, tunaposikia Sauti ya Mungu ikinena na kuufungua:   Muhuri Wa Tano 63-0322.

Ndugu. Joseph Branham
    

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Danieli 9:20-27
Matendo 15:13-14
Warumi 11:25-26
Ufunuo 6:9-11 / 11:7-8 / 22:8-9