25-0309 Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

UJUMBE: 63-0317E Pengo Kati Ya Nyakati Saba Za Kanisa Na Ile Mihuri Saba

PDF

pakua – m4a

pakua – amr

BranhamTabernacle.org

Wapendwa Waliorejeshwa,

Sichoki kamwe kuisikia Sauti ya Mungu ikituambia sisi ni nani, wapi tunatoka, wapi tunakwenda, sisi ni warithi wa nini, na jinsi gani Yeye anavyotupenda.

Ukuhani wa kiroho, taifa la kifalme, wanaomtolea Mungu dhabihu za kiroho, matunda ya midomo yao, wakilisifu Jina Lake.” Ni watu wa—wa ajabu jinsi gani! Yeye anao.

Faraja na amani yetu pekee huja kwa kuisikia Sauti ya Mungu ikinena nasi, kisha tunamjibu Baba kwa kutoa dhabihu za kiroho kwa matunda ya midomo yetu, tukilisifu Jina Lake.

Ulimwengu wote huu unaugua. Maumbile yanaugua. Tunaugua na kungojea kule kuja kwa Bwana. Dunia hii haina kitu kwetu sisi. Tuko tayari kuondoka na kwenda kwenye Karamu yetu ya Arusi na Makao ya Baadaye pamoja Naye na wale wote ambao tayari wako Huko, ng’ambo tu ya pazia la wakati, wakitungojea.

Hebu na tuamke na tujitikise! Tufinye dhamiri zetu, tuamke kwa kile kinachoendelea sasa hivi na kile kinachoenda kutukia katika dakika moja kufumba na kufumbua jicho.

Kamwe katika historia ya ulimwengu haijawahi kuwezekana kwa Bibi-arusi wa Kristo kuungana kutoka ulimwenguni kote, wote kwa wakati ule ule mmoja, kuisikia Sauti ya Mungu ikinena na kulifunua Neno Lake kwa Bibi-arusi Wake.

Enyi Waaminio, jiulizeni wenyewe, ni sauti gani, mhudumu gani, ni mtu gani anayeweza kumuunganisha na kumkusanya Bibi-arusi wa Kristo wote pamoja? Kama wewe ni Bibi-arusi wa Kristo, unajua kwa urahisi hakuna kabisa Sauti nyingine ila Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda.

Ndiyo, Roho Mtakatifu yu ndani ya kila mmoja wetu, kila ofisi ya kanisa, lakini Mungu Mwenyewe alituambia angeuhukumu ulimwengu kwa Neno Lake. Bibi-arusi anajua Neno Lake huja kwa nabii Wake. Nabii Wake ndiye mfasiri PEKEE wa Kiungu wa Neno Lake. Kile asemacho hakiwezi kuongezewa lolote wala kuondolewa kitu. Ni Neno, lililo kwenye kanda, ndilo sisi sote tutakalohukumiwa kwalo, na wala si neno lingine ama fasiri ya Neno hilo.

Haiwezekani kwa sauti nyingine yoyote kumuunganisha Bibi-arusi. Ni Sauti ya Mungu peke yake iliyo kwenye kanda ndio inayoweza kumuunganisha Bibi-arusi Wake. Ndilo Neno pekee ambalo Bibi-arusi wanaloweza kukubaliana kwalo. Ndio Sauti pekee ambayo Mungu Mwenyewe aliithibitisha kuwa Sauti Yake kwa Bibi-arusi Wake. Bibi-arusi Wake lazima awe katika Nia Moja na Moyo Mmoja ili kuwa pamoja Naye.

Wahudumu wanaweza kuhudumu, waalimu wanaweza kufundisha, wachungaji wanaweza kuchunga, lakini Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda lazima iwe ndio Sauti iliyo muhimu zaidi wanayopaswa kuiweka mbele ya watu. Ndio Yakini ya Bibi-arusi.

Ikiwa unao Ufunuo wa jambo hilo, basi hiki ndicho kitakachoenda kutukia.

Neno linatuambia Adamu alipoteza urithi wake, dunia. Ulitoka mkononi mwake ukaenda kwa yule aliyemwuzia, Shetani. Aliuza imani yake katika Mungu, akachukua hoja za Shetani. Akapoteza kila kitu kikaenda kwenye mikono ya Shetani. Aliutoa mkononi mwake akampa Shetani.

Mungu ni Mungu wa ulimwengu, kila mahali. Lakini mwanawe alikuwa na mamlaka juu ya dunia hii. Angeweza kunena, aliweza kutoa majina, aliweza kusema, aliweza kusimamisha maumbile, aliweza kufanya lo lote alilotaka kufanya. Alikuwa na mamlaka makamilifu juu ya dunia.

Adamu alipoteza yote, lakini utukufu kwa Mungu, yote yeye aliyopoteza na kuachilia yamekombolewa na Mkombozi wetu aliye Jamaa wa Karibu, si mwingine ila Mungu Mwenyezi, ambaye alifanyika Imanueli, mmoja wetu. SASA, NI YETU.

Sisi ni wana na binti Zake watakaotawala na kuwa wafalme na makuhani pamoja Naye. Tunao uzima wa milele pamoja Naye na wale wote tuwapendao. Hakuna magonjwa tena, hakuna huzuni tena, hakuna kifo tena, yote ni milele tu pamoja.

Tunapoliwazia hilo, tunawezaje kumwacha shetani atushushe? Ni YETU, huko ndiko tunakoelekea hivi karibuni. Yeye ametupa jambo lililo kuu zaidi awezalo kutupa. Siku hizi chache za mitihani na majaribu hapa duniani zinamezwa kwa haraka na USHINDI wetu MKUU ULIO SIKU CHACHE TU ZIJAZO MBELE YETU.

IMANI yetu haijawahi kuwa kubwa jinsi hii. Furaha yetu haijawahi kuwa juu jinsi hii. Tunajua sisi ni nani na ni wapi tunakoenda. Tunajua tuko katika Mapenzi Yake makamilifu kwa kudumu na Neno Lake. Yote tunayohitaji kufanya ni kudumu na kanda na kuamini kila Neno; si kulielewa lote, BALI KUAMINI KILA NENO…nasi TUNAAMINI!

Imani huja kwa kusikia, kulisikia Neno. Neno huja kwa nabii. Mungu alilinena Hilo. Mungu alilirekodi Hilo. Mungu alilifunua Hilo. Tunalisikia Hilo. Tunaliamini Hilo.

Unaweza tu kuupata Ufunuo huu kwa kuisikia Sauti ya Mungu kwenye kanda.

“Yote yale ambayo Kristo atafanya wakati wa mwisho yatafunuliwa kwetu juma hili, katika ile Mihuri Saba, kama Mungu ataturuhusu. Unaona? Vema. Yatafunuliwa. Na kufunuliwa, wakati Mihuri hii inapovunjwa na kufunguliwa kwetu, ndipo tunaweza kuona mpango huu mkubwa wa ukombozi ulivyo, na ni lini na ni vipi utafanyika. Yote yamefichwa katika Kitabu hiki cha siri hapa. Kimetiwa muhuri, kimefungwa kwa Mihuri Saba, na kwa hiyo Mwana-Kondoo Ndiye pekee Ambaye anaweza kuivunja.

Jumapili hii saa 6:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville, (Ni Saa 1:00 MOJA JIONI ya Afrika Mashariki) sehemu ya Bibi-arusi kutoka ulimwenguni kote watakuwa wakiisikiliza Sauti ya Mungu wote kwa wakati mmoja. Tutakuwa tukiivumisha mbingu kwa maombi yetu na kumwabudu. Ninawaalika mje muungane nasi tunaposikia: Pengo Kati ya Nyakati Saba za Kanisa na ile Mihuri Saba 63-0317E.

Tafadhali msisahau kuhusu mabadiliko ya masaa huko Jeffersonville wikendi hii.

Ndugu. Joseph Branham