25-0323 Muhuri Wa Pili

UJUMBE: 63-0319 Muhuri Wa Pili

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa wasikilizaji Wa Kanda,

Swali: Je! tuko katika Mapenzi Yake makamilifu kwa kuzicheza Kanda?
Jibu: NDIYO.

Swali: Je! Bibi-arusi anahitaji zaidi ya yale yaliyosemwa kwenye Kanda?
Jibu: HAPANA.

Swali: Je! tunakosa kitu kwa sisi kusikiliza Kanda TU?
Jibu: HAPANA.

Swali: Je! tunaweza kuwa Bibi-arusi kwa kusikiliza Kanda TU?
Jibu: NDIYO, KWA MSISITIZO ZAIDI!

Sasa kumbukeni, “Hakuna lo lote linaloweza kufunuliwa; Mungu hatafanya neno lo lote, hata kidogo, mpaka kwanza alifunue kwa watumishi Wake, manabii.”

Hivyo, YOTE tunayohitaji yamekwisha nenwa na yako kwenye kanda; au, wakati malaika Wake wa saba atakaporudi duniani, YEYE atatuambia basi.

Loo! Bibi-arusi, hebu na tuwazie kile kinachotendeka miongoni mwa Bibi-arusi wa Kristo ulimwenguni kote. Baba anamkusanya Bibi-arusi Wake pamoja kwa Sauti Yake Naye Ananguruma, “Bwana Asema Hivi.”

Kumbukeni, alituambia zile Ngurumo zilikuwa kitu gani: “sauti kuu ya kishindo cha Ngurumo ni Sauti ya Mungu”. Nayo Sauti ya Mungu kwa Bibi-arusi ni nini? Malaika-mjumbe wa saba wa Mungu, William Marrion Branham.

Yeye alisema kunakuja Ngurumo saba za siri ambazo hata hazijaandikwa kamwe. Na ya kwamba kupitia Ngurumo hizo Saba, zitamkusanya Bibi-arusi pamoja kwa ajili ya kupata imani ya kunyakuliwa.

Neno la Bwana huwajia manabii Wake. Kama angekuwa na utaratibu bora zaidi, angeliutumia. Yeye alichagua utaratibu bora zaidi ya wote hapo mwanzo Naye hawezi, na hatabadilika.

Kwa hiyo, Sauti ya Mungu, inayonena kupitia malaika Wake wa saba, inamkusanya Bibi-arusi Wake pamoja na kutupa Imani ya Kunyakuliwa.

Kanisa halijashangaa tangu mwaka wa 1933, kule chini mtoni siku ile, ya kwamba William Marrion Branham ndiye Sauti ya Mungu, Inayonguruma, “Bwana Asema Hivi,” naye alitumwa kumwita, kumkusanya, na kumwongoza Bibi-arusi.

Ningependa kuwaalika mje msikilize pamoja nasi Jumapili saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) wakati Bwana wetu Yesu anapokifungua kile Kitabu, kuuvunja huo Muhuri, na kuutuma duniani, kwa malaika Wake wa saba, atufunulie huo SISI!

Ndugu. Joseph Branham

Tarehe: Jumapili, 23 Machi, 2025

Ujumbe: Muhuri wa Pili 63-0319

Muda: Saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki)

Maandiko ya kusoma kabla ya kuusikiliza Ujumbe:

Mathayo Mt. 4:8 /11:25-26 / 24:6
Marko Mt. 16:16
Yohana Mt. 14:12
2 Wathesalonike 2:3
Waebrania 4:12
Ufunuo 2:6 / 6:3-4 / Sura ya 17 / 19:11-16
Yoeli 2:25
Amosi 3:6-7