UJUMBE: 63-0318 Muhuri Wa Kwanza
- 25-0316 Muhuri Wa Kwanza
- 23-0723 Muhuri Wa Kwanza
- 22-0130 Muhuri Wa Kwanza
- 21-0124 Muhuri Wa Kwanza
- TAI WANAKUSANYIKA PAMOJA
- 19-0331 Muhuri Wa Kwanza
- 17-0325 Muhuri Wa Kwanza
Kipenzi Malkia wa Mbinguni,
Ninayo mengi sana kwa ajili yako Jumapili hii. Kwanza, utasikia kishindo cha Ngurumo. Itakuwa Sauti Yangu, Sauti ya Mungu ikinena nawe, Bibi-arusi Wangu. Nitakuwa nikikufunulia wewe Neno Langu zaidi ya hapo awali. Utaniona Mimi, yule Mwana-Kondoo aliyelowa damu ambaye aliyechinjwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu, nikikitwaa na kukifungua kile Kitabu, na kuichana ile Mihuri, na kukituma duniani, kwa malaika-mjumbe Wangu wa saba, William Marrion Branham, kuwafunulia NINYI siri ambazo zimefichwa tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu!
Kutakuwa na vigelegele, vifijo, na zile haleluya kutoka kote ulimwenguni wakati nizungumzapo nawe. Simba atakuwa akinguruma; watiwa mafuta, nguvu, utukufu, dhihirisho haitaelezeka. Wewe, Malkia Wangu, utakuwa umeketi pamoja katika ulimwengu wa roho Nikisema nawe na kukupa Imani ya kunyakuliwa.
Kumbuka, huna budi kuwa na hiyo Imani waliokabidhiwa watakatifu mara moja. Nilikuambia, lazima umsikilize malaika Wangu Niliyekutumia.
Yeye “atairudisha Imani ya watoto ielekee baba zao.” Ile imani asili ya Biblia itarudishwa na malaika wa saba.
Neno Langu linakuambia, katika siku za Sauti ya malaika wa saba, kupiga kwake baragumu, kupiga baragumu ya Injili; anapaswa kumaliza siri zote za Mungu. Hakuwezi kuwa na kitu hata kimoja chakuongezwa na hakuna kitu chakuondolewa kutoka kwenye yale niliyosema kwenye kanda; wewe sema tu kile Nilichosema Mimi kupitia malaika-mjumbe Wangu. Ndio maana niliirekodi, ili uweze tu KUBONYEZA PLAY na kusikia hasa kile nilichosema, na jinsi Nilivyosema. Itakupa Imani ya Kunyakuliwa.
Malkia Wangu kipenzi, Machoni Pangu, wewe ni mkamilifu, huna dhambi kabisa mbele Zangu. Usijali, HUTAPITIA katika ile dhiki; kwa kuwa umeikubali Damu Yangu, Neno Langu, malaika Wangu, Sauti Yangu, hivyo huna dhambi kabisa mbele Zangu.
Ninayo mambo makubwa sana niliyokutunzia. Unaliona Neno Langu likifunuliwa mbele ya macho yako kila siku. Nimekuwa nikiziweka ishara angani kukuambia wewe jambo fulani liko karibu kutukia. Ninakuja, jiandae. Liweke Neno Langu, Sauti Yangu, kuwa ya kwanza katika maisha yako.
Weka kila kitu kando, hakuna kitu kilicho muhimu zaidi kuliko Neno Langu. Najua adui anajaribu kukuangusha chini, lakini nilikuahidi nitakuinua. Mimi nipo pamoja nawe, hata NDANI YAKO. Wewe na Mimi tunakuwa Mmoja ninapokufunulia Neno Langu. Unajua moyoni mwako, wewe ndiwe Bibi-arusi Malkia Wangu. Unajua nilikuchagua tangu awali. Unajua Nakupenda. Unajua Niko pamoja nawe kila sekunde ya kila siku. Unajua SITAKUACHA KAMWE.
Tutakuwa na wakati mzuri sana pindi Ninapokufunulia zaidi kila Jumapili, kila siku, unaponisikia Mimi nikinena kila Jumapili, Nikinena nawe kupitia malaika Wangu. Huenda wengine wasielewe au kuona kile wewe unachokiona, lakini Imetia nanga ndani ya moyo wako kwamba hii ndiyo Njia Yangu niliyoiandaa.
Ni kimbilio lililoje nililokuwekea. Unaweza kwa urahisi tu Bonyeza Play wakati wowote, mchana au usiku, kunisikia Mimi nikinena nawe. Nitailetea faraja nafsi yako wakati ninapolifunua Neno Langu na kukuambia wewe ni nani. Kila Ujumbe ni kwa ajili yako, na kwa ajili yako peke yako. Tunaweza kushiriki na kuabudu pamoja wakati wowote unapotaka.
Jumapili saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) sehemu ya Bibi-arusi itakusanyika kutoka ulimwenguni kote kuzisikia siri hizi kuu zikifunuliwa. Ninawaalika mje mkaungane nasi tunaposikia, 63-0318 – “Muhuri Wa Kwanza”.
Ndugu. Joseph
Maandiko ya kusoma kwa ajili ya maandalizi ya kusikiliza Ujumbe:
Mathayo Mt 10:1 / 11:1-14 / 24:6 / 28:19
Yohana 12:23-28
Matendo 2:38
2 Wathesalonike 2:3-12
Waebrania 4:12
Ufunuo 6:1-2 / 10:1-7 / 12:7-9 / 13:16 / 19:11-16
Malaki Sura ya 3 na 4
Danieli 8:23-25 / 11:21 / 9:25-27