25-0330 Muhuri Wa Tatu

UJUMBE: 63-0320 Muhuri Wa Tatu

PDF

BranhamTabernacle.org

Mpendwa Hawa Wa Kiroho,

Hebu niianze barua yangu leo ​​na bomu la atomiki la Mungu; si bunduki aina ya 22, BOMU LA ATOMIKI kwa Bibi-arusi wa Yesu Kristo.

Sasa, kama unataka kuandika mambo hayo; bila shaka, nyote mnayajua: Yesu, Yohana 14:12; na Yoeli, Yoeli 2:38; Paulo, Timotheo wa Pili 3; Malaki, mlango wa 4; na Yohana mfunuzi, Ufunuo 10, kumi na saba, moja hadi kumi na saba. Unaona, ni vile vile ambavyo ingetukia sasa!

Notisi na onyo: Nukuu ifuatayo si kwa ajili yako ikiwa wewe unaamini.

“Tunamwelezea sana nabii wa Mungu.” “Huwezi kuwa Bibi-arusi ikiwa tu unamsikiliza nabii.” “Kuzicheza kanda kanisani ni kosa.” “Mwenge umepitishwa; jambo lililo muhimu zaidi leo ni kuwasikiliza wahudumu.” “Kubonyeza play wote kwa wakati mmoja ni dhehebu.”

Kwa kanisa, ni Kitu gani? Neno lililofanyika mwili likifanywa mwili miongoni mwa watu Wake tena! Unaona?

KABUUM…Kwa hivyo kwa kubonyeza play, tunaweza kulisikia Neno lililofanyika mwili, likinena nasi mdomo kwa sikio anapolifunua Neno Lake.

Na mtu fulani anaweza kusema ati Sio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI UNAYOPASWA KUISIKIA? Sehemu hii ya nukuu ni kwa ajili yako.

Nao hawaliamini Hilo kamwe.

Kadiri Bwana anavyozidi kutupa sisi Ufunuo zaidi wa Neno Lake, na sisi ni nani, ndivyo kila mtu aliye nje ya Ufunuo huo anavyozidi kuwa mbali zaidi.

Hebu niseme jambo hilo, vizuri hasa, ili mninii… litadidimia ndani sana. Ninataka hili lilipatie hasa. Hiyo ndiyo shida yenu leo, mnaona, hamlijui Neno! Mnaona?

Mungu anao watu waliotiwa mafuta kuhubiri Ujumbe Huu, lakini kuna Yakini moja tu: Neno. Unapomsikia mhudumu, au mtu ye yote akinena, ni lazima uwe na imani ya kuamini kuwa anachokisema ndicho HASA ambacho nabii wa Mungu alichokwisha sema. Neno lao, ufunuo wao, fasiri yao inaweza kushindwa; Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda HAIWEZI KUSHINDWA KAMWE.

Nena kuhusu Mungu katika urahisi kwa kubonyeza play…Yeye analisema TENA.

Wanapitwa Naye, Neno lililo hai lililodhihirishwa katika mwili, kwa Neno lililoahidiwa. Neno liliahidi kufanya mambo haya. Ahadi ilifanywa, ya kwamba itakuwa hivi katika siku za mwisho.

Sikiliza Ngurumo Yake. Ngurumo ni Sauti ya Mungu. William Marrion Branham ndiye Sauti ya Mungu kwa kizazi hiki.

Bi-Bibi arusi hajawa na uamsho bado. Mnaona? Hakujakuwako na uamsho humo, hakujakuwako na madhihirisho ya Mungu kumwamsha Bibi-arusi bado. Mnaona? Tunautarajia huo sasa. Itahitaji hizo Ngurumo Saba zisizojulikana kule nyuma, kumwamsha Yeye tena, unaona. Naam. Yeye atazituma. Aliliahidi. Sasa angalia.

Unaweza kulipindisha hilo ukipenda, lakini zile Ngurumo Saba zitampa Bibi-arusi changamko kwa Ufunuo na imani ya kunyakuliwa, ambayo huja tu kwa Roho Mtakatifu akizungumza kupitia nabii wa Mungu. Hilo linatendeka SASA HIVI ulimwenguni kote. Mungu amemchangamsha Bibi-arusi Wake na Neno Lake.

Si hivyo tu, bali tayari Yeye amekwisha mwambia adui yetu la kufanya.

Usiwaguse. Wao wanajua wanakoenda, kwa maana wametiwa Mafuta Yangu. Na kwa kutiwa kwa Mafuta Yangu, wao wana divai ya furaha, maana wanajua Neno Langu la ahadi, ‘Nitawafufua tena.’ Usidhuru Hao! Usiende ukajaribu kuwachafua.

Yeye amemwambia adui yetu aiondoe mikono yake michafu mbali nasi. Lakini je! ugonjwa bado ungali unaweza kutushambulia? Ndiyo. Je! bado tungali tunayo matatizo? Ndiyo. Lakini Yeye pia alituambia la kufanya.

Ni la kilindi. Lisome polepole na mara tena na tena.

Kabla ya kuwa Neno, ni wazo. Nalo wazo halina budi kuumbwa. Vema. Kwa hiyo, mawazo ya Mungu yakawa uumbaji wakati yaliponenwa, kwa Neno. Hapo ndipo wakati anapoyaleta kwa—kwako kama wazo, wazo Lake, nalo linafunuliwa kwako. Halafu, lingali ni wazo mpaka wewe utakapolinena.

Mawazo Yake yakawa uumbaji wakati yaliponenwa. Kisha, mawazo Yake yaliletwa na kufunuliwa kwetu kama Neno. Sasa lingali ni wazo kwetu mpaka tutakapolinena. KWA HIYO TUNAYANENA… NA KUYAAMINI.

Mimi ni Uzao wa Kifalme wa Ibrahimu. Mimi ni Bibi-arusi wa Kristo. Niliteuliwa na kuchaguliwa tangu zamani kabla ya kuwekwa misingi ya ulimwengu kuwa Bibi-arusi Wake, na hakuna kitu kinachoweza kulibadili hilo. Kila ahadi katika Biblia ni yangu. Ni Neno Lake kwangu. Mimi ni mrithi wa Ahadi yenyewe. Yeye ndiye Bwana Mungu aniponyaye magonjwa yangu yote. Chochote ninachokihitaji ni changu, Mungu alisema hivyo.

Mungu katika Urahisi: Imani huja kwa kusikia, kulisikia Neno. Neno huja kwa nabii.

Kila mtu anataka kuzitumia “NUKUU” kuthibitisha mawazo yao, mafikara yao, ujumbe wao. Nao wako sahihi, nafanya vivyo hivyo na mimi, ndio maana yote niwapayo ni nukuu za kuwaambia: Dumuni na Kanda. Isikilizeni hiyo Sauti. Sauti hiyo ni Sauti ya Mungu. Hamna budi kuamini kila Neno lililo kwenye Kanda, si yale mtu mwingine yeyote asemayo. Hiyo Sauti NDIO SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI MNAYOPASWA KUISIKIA.

Wengine huzitumia nukuu kuwaleta ninyi kwenye huduma yao, kwenye kanisa lao, kwenye fasiri zao, ufunuo wao. “Dumuni na mchungaji wenu.” (Vema, ninaipenda hiyo pia, kwa sababu sisi tunadumu naye, ila tu mchungaji tofauti.) “Yeye siye changarawe pekee ufukoni.” “Yeye hakusema kamwe kuzicheza kanda kanisani.”

Usiweke fasiri yo yote ya kibinafsi Kwake. Yeye anataka Neno lililo safi, lisiloghoshiwa, hata ubembe wo wote usiwepo. Singetaka mke wangu afanye ubembe na mwanamume mwingine. Na unapoanza kusikiliza hoja za namna yo yote, zaidi ya Hilo, unasikiliza, unafanya ubembe na Shetani. Amina! Hilo halikufanyi ujisikie kubarikiwa? Mungu anakutaka ubakie msafi kabisa. Udumu daima hapo na Neno hilo. Dumu Nalo. Vema.

Mimi na nyumba yangu, tutabonyeza play na kulifuata Neno la Mungu lililofanyika Mwili linenalo kupitia malaika-mjumbe Wake wa saba. Hatutaongeza fasiri yetu ya kibinafsi Kwake; hatutabembana au kusikiliza hoja yoyote. TUTADUMU NA NENO HILO KAMA LILIVYONENWA KWENYE KANDA. Ni Mungu katika Urahisi.

Ni wakati mtukufu jinsi gani tutakaokuwa nao Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) Tusikiapo: Muhuri Wa Tatu 63-0320. Ningependa kuwaalika mje mkaungane nasi tunapoungana katika Neno la leo.

Ndugu. Joseph Branham

Maandiko ya kusoma kabla ya kusikiliza Ujumbe:

Mathayo mt. 25:3-4
Yohana Mt. 1:1, 1:14, 14:12, 17:17
Matendo Sura ya 2
I Timotheo 3:16
Waebrania 4:12, 13:8
1 Yohana 5:7
Mambo ya Walawi 8:12
Yeremia Sura ya 32
Yoeli 2:28
Zekaria 4:12

Hebu nichukue fursa hii kuliweka wazi kwa mara nyingine tena. Mimi sipingani na huduma tano. Ninaamini katika huduma tano. Sioni ni vibaya kumsikiliza mhudumu. Naamini unapaswa kumsikiliza mchungaji wako pale ambapo Mungu amekuweka. Nisemalo ni kwamba, Ninaamini Mungu alimtuma nabii katika siku yetu. Mungu alilifunua Neno Lake kwa nabii Wake. Mimi naweza kukosea, mchungaji wako anaweza kukosea, lakini LAZIMA tukubaliane (tukisema tunauamini UJUMBE HUU ni kweli na Ndugu Branham ni nabii wa Mungu) yale yaliyosemwa kwenye kanda ni Bwana Asema Hivi. Kama huamini hilo, basi wewe huamini Ujumbe huu. Hivyo, Mimi ninaamini ndio SAUTI ILIYO MUHIMU ZAIDI UNAYOPASWA KUISIKIA. Huhitaji kunisikia mimi, huhitaji kumsikia mtu mwingine yeyote, lakini LAZIMA UISIKIE SAUTI HIYO ILIYO KWENYE KANDA.