Ujume: 62-1230E Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
- 25-0223 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
- 23-0625 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
- 22-0109 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
- 18-1230 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
- 16-1218 Hii Ndiyo Ishara Ya Mwisho, Bwana?
Mabwana Wapendwa,
Hii ndiyo, Ishara. Huu ndio, wakati wenyewe. Huu ndio, Ujumbe. Hili ndilo, Neno. Hii ndio, Sauti ya Mungu. Huyu ndiye, Mwana wa Adamu. Hii ndio, njia ya Mungu iliyoandaliwa. Huu ndio, mwisho wa wakati.
Hakuna nabii, hakuna mtume, kamwe, katika wakati wowote, aliyewahi kuishi katika wakati kama huu tunaoishi sasa. Imeandikwa mbinguni. Imeandikwa juu ya uso wa dunia. Imeandikwa katika kila gazeti. Huu ndio mwisho, ikiwa unaweza kusoma maandishi ya mkono.
Yeye aliye na sikio, na asikie yale Mungu aliyonena, na aliyorekodi, ili lisiwe neno langu, mawazo yangu, wazo langu, bali Sauti ya Mungu yenyewe ikimuelekeza Bibi-arusi Wake ni ipi njia Yake PEKEE kamilifu iliyoandaliwa kwa ajili ya siku hii.
Njoo usikilize anapotuambia na kutufunulia kwa maandiko, kwa maono, kwa fasiri ya ndoto, kudumu na Ujumbe, kudumu na kanda. Sema TU kilicho kwenye kanda.
Hakuna njia iliyo bora, wala njia iliyo ya hakika, kuliko kuisikia Sauti ya Mungu kutoka kwa Mungu Mwenyewe. Mungu alimwamuru Bibi-arusi Wake kwa kunena kupitia nabii Wake na kutuambia, BONYEZA PLAY, kwisha.
Linene Hilo, lihubiri Hilo, lishuhudie Hilo, na uuambie ulimwengu kuhusu Hilo, bali Yeye anatuambia kuna njia moja tu kamilifu iliyoandaliwa ya kumkamilisha Bibi-arusi: sikilizeni Sauti ya Mungu iliyo kwenye kanda. Ikiwa jambo fulani linakutatiza, cheza kanda. Ni lazima iwe ndio ya KWANZA, na Sauti iliyo muhimu zaidi ikupasayo kuisikia. Ndilo Neno Lake kamilifu aliloliweka kwenye kanda.
“Sasa linganisha hilo na zile nyingine, zile ndoto. Hili lilikuwa ono. Kile Chakula; Hiki hapa. Mahali penyewe ni hapa.
Sikiliza, kwa ndoto na maono, Chakula cha Bibi-arusi kiko wapi? Mahali penyewe ni wapi? Ujumbe wa Bibi-arusi uko kwenye kanda.
“Ninajisikia nyumbani hapa. Hapa ndipo panapofaa. Na kama ukiangalia, ndoto ile ilizungumzia jambo lile lile. Unaona, kilipo Chakula.
Ili kuhakikisha tumelipata, anatuambia kwa mara nyingine tena, kanda hizo ndicho Chakula cha Bibi-arusi.
“Wakati umekwisha.” Kama ndivyo ilivyo, hebu na tujiandae, marafiki, kumlaki Mungu wetu.
Naam, Bwana, hiyo ndiyo shauku ya mioyo yetu, ni kuwa tayari kukulaki Wewe, kuwa Bibi-arusi Wako. Tufanye nini Bwana? Njia Yako iliyoandaliwa ni ipi? Mpango Wako ni upi? Njia Yako kamilifu ni ipi? Ulitutumia nabii ambaye Ungeweza kunena kupitia yeye kutuambia sisi. Tafadhali tuelekeze.
“Kumekwisha wekwa chakula kingi sana sasa; hebu na tukitumie. Hebu na tukitumie sasa.
Mtu anawezaje kuwa kipofu? Yeye anatuambia nini cha kufanya: kuna chakula kingi sana kilichohifadhiwa kwenye kanda; kitumieni SASA. Haya ndio maagizo ya Mungu kwa Bibi-arusi Wake.
Ikiwa unadai unauamini Ujumbe huu, amini William Marrion Branham ndiye nabii-mjumbe wa Mungu aliyetumwa kumwita Bibi-arusi atoke; maisha yake yanatimiza maandiko yote yaliyonenwa kumhusu yeye; amini ndio Sauti ya Mungu ya siku hii, basi YEYE; Mungu, akinena kupitia nabii Wake, anamwambia Bibi-arusi kwa Kiingereza kilicho wazi nini cha kufanya.
Ingawa tunadhihakiwa, tunateswa, na kudharauliwa kwa sababu tu tunasikiliza kanda, tunafanya yale hasa Yeye aliyotuambia sisi tufanye. Asante Bwana kwa Ufunuo.
Ninataka kuualika ulimwengu mzima kuungana nasi Jumapili hii saa 06:00 SITA MCHANA, saa za Jeffersonville,(Ni saa 2 MBILI USIKU ya Afrika Mashariki), wakati tunaposikia: “Hii Ndiyo Ishara ya Mwisho, Bwana?” Tutasikia kila kitu kuhusu:
Ngurumo, Mihuri Saba, Mwamba wa Piramidi, Chakula cha Kiroho, Umilele, Kundi la Malaika, Makao Makuu Yangu, Ono, Ndoto, Unabii, Siri Zilizofichwa, Andiko baada ya Andiko.
Hakuna jambo lililo kuu katika maisha haya kuliko kuisikia na kuitii Sauti ya Mungu.
Ndugu. Joseph Branham
Maandiko:
Malaki Sura ya 4
Mathayo 13:3-50
Warumi 9:33 / 11:25 / 16:25
1 Wakorintho 14:8 / Sura ya 15
Wagalatia 2:20
Waefeso 3:1-11 / 6:19/ 5:28-32
Wakolosai 4:3
1 Wathesalonike 4:14-17
1 Timotheo 3:16
Waebrania 13:8
2 Petro 2:6
Ufunuo 1:20 / 3:14 / 5:1 / 6:1 / 10:1-7 / Sura ya 17